Najaribu kufikiria. Kuna wanaosema hii bado ni awamu ya 5 part 2 inayomaliziwa na co-pilot (captain ad interim) baada ya captain kuzimika ghafla angani. Polepole anasimamia hoja hii na bado hajafikishwa hukumuni.
Lakini aliyekuwa co-pilot keshatuaminisha kuwa hii ni part 1 ya awamu ya 6 na yeye ndiye captain mpya kamili. Hivyo, 2025 atastahili form 1 ya peke yake kuingia part 2 kama desturi ya CCM inavyotaka.
Baada ya hapo inawezekana wataalamu mahiri wa sheria wakaibuka na nguvu ya hoja kusahihisha kosa “la kikatiba” lililofanyika kwa bahati mbaya na kurejesha ukweli wa Polepole kuwa 2025 ndipo awamu ya 5 inapoishia na part 1 ya awamu ya 6 kuanza.
Wenye chama, “any objection?”
Mkitoa pingamizi nikiwa judge natoa tu kiroho safi: “overruled”!