Yuko wapi Charles Jangalason?

Yuko wapi Charles Jangalason?

ZVI ZAMIR

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
921
Reaction score
2,163
Huyu Mtumishi wa Mungu aliekuwa akihudumu zaidi katika uimbaji nyimbo za injili ...alikuwa akisikika sana siku za nyuma na nyimbo zake zilikuwa na mafundisho mengi sana sio tu kwa watu walimpokea Bwana Yesu ila na wale ambao bado hawajampokea.

NYIMBO ZAKE:
Malaya wameoza
Dungwa sindano.
kila mtu ana kwao.
Ulevi ni pepo.
Dawa ya ndoa.
Na nyimbo nyingine nyingi aliimba..Wadau wa Mziki wa injili haswa wale wa kuanzia miaka ya 2007 kurudi nyuma mtakuwa mnamkumbuka. Naomba mnijuze na muwazuje wadau juu ya huyu Mtumishi wa Bwana.
 
Kuna wimbo wake enzi hizo uliitwa Kanyumba kadogo. Niliupenda Sana huo wimbo. Watoto wanakufa njaa sababu ya Kanyumba kadogo.
 
Huyu Mtumishi wa Mungu aliekuwa akihudumu zaidi katika uimbaji nyimbo za injili ...alikuwa akisikika sana siku za nyuma na nyimbo zake zilikuwa na mafundisho mengi sana sio tu kwa watu walimpokea Bwana Yesu ila na wale ambao bado hawajampokea.

NYIMBO ZAKE:

Na nyimbo nyingine nyingi aliimba..Wadau wa Mziki wa injili haswa wale wa kuanzia miaka ya 2007 kurudi nyuma mtakuwa mnamkumbuka. Naomba mnijuze na muwazuje wadau juu ya huyu Mtumishi wa Bwana.
Bila kumsahau Pastor KYANDE huyo alikua ni moto sana
 
Bila kumsahau Pastor KYANDE huyo alikua ni moto sana
Wachungaji
Maisha ya wawili
Israel waliteseka
Nabii hana hesima kwao
Nani kasema
Waganga wa kienyeji (huu wimbo nimeutafuta sana siupati)

N.k

Hawa ndio walikuwa wanasimamia kile wanachohubiri, sio hawa wa fuata maneno yangu usiagalie matendo. Washenzi wakubwa, unawezaje kuwalazimisha watu wafanye kile kilichokushinda?
 
Back
Top Bottom