Yoweri Museveni Rais wa Uganda amepiga marufuku Mitumba. Amesema ni Nguo zilizoachwa na Wafu wa Ulaya

Yoweri Museveni Rais wa Uganda amepiga marufuku Mitumba. Amesema ni Nguo zilizoachwa na Wafu wa Ulaya

Tatizo siyo kupinga. Tatizo ni uzalishaji, bei za bidhaa hizo na umasikini. Ndiyo inafanya nguo za mitumba hazina soko.
Uzalishaji ukiwa mkubwa watu hawatangaika na mitumba. Na pia maisha ya watu yakiboreshwa (kupunguza umasikini).
Hapa Tanzania kuna majiko ya gesi na umeme lkn kuna watu bado wanatumia mkaa na kuni. Unafikiri kwa nini?
Mtu na pesa zako unaweza kununua mtumba?
Majiko ya China, mobile phone, electonics nyingi tu zinalipuka. Viatu vya China baada ya siku mbili soli inatoka.

Liwe lengo, iwekwe mikakati, viwanda vijengwe kutosha matumizi ya ndani bei ziwe rafiki.

Viwanda vingi vilikufa kwa kukosa soko Tanzania kutokana na ushindani Mwatex, urafiki, nyumbu siini magari yao mtaani.
 
Ni idea nzuri.
Lakini kabla hatajaiga walichofanya ni busara kama tutahakikisha tunazalisha nguo za kutosha na zinazo kidhi mahitaji ya makundi yote ya watanzania.

Huo uzalishaji kwa sasa haupo.

Inabidi tuwapatie wauza mitumba alternative endapo tutakataza mitumba.
Yep ajira kwenye hivyo viwanda vya uzalishaji.
 
Ila mitumba inavalisha watu wengi xnaa na pia kutoa ajira kwa vijana wengi mno.sidhani kama ni busara kuifungia
Wengine hapa, wanaongea kishabiki tu! Wakati nakua mimi, kukutana na mtoto mwenzio matako nje, lilikuwa ni jambo la kawaida tu. Leo hii mama, anaenda mitumbani na 5,000/= tu, anakuja na nguo za watoto 6.
Nyie muwezao kununua nguo, viatu SPESHO, nunueni! Sie WALALA HOI, mtuachie MITUMBA yetu! Shukraan sana SALIM AHMED SALIM!
 
Rais Museven amepiga Marufuku Nguo za Mitumba kuingiza nchini mwake akidai Hizo ni Nguo za marehemu Wazungu

Hapa Bongo Sidhani kama angeeleweka 😂😂😂

Source: Kitenge tv

Nawatakia Sabato Njema 😄
Museveni ni takataka,wananchi wana uwezo wa kununua ngua mpya dukani? Linazeeke vinaya stupid
 
Wabongo mtumba sahv unatoka China,ule UK na Canada siyo sana

Ova
Huo mtumba unanunuliwa Europe, Ulaya, USA unasafishwa na kupangwa unaletwa Afrika kwa mabelo, container, nguo za watoto, wanawake, wanaume, jeans.

China bado wanavaa nguo zao hadi zichakae kabisa kama Waafrika na wahindi.
 
Rais Museven amepiga Marufuku Nguo za Mitumba kuingiza nchini mwake akidai Hizo ni Nguo za marehemu Wazungu

Hapa Bongo Sidhani kama angeeleweka [emoji23][emoji23][emoji23]

Source: Kitenge tv

Nawatakia Sabato Njema [emoji1]
Wakati wa Waganda kuanza kuvaa viraka umefika Rasmi
 
Nimekwambia pale juu kuwa una huruma na uwezo mdogo wa mlala hoi ila huna huruma ya kumtoa hapo alipo.
Kwa maelezo yako nianavyo ni kuendelea kumfanya mlala hoi awe na uwezo mdogo wa kununua .
Mvaa mitumba ameathiliwa na uwepo wa mitumba. Mitumba inamsaidia hapo hapo unamdumaza kiuchumi mara 3 zaidi.
Mkulima wa pamba ambae angeuza pamba yake kwa bei nzuri kiwandani angeweza kununua nguo mpya.
Muuza mitumba angefungua duka la kuuza nguo mpya badala ya mitumba.
Mshona nguo angepata order nyingi zaidi kwenye kampuni za kuuza nguo.
sekta ya logistic ingekuwa zaidi kwa mzunguko wa uzalishaji nguo, export ingekuwa kubwa zaidi na kutusaidia kupata dola ambayo tungeitumia kununua heavy duty textile machine( huu ni mlishano wenye tija ya kumuinua mlala hoi)
Miitumba imeua huo mzunguko wote kwenye sekta ya nguo, ni vipi mlsla hoi atainuka?.
Mfano hapa nilipo tunalima viazi mviringo. Bei ya viazi inapokywa juu kila myu anapata nguvu ya kununua, na inaposhuka kila mtu anauwezo wa kuvila viazi na kusaza ila hakuna mwenye hela kila mtu anakuwa masikini. ndio case ya mitumba
Mitumba inatengeneza vicious cirle ya umasikini mbaya sana si utajiri na kujikomboa.
Masikini mmoja anaongeza umasikini kwa mwenzie. Wanaonufaika kwenye mitumba ni wahindi, wazingu na madalali wachache.
Twende kwenye vuwanda vya nguo kila kitu kitajurekebisha chenyewe, tupo ktk karne ya sayansi na teknolojia uwekezaji ndio kila kitu.
Hakuna atakaetembea uchi.
Tukizungumzia kiwanda hatuzungumzii tu wafanyakazi wa mle kiwandani.
Kiwanda kinaanzia kule malighafi ilipozalishwa mpaka kuwa bidha.
Mimi siangalii kiwanda kwa maana ya wafanyakazi, hao ni sehemu ndogo sana ktk industrislization.
Ngoja nikupe mfano mdogo sana unajua viwanda vingi na vikubwa vya Nike vipo nchi gani ? Na hizo nchi ndio wavaaji wakubwa wa hizo Nike au zinapelekwa sehemu yenye watu wenye buying power kubwa ? Viwanda vya Nike vingi vipo Asia Why ? (Cheap Labour)

Unadhani kwa gharama ya hii nishati nchi hii hata kama tungekuwa na nguvu ya marketing, distribution n.k. tunaweza tukatengeneza vitu cheaply ? Ofcourse wanajaribu kina A to Z na Sunflag, lakini bado hata kwa hapa nchini pricewise ni gharama ya juu....

Tatizo kubwa katika hii equation ni watu hawana buying power, na kubadilisha hilo inabidi kufanya revamption ya hali ya juu na ufanyaji huo wa revamption hauanzii kwenye kupiga marufuku wakati soko lako halijitoshelezi wa quantity wala quality....
Bro hakuna TRANSFORMATION/ TRANSITION isio na gharama.
BRICKS wanataka kuondoka ktk utumwa wa DOLLAR, je wakatae kisa kuna mambo watayakosa? Unadhani kwamba BRICKS kuna vitu hawatavikosa ?
Kama wenzetu wanatoka kwenye jambo kubwa la kutegemea DOLLAR sisi ni nani tushindwe jambo dogo la nguo !
Kwahio Brics walipiga marufuku dollar wakati hawana alternative ya pesa, au unadhani watapiga marufuku dollar au watawapa alternative watu ?
Kuhama kutoka kwenye mitumba nalo ni kubwa sana kama tukisema sasa mitambo na madawa ya west bas ?
Kama tu tunapingana kutoka katika mitumba tunaweza kukubaliana kujitegemea sekta kubwa kubwa mfano military, medicine nk.
TRANSFORMATION ina gharana zake but in long run it is fruitful!
Na aliyokukata kufanya hayo ni nani ? Fanya na hata ikibidi uza nje watu wanunue sio ndani tu The world is your oyster, ila sio nyumbani kwako badala ya kuhangaika kuweka shamba na kulima mahindi unapiga marufuku watoto wako wasiende kununua mahindi kwa jirani hivyo wanakufa njaa, There is a practical way and political way of doing things one is sustainable na nyingine ni kujazana ujinga
Noipo tiyari kuvaa magome iwapo yu bionhozi wangu wataonesha nia ya kweli.
Nwabafalsafa nguli wa kiafrika MALCOM X
aliongekea
HOUSE NEGRO
FIELLD NEGRO.
Unadhani hayo magome ya miti ni cheaper ? Siongelei quality pekee bali na affordability na watu kupata moja ya basic needs unaongelea used clothes hivi unajua hata USA na UK kuna maduka ya Second Hand Clothes ?


Huoni unatuhamasisha kuendelea kywa HOUSE NEGRO oli tuke makombo ya mzungu.
Kwa nini karne ya 21 uwe HOUSE NEGRO?
Bto viongozi wetu gawajatai mutumba kwa sababu haitusaidii bali jwa sababu inatudhalolisha na kudololesha UCHUMI WA NCHI.
Kwahio msaada ni kupiga marufuku hizo nguo ambazo ni bei rahisi kwa watu badala ya kuhakikisha kuna viwanda vya ku-compete na hizo bei au alternatively kukuza kipato cha watu ?
Kumbuka hapa hatuzungumzii mimi na wewe, tunazungumzia jamii tunazungumzia Africa. NEO AFRICANISM!
Umesoma nilichokuandikia hapo juu nimekupa jinsi ya kuondokana na umasikini na ubangaizaji kwa dhamila ya kweli..., usidhani kama ukipaga marufuku watu wasile mkate basi watakula keki..., kama kipato chao ni kidogo watu hawa watakunywa chai tupu
Nje ya mada :
Halafu nyie wachumi mbuni mbinu zinazoendana na mazingira yetu, theory za wazungu mnazonukuu zimefeli kufanya kazi hapa Afrika ndio maana tunaendelea kuwa na mataifa masikini na wachumi wamejazana tu na kuzipotosha serikali zetu.
Ndio maana raisi JPM aliwapuuzia mbali akafanya mambo yske ba yakaenda.
WARABU,WACHINA hawajatumia theory za wazungu kuinua UCHUMI wao bado nchi zao zina excel. Wanathibitisha kuwa tunaweza endelea bila theory za hao wazungu.
Nani mchumi ? Yaani kuona haya mambo lazima uwe mchumi unaongelea wachina na waarabu ngoja nikue list ya most countries wanaoagiza mitumba....

Imports In 2021, China imported $49M in Used Clothing, becoming the 38th largest importer of Used Clothing in the world. At the same year, Used Clothing was the 800th most imported product in China.

In 2021, the top importers of Used Clothing were Ghana ($214M), Pakistan ($180M), Ukraine ($177M), United Arab Emirates ($173M), and Kenya ($169M).
 
Hii safi sana.

Nimelikemea hili na nimeliponda kwa miaka mingi sana.

Waafrika wote tupige marufuku mitumba yote. Ya nguo, ya magari, ya nafriji na kila kitu.

Ndipo tutakapoweza kufanya vyetu wenyewe.

Hapa namuunga mkono Museveni 100%.
Sasa magari Bibi tutaweza kumiliki gar Kweli ist jipya c itakiwa milioni 45
 
Cha kujiuliza nguo zinapatikana kwa bei nafuu? Tunapenda, mitumba, kwa vile ni nafuu,
Kingine sio kweli kwamba nguo za mitumba ni za wafu,
Kwa wenzetu nguo wakishazitumia, huziuza, ni swala LA kawaida,
Huyo Museveni aseme tangu 1984! Amefanya nini cha maana kwa nchi ya Uganda, na anaplan gani baada ya kuondoka,
 
Hii safi sana.

Nimelikemea hili na nimeliponda kwa miaka mingi sana.

Waafrika wote tupige marufuku mitumba yote. Ya nguo, ya magari, ya nafriji na kila kitu.

Ndipo tutakapoweza kufanya vyetu wenyewe.

Hapa namuunga mkono Museveni 100%.
Kama hayumo kwenye AGOA atafanikiwa. Jiwe Mwamba Magufuli alijaribu, lakini Mkataba wa AGOA ulimbana.
 
Nani mchumi ?
Basi nikuite tu mkereketwa wa nadharia za kimagharibi
Theory za kiuchumi za kimaghatibi zimefeli kitambo hapa kwetu, utaishia kunukuu nikuu hakuna unachoweza onesha kama mfano wa mafanikio wa hizo nadharia.

Kuhusu China kuagiza mitumba ulaya inawezekana ila hawategemei mitumba kama sisi na wanazalisha matani ya nguo ambayo Fred vunja bei anatuletea hapa kwa bei poa walau kupoza dharau za malonya.

Unatakiwa ulete suluhisho sio mtanziko.
Sisi tunazumgumzia kuchechemua viwanda viwakomboe watu waache kuvaa mitumba, wewe unazungumzia kiwanda cha kuchuuza waste product from USA kumpa ahueni ya muda mnunuzi. Kuna vitu vinaletwa huku mpaka unajiuliza waliobeba walikuwa timamu, ni uchafu! uchafu!
Nimalize mjadala kuwa wewe unaangalia leo, mie naangalia kesho. Kwa hio hatuwezi kukubaluana. Ila naamini Mseveni tayari atakuwa ameisha tuacha hatua kumi mbele. Ameishawaokoa wakulima wake wa pamba . Atawasaidia waganda kuijua sekta ya nguo inavyooendeshwa na anaweza ku export kupata Dolla huku sisi tukiendelea kuchoma Dolla kuagiza malonya.

Ninasema malonya kwa sababu masokoni yamejaa malonya kuliko hizo grade unazozipigia upatu.
Sikatai mitumba kwa sababu haitusaidii bali kwa sababu inadumaza, akili, uchumi na kuleta dharau kutoka kwa waliotuletea.
vilevile inachafua mazingira
Nitasimama kama mwafrika anaependa kuona utu wake unakuwa sawa na wa wengine.
Nje ya mada
Nimpongeze mchina walau ameonesha njia kwenye vifaa vya electronics hata kwenye nguo itawezekana. Sasa ma TV, Redio ya mtumba yamepungua sana.
 
Nashangaa watanzania wenzangu mnaosema tutengeneze vya kwetu eti mtumba haufai..!!. Hizi nchi zetu bado sana kuweza kukataa mtumba. Kabla ya kujimwambafy tujitajidi tuwe na umeme wa uhakika, sera na sheria rafiki kuhusu viwanda bila kusahau kodi. Kikubwa zaidi tufikirie kwa undani pa kuwapeleka kundi kubwa la vijana lililojiajiri kwenye mtumba.

Mimi ninashauri kama umeme wa bwawa la nyerere ukiwa tayari vianzishwe viwanda vitakavyotengeneza nguo na kuuza kwa bei nafuu ili biashara ya mtumba ijifie taratibu.
 
vilevile inachafua mazingira
Ili kuepuka mazungumzo marefu ngoja nichukue point yako moja tu, ili nikuelimisha unaongelea mazingira ?!!! Hivi unajua katika vitu vinavyoharibu mazingira nguo / fashion na overproduction ya hivyo vitu ni uharibifu mkubwa wa mazingira ?, Kwa taarifa yako mitumba inasaidia mazingira sababu nguo zinakuwa recycled / reused....

Kuna mpango wa watu kurecycle fibres sababu hio cotton kuanzia umwagiliziaji, kutumia mbolea na dawa za kuulia wadudu ni uharibifu mkubwa wa mazingira..., nikupe taarifa tu kwa ufupi hayo mengine naona najirudia rudia (sijui ni wapi nimesema watu wasivae nguo mpya au viwanda visifanye kazi..., nimekwambia na narudia tena nimesema hakikisha kuna quantity, quality na affordable prices kabla haujaondoa mbadala kwa watu...
 
Back
Top Bottom