mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Hebu tutupie hapa mchango wake kwenye siasa na maendeleo ya nchi yetu!
Kikubwa ninachokikumbuka ni uthubutu wake wa kusimamia uletaji wa maji Dodoma toka ziwa victoria. Haikuwa rahisi!! Ilibidi kuvunja mikataba ya kimataifa iliyokuwa inazuia kuvuta maji toka ziwa victoria! Uthubutu wake uliwezesha jambo hili. Leo Jiji la Dodoma ni full kijani kibichi, si jangwa tena! Vijana wengi hawalijui hili kuwa hizo ni juhudi za Lowasa!!
Usafiri Dar-es- Salaam (UDA), ni juhudi za Lowasa!! Kulikuwa na mabasi mengi yaliyokuwa yanahudumia usafiri Dar-es-Salaam. Bei ya nauli ilikuwa shilingi moja (01). Baada ya kuonekana kuwa hayo mabasi ya UDA hayakutosheleza mahitaji ya usafiri wa Dar, wenye mabasi binafsi walikuwa wanabeba watu kwa shilingi tano (5) au Dala!! Shilingi 5 kutokana na umbile lake/shape yake ilikuwa inaitwa dala, na mabasi yale yalikuwa yanatoza shilingi tano tano yaani dala dala. Lakini ilikuwa ni kinyume cha sheria maana hiyo bei ya shilingi tano haikuwa rasmi, ni ukiukaji wa sheria zilizokuwepo na matrafiki walikuwa wanawakamata na kuwasumbua. Hapo ndipo namkumbuka tena Lowasa, alipohalalisha hayo mabasi ya watu binafsi na kuhalalisha hiyo bei ya dala dala. Wenye mabasi hayo wakafanya kazi bila usumbufu na likawa suluhisho kwa tatizo la usafiri Dar enzi hizo. Hicho ndiyo chanzo cha mabasi yanayoitwa dala dala hadi leo, japo nauli si dala tena!! Hayo ni machache miongoni mwa mengi!! Tujifunze kuwaenzi wazee wetu wakiwa wangali hai, hiyo itawaongezea miaka ya kuishi!! Karibuni hapa tueleze mchango wa Lowasa kwenye nchi yetu!!