YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

Hawa wakenya wanakula 30-40% ya gross income na wamesaidia kuboost YouTube channel za Wasafi, Barnaba na wengine na pia kuna watanzania walikuwa wanafanya kazi hapo wakaja kufungua kampuni kama Slide Digital na SmileSasa.
Kwa sasa muziki umekuja kulipa sana kwenye Digital platforms, sync licensing pamoja na publishing
Ndio, kwa sababu wao tayari ni YouTube partner, na ni contents id manager.
 
Nimepitia jalalani nimejifunza vitu vichache ili utoboe youtube wanazingatia mambo mawili makuu demographic na content.
~ndugu joel nanauka ana silver youtube creator award (naona content hapa ndio imembeba)
~Nas daily bussiness (ukiwachimba kwa ndani kuna mengi ya kujifunza
~marketing knowledge and strategies ni muhimu

N.B:wabongo tunapuuza kusoma deep then tunategemea matokeo mazuri.
 
Ni kweli mkuu. Kuna mtu anaanzisha YouTube Channel hata policies hajasoma, yeye anachoangalia ni dola tu. Kwenye YouTube ukiwa contents creator mzuri halafu ukawa mbunifu, YouTube inakupaisha wala huwezi kufanya kazi nyingine.
 
  • Thanks
Reactions: Sax
Wakuu mambo vipi?

Ni muda mwingine tumekutana tukiwa salama kabisa, ila poleni sana kwa wale mnaopitia changamoto kinamna yoyote ile na ninawaombea muweze kurudi katika utimamu.

Wakuu, uzi huu leo naupitisha katika sindano ya YouTube.

Mimi nimekuwa YouTube Creator it's about 10yrs now, and I know YouTube as well. Nimeshachukua pesa za Youtube mara nyingi sana, that time nilikuwa nachukua pesa kupitia 'Western Union' kabla YouTube hawajaitoa na kubakisha 'Wire transfer'.

Siku hizi vijana wengi wameajiriwa na YouTube. You make money depends on what you're doing.

Kwa hapa Bongo neno linaloshika sana na linalomshawishi mtu naye aweze kuwa YouTube Creator, ni "Youtube inalipa".

Binafsi mimi huwa sipendi kulitumia neno hili kwa sababu najua challenges zilizo kwenye YouTube.

Kibongo bongo hapa ukisikia mtu anakuambia anapiga hela YouTube hapo usikubali moja kwa moja.
Kuna watu wanaficha aibu. Unakuta miezi 6 ndio anapata $100, halafu anasema eti anapiga hela. Seriously, hii haisound poa.

Kiukweli, ili upige hela za YouTube lazima utengeneze unique contents halafu ziwe kwenye moja ya lugha zilizotajwa kwenye Adsense na sio kiswahili. Kingine ukitaka YouTube chaneli yako iwe na matangazo yenye CPC (Cost per click) kubwa, lazima contents zako ziwe zinazungumzia mambo ya pesa.

Mfano: Buy, Sell, Credit, Money, nakadhalika. Hizi zinakuwa na CPC kubwa kuanzia $10 kuendelea. Hapo utakuta unapiga $20 kwa siku. Lakini kama contents zako ni za kiswahili, sahau hilo, kwa sababu 'Kiswahili' ni miongoni mwa lugha ambazo hazijatajwa kutumika kwenye Adsense.

Mara nyingi kwa wastani chaneli yenye contents za kiswahili 'cpc' yake huchezea kwenye $0.01 au $0. Ikipanda sana ni $0.03 inategemea upepo wa contents za siku hiyo.

Mfano, una video moja kwenye chaneli yako imepata Views 30,000 watu 100 wakabonyeza matangazo, hapo utakuwa umeingiza $1 au $1.5.
Youtube hawalipi kwa views, wanalipa kwa watu waliobonyeza matangazo na sio kila video inaweza kuwekewa matangazo. Unaweza ukaona video ya mtu ina Views Milioni 3 lakini asiwe amefaidika chochote.

Lakini tukihamia upande wa pili wa lugha na aina ya contents kama nilivowaeleza hapo juu, hapa unaweza piga pesa ndefu kwa sababu cpc kwa wastani inachezea kwenye $2 per click.

Mfano una video ina views 30,000 na watu waliobonyeza matangazo ni 100, chukua hiyo $2 zidisha kwa hao watu 100, ambapo ni sawa na $200. Hii ni pesa ndefu! Kama ukiwa na unique contents za kutosha kwenye chaneli yako, hapo maisha ni mtelezo tu.

Narudia teena 'Youtube inalipa hila sio hapa Bongo'. Na ukikuta mtu anakuambia anapiga hela Youtube na yupo hapa bongo na contents zake ni za kiswahili tena ni za kusimulia, mwambie akuoneshe Adsense ama YouTube Dashboard asikudanganye kirahisi. Bora hata za muziki zinalipa kidogo.

Na hii ni kwa hata wale ambao Tovuti au Blog zao ziko monetized na Adsense. Wembe ni ule ule! Tena kule kwenye site, ukiwa unapost kwa kiswahili, unaondolewa kabisa matangazo.

Ahsanteni wakuu; Kama utapendezwa na elimu zaidi, napatikana kupitia deoperacc kwenye mitandao ya kijamii. Huwa si mpenzi wa kupost sana kule ila unaweza uka -DM tu.
hatukujua ni muda wa wasomi kuanza kutengeneza mitandao yao
 
Inawezekana vipi kufanya hii biashara hapa bongo mkuu?
Ni businesses plans tu mkuu. Unaandaa proofs za uhakika, na records then unawasiliana na YouTube moja kwa moja. Hapo unaweza kuwaambia unataka kujiunga na YouTube's Contents Managing System (CMS). Nadhani hao ndio wanaweza wakakupa muongozo positively.
 
Sawa mkuu, ngoja niifanyie kazi
 
Naomba kuchangia,

Mtoa mada ameongea mengi na mazuri japo kuna mengne mengi katudanganya kidogo kwa sababu amekuja na kauli ya kuwa you tube Hailipi hapa bongo, ki uhalisia sio kweli kabisa kabisa na mimi nasema kuwa YOU TUBE INALIPA saana kulingana na utakavyoijua, utakavyoamua kuitumia na utakavyoifanyia setting zako.

I know kwa mnaoijua you tube juu kwa juu mtaamini kuwa hailipi sababu kupata $100 tu ni kasheshe kweli kama alivyosema mtoa mada, lakini sasa kama unaijua vyema na jinsi ya kucheza nayo utapiga hela swaafi kabisa.

mimi nimeanza mambo ya you tube nina miaka kama mi 4 tu na nimekuwa nikiuza sana chanela zangu pale inapotokea mtu akifika bei nzuri (sababu ya njaa) nadani ya hii miaka 4 nimeuza chanel zinazoingiza pesa zaidi ya 5, na sasa ninazo chanel 2 tu, moja inaingiza $ na haina haya mwaka bado na nyingne ipo pending sijaombea matangazo, hii nayotumia ina sub 5.8tu. lakini huwa naingiza mpaka $200+ kwa mwezi na hapa navyoandika sijaweka content nazaid ya miezi 3.
Nashahuri kufanya tafiti, kujifunza sana pale unapotaka kuingia katika industrial za Social Network.

mnaweza kuangalia accout yangu moo entertainmenttz hii accout inalipwa kuliko mwenye accout za sub30k.

hapa nime attach YT dashbod yangu ya leo kuona na hii ni 28day pekee

NB: nakuza pia accout zote za social Medi, instagram Tik tok, Facebook twiter na nyingnezo (tangazo baada ya maelezo na habari)
 
Attachments

  • Image 2023-02-21 at 9.03.41 AM.jpeg
    Image 2023-02-21 at 9.03.41 AM.jpeg
    29.7 KB · Views: 37

Know that, you can't earn more kwa kutumia swahili contents. I used Bongo nikimaanisha swahili.
 
Acha kuwakatisha watu tamaa

Hakuna mtandao Kama YouTube katika malipo

Ukiwa na 400hrs
Na subscribe 1k unaanza kuchukua $200 at the first time

YouTube wanalipa vizuri Sana Tena sana
Wewe ni YouTuber ?
Au umeamua kuropoka , ili ufurahishe wajinga wenzako na uonekane unajua?
 
Back
Top Bottom