Huyu jamaa alikuwa 'shortsighted'. Wenzake aliotumwa nao walikuwa wataratibu sana yeye kimbelembele. Sasa leo Nape kateuliwa tena kwenye Ile nafasi.
Pia Nape asingekuwa wazir tena leo kama asingejishusha na kunyenyekea kwa Jiwe siku ile akitembeza huku akirekodiwa jasho likimtoka magogoni. Jiwe angempoteza kabisa na ubunge asingeupata tena.
Siasa za Tanzania siyo burudani tu bali tunajifunza jinsi maisha yalivyo.
Mrisho Gambo naye namsifu Sana. Alishaanzaga za kibashite bashite baadaye akashtuka akawa anaenda taratibu.
Sasa sijui huyu Hapi atapona kwa mshika remote? Labda 'imani' yake huenda ikamuokoa.
Hadi kuna siku Prince aliongea kwa hisia sana aliposema yani jamaa walimtoa shimoni wakaweka kwenye spotlight baadaye kawageuka. Namsifu sana huyu msomali Bashe licha ya figisu Mshika remote na mzee makamba walimfanyia dhidi yake wakamchomeka Kigwa Nzega jamaa alitulia tu . Aliamua kucheza karata zake vizuri.