YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

Nafaka inaonyesha una upeo mpana kuhusu kazi za kimtandao...hongera!

Ili kuwasaidia vijana wenzio hebu fungua darasa fupi ili wapate mwanga( basic) jinsi kufanya na taratibu zake.
Mf. ukusanyaji wa hizo data za lugha na utaratibu wake.

Ukifanya hivyo utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kwa hiki kizazi na kuliweka jina lako kwenye kumbukumbu ya wengi.
Mkuu, kwanza watu wana msemo humu ukiitwa kwenye fursa jua wewe ndio fursa. Una ukweli kwa 80% na hivyo kutokana na hilo ndio maana kuna watu wengi wanafahamu mambo ila wanakaa kimya wasije itwa matapeli.
Pia kama madarasa yapo mbona watu wanakutana kila mara yakiongozwa na baraka mafole watu wanakutana na kushare vitu huko. Mimi sijawahi kwenda ila nina appreciate baraka anachikifanya maana watu wameanza yamefanya toka 2014 ila baraka ndani ya miaka miwili ya harakati zake hizi kafanya wengi wajue kuhusu pesa mtandaoni.
So mkuu watu wajiunge huko kwenye magrup na kuhudhuria ma event.
Halafu mimi shida huwa sio mwalimu mzuri pia.
 
Yes, asikwambie mtu.

Blogging na YouTube siyo kazi rahisi hata kidogo.

Labda uwe mtu maarufu, uwe unwaelekeza waasi wako ulionao kwenye social media kwenda kwenye channel yako.

Vinginevyo, uwe na content unique sana ili channel iweze ku-blow up haraka
Hivi facebook si inalipa watengeneza contents siku hizi
 
Wakuu mambo vipi?

Ni muda mwingine tumekutana tukiwa salama kabisa, ila poleni sana kwa wale mnaopitia changamoto kinamna yoyote ile na ninawaombea muweze kurudi katika utimamu.

Wakuu, uzi huu leo naupitisha katika sindano ya YouTube.

Mimi nimekuwa YouTube Creator it's about 10yrs now, and I know YouTube as well. Nimeshachukua pesa za Youtube mara nyingi sana, that time nilikuwa nachukua pesa kupitia 'Western Union' kabla YouTube hawajaitoa na kubakisha 'Wire transfer'.

Siku hizi vijana wengi wameajiriwa na YouTube. You make money depends on what you're doing.

Kwa hapa Bongo neno linaloshika sana na linalomshawishi mtu naye aweze kuwa YouTube Creator, ni "Youtube inalipa".

Binafsi mimi huwa sipendi kulitumia neno hili kwa sababu najua challenges zilizo kwenye YouTube.

Kibongo bongo hapa ukisikia mtu anakuambia anapiga hela YouTube hapo usikubali moja kwa moja.
Kuna watu wanaficha aibu. Unakuta miezi 6 ndio anapata $100, halafu anasema eti anapiga hela. Seriously, hii haisound poa.

Kiukweli, ili upige hela za YouTube lazima utengeneze unique contents halafu ziwe kwenye moja ya lugha zilizotajwa kwenye Adsense na sio kiswahili. Kingine ukitaka YouTube chaneli yako iwe na matangazo yenye CPC (Cost per click) kubwa, lazima contents zako ziwe zinazungumzia mambo ya pesa.

Mfano: Buy, Sell, Credit, Money, nakadhalika. Hizi zinakuwa na CPC kubwa kuanzia $10 kuendelea. Hapo utakuta unapiga $20 kwa siku. Lakini kama contents zako ni za kiswahili, sahau hilo, kwa sababu 'Kiswahili' ni miongoni mwa lugha ambazo hazijatajwa kutumika kwenye Adsense.

Mara nyingi kwa wastani chaneli yenye contents za kiswahili 'cpc' yake huchezea kwenye $0.01 au $0. Ikipanda sana ni $0.03 inategemea upepo wa contents za siku hiyo.

Mfano, una video moja kwenye chaneli yako imepata Views 30,000 watu 100 wakabonyeza matangazo, hapo utakuwa umeingiza $1 au $1.5.
Youtube hawalipi kwa views, wanalipa kwa watu waliobonyeza matangazo na sio kila video inaweza kuwekewa matangazo. Unaweza ukaona video ya mtu ina Views Milioni 3 lakini asiwe amefaidika chochote.

Lakini tukihamia upande wa pili wa lugha na aina ya contents kama nilivowaeleza hapo juu, hapa unaweza piga pesa ndefu kwa sababu cpc kwa wastani inachezea kwenye $2 per click.

Mfano una video ina views 30,000 na watu waliobonyeza matangazo ni 100, chukua hiyo $2 zidisha kwa hao watu 100, ambapo ni sawa na $200. Hii ni pesa ndefu! Kama ukiwa na unique contents za kutosha kwenye chaneli yako, hapo maisha ni mtelezo tu.

Narudia teena 'Youtube inalipa hila sio hapa Bongo'. Na ukikuta mtu anakuambia anapiga hela Youtube na yupo hapa bongo na contents zake ni za kiswahili tena ni za kusimulia, mwambie akuoneshe Adsense ama YouTube Dashboard asikudanganye kirahisi. Bora hata za muziki zinalipa kidogo.

Na hii ni kwa hata wale ambao Tovuti au Blog zao ziko monetized na Adsense. Wembe ni ule ule! Tena kule kwenye site, ukiwa unapost kwa kiswahili, unaondolewa kabisa matangazo.

Ahsanteni wakuu; Kama utapendezwa na elimu zaidi, napatikana kupitia deoperacc kwenye mitandao ya kijamii. Huwa si mpenzi wa kupost sana kule ila unaweza uka -DM tu.
Nahitaji kumiliki You Tube channel
 
Wahindi ukifanya nao kazi mtandaoni wanabana sana aisee wale halafu wezi wanawaibia hadi wahindi wenzao wanawafanyisha kazi halafu hawawalipi
Yes, Wahindi ni janja janja sana.
 
Mimi ni YouTuber pia...lakin natumia kingereza tu.

Uliyosema ni kweli...

Unahitaji elimu ya kutosha kuhusu Youtube kabla ya kuanzisha channel ya youtube...


All in all Kupata views nyingi ni kitu cha muhumu sana kabla ya yote
Voice over unatumia sauti yako au una-outsource?

Video editing software gani unatumia?
 
Mimi ni YouTuber pia...lakin natumia kingereza tu.

Uliyosema ni kweli...

Unahitaji elimu ya kutosha kuhusu Youtube kabla ya kuanzisha channel ya youtube...


All in all Kupata views nyingi ni kitu cha muhumu sana kabla ya yote
Kabisaa!
 
Yani kama msanii akifikisha views 1000 basi anaingiza $3 ..sasa apo piga hesabu mufano wamefika viewers Million 1,2,3,10,50,100 viewers billion 1,2,3 ...
FD05D091-3E66-4155-B81C-7A4ECCEB29AD.jpeg


Naomba nieleweshe na hapa mkuu

Cc instanbul deoperacc
 
Back
Top Bottom