Hivi bado kuna watu wanaamini EA radio itakufa kwa kuondoka mtu? ....Naamini wengi humu mna miaka si zaidi ya 10 kusikiliza radio seriously ....wengine tumeona vizazi kibao vya radio zetu hizi za FM toka zinaanza ....Hao EA radio ndio walivyo toka enzi za akina Bashiru Mohammed ....wanazalisha vipaji vya watangazaji na DJs ....DJs waliotikisa nchi hii wengi wamepita pale toka DJ JD, DJ Habib, DJ Rico, DJ Steve B ,DJ Mackey, DJ Ray C (Rehema Chalamila) , DJ Too hot na huyu mnayemjua wengi wa kizazi hiki ...DJ Mafuvu ...pale hapafi ...ni bandika bandua ....