Yuko wapi Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango?

Yuko wapi Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango?

Kama Mtanzania mpenda Viongozi wangu na Utendaji wao mzuri naomba Kujulishwa yuko wapi Makamu wangu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Nikimwona Uwanja wa Uhuru Keshokutwa ( Alhamisi ) katika Siku ya Uhuru wetu GENTAMYCINE nitakuwa ni mwenye Furaha na nitajitahidi 'nipenyepenye' mpaka nikamsalimie Mtani wangu wa Kiha kutoka kwa 'Washamba' Mkoani Kigoma.

au kama yupo ( tunae hapa JamiiForums ) tafadhali naomba ajitokeze tu anijibu kuwa yuko na anaendelea na Majukumu yake ili tu Roho yangu iridhike kwani 'nimemmisi' sana Makamu wangu wa Rais Dk. Philip Mpango.

Waha niambieni Ndugu yenu yuko wapi?
Ujio wa Nchimbi ambaye mwanzoni alitanabaishwa kuwa makamu..

uwepo wa inachosemekana Sgang, na Makamu wa sasa kuhusishwa..

kutokukubalika kwa makamu ndani ya team msoga (Wahuni vs Washamba/wakuja).

na mengineyo kama hayo kumefanya nguvu yake ipungue na kuna mkakati kabambe wa kumuondoa.

lakini ni mpe onyo/angalizo SSH.
Lolote litakalo fanyika kwa Mpango basi atalipiziwa mara 7 kwake.

kuna mission y chini chini inaendelea inawahusisha viongozi 3.
kama ikifanikiwa watanzania hawatakaa kuamini.

Niishie hapo.
 
Ujio wa Nchimbi ambaye mwanzoni alitanabaishwa kuwa makamu..

uwepo wa inachosemekana Sgang, na Makamu wa sasa kuhusishwa..

kutokukubalika kwa makamu ndani ya team msoga (Wahuni vs Washamba/wakuja).

na mengineyo kama hayo kumefanya nguvu yake ipungue na kuna mkakati kabambe wa kumuondoa.

lakini ni mpe onyo/angalizo SSH.
Lolote litakalo fanyika kwa Mpango basi atalipiziwa mara 7 kwake.

kuna mission y chini chini inaendelea inawahusisha viongozi 3.
kama ikifanikiwa watanzania hawatakaa kuamini.

Niishie hapo.

Acheni uzushi unadhani inaweza ikawa rahisi kiasi hicho?
 
Wewe 'Raia' hujuhi kitu, subiri taarifa uone meza zinavyopinduliwa.

kutoka kwa VP si lazima 'Kifo'
what if akasema ame resign??

viongozi wanapitia wakati mgumu sana, raia hawajuhi tu.
kuna kulogana na kufitiana.

IMG_8680.jpg

Masaa kumi na mbili yaliyopita alikua anachapa kazi na nimeongea nae kwa simu sio muda mrefu yuko salama salmin mimi ni raia mwenye akili
 
Wala usichukie kuambiwa mshamba na mtani wako, huyo watani zake ni waha, wanyiramba, wahaya, warangi, n.k amekuwahi tu ndio utamaduni hata angepita akakuta mnasafirisha maiti kwenda kuzika angekataa msiendelee akazua jambo kua alikua anamdai marehemu hivo lazima alipwe na mngempa pesa, na mkiwa msibani ninyi mnalia yeye anacheka wala haumfanyi kitu ndio utani mkuu au umekua juzi juzi.


Mtani akitaniwa je naye asijibu utani??---- wewe huoni hicho kicheko katika majibu yangu??!!, hicho ni kicheko cha utani tu isitoshe lini Kigoma ilikuwa ni nchi??!, hayo yote ni mambo ya utani tu,🤣🤣.

Wewe ndiye uliyezaliwa juzijuzi usiyejua jinsi utani unavyokolezwa.

Huyo Gentamycine ni Mzanaki na ndio maana ni mshamba kama Baba wa taifa alivyokuwa.🤣🤣🤣
 
Nahisi mda mwingi yupo ikulu kusaidia kazi za mama maana mama yeye mda mwingi anasafiri kutafuta wawekezaji
 
Makamu Wa Rais Afungua Kikao Nchi Wanachama Wa AU

MPEKUZI / 15 hours ago

[https://blogger]


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo desemba 6, 2021 amefungua kikao cha awali cha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika cha Jukwaa la Kujadili Masuala ya Usawa wa Kijinsia kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao. Kikao hicho kinachagizwa na kauli mbiu isemayo “Kuimarisha upatikanaji wa fursa kwa wanawake katika uongozi na nafasi za maamuzi ili kufikia ajenda ya Afrika tunayoitaka”.

Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Mpango Amesema mchango wa wanawake katika ukombozi wa bara la Afrika na hata baada ya kupata uhuru ni mkubwa bila kujali uwepo wao mstari wa mbele au mchango wao kwa waliopo mstari wa mbele. Amesema pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika ufanyaji biashara na kazi lakini bado bara la Afrika lina idadi ndogo ya uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi.

Aidha ameongeza kwamba ili kufikia ajenda ya “Afrika Tuitakayo” bara la Afrika linahitaji usawa katika uongozi, uwakilishi sawa katika masuala ya siasa pamoja na mazingira ya usawa katika masuala ya kijamii na kiuchumi.

Makamu wa Rais amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kwamba usawa wa kijinsia pamoja na uwezeshaji wanawake kiuchumi ni nguzo muhimu katika kufikia maendeleo endelevu kwa jamii yeyote ile ndio maana serikali imekua ikiingia katika mikataba ya kitaifa, kikanda na kimataifa inayohusu kuimarisha usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuimarisha uwezo wa wanawake katika uongozi na nafasi za maamuzi katika sekta zote za maendeleo.

Amesema Tanzania inaendelea kutekeleza ahadi zake ilizotoa katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) ambazo zililenga kukuza na kulinda haki za kiuchumi kwa wanawake.

Ameongeza kwamba kwa kutambua Elimu ndio msingi utakaowezesha kufikia malengo ya ushiriki sawa wa wanawake katika masuala ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni ikiwemo kuwawezesha wanawake kushiriki katika uongozi, serikali ya Tanzania tangu mwaka 2016 ilianzisha sera ya elimu bila malipo kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne pamoja na kuhimiza wasichana kusoma masomo ya sayansi kwa kuweka miundombinu itakayowawezesha ikiwemo ujenzi wa shule za sayansi maalum kwa wasichana katika kila mkoa.

Pia Makamu wa Rais amesema serikali imeondoa vikwazo vya umiliki wa ardhi kwa wanawake nchini Tanzania pamoja kuwawezesha kupata mikopo kutoka katika asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ili kuwawezesha kiuchumi.

Makamu wa Rais amesema ni muhimu nchi za Afrika kuendelea kuchukua hatua katika kuweka sera na sheria rafiki pamoja na kuwasihi viongozi wa Afrika kuweka mikakati itakayowezesha kutatua changamoto zote zinazokwamisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na nafasi za maamuzi.

Ufunguzi wa kikao hicho cha awali umehudhuriwa na Viongozi wa Juu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika , Wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yasio ya serikali. Kikao hicho ni maandalizi ya mkutano mkuu wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika Februari 2022.
Visit website
 
Hivi nyie Washamba Waha Watani zangu si mpo wengi tu hapa JamiiForums? Hebu niambieni upesi Mzanaki Mimi aliko Ndugu yenu Makamu wa Rais Dk. Philip Isidori Mpango tafadhali.

Kuna Shehena ( Consignment ) moja ya Corona ( UVIKO-19 ) nataka kuipeleka Mkoani Kwenu Kigoma na nataka Yeye ndiyo akaipokee kwani imetengenezwa 'Kienyeji' kutoka kwa 'Mashujaa' wa Tanzania Watu wa Mkoa wa Mara ( Musoma )


Watu wa kigoma huwa hawaugui kirahisi, Mungu anawalinda sana, angalia Kigoma ndio the least Hiv infected country/region both in Tz and EA region in general, kama HIV imedunda vipi hako kamafua/corona??!🤣🤣, hiyo consignment wapelekeeni Wazungu watawashukuruni sana, Mura mtani.🤣
 
Nakumbuka mwendazake alimtoa hospitalini ili aongee kuthibitisha yuko salama. Mzee alikohoa mpaka akatia huruma...
[emoji16][emoji16]alikohoa mpka akalegea,yani unakosa utu kwa sababu ya kupewa madaraka,ile clip ni fedhea sana
 
Wewe 'Raia' hujuhi kitu, subiri taarifa uone meza zinavyopinduliwa.

kutoka kwa VP si lazima 'Kifo'
what if akasema ame resign??

viongozi wanapitia wakati mgumu sana, raia hawajuhi tu.
kuna kulogana na kufitiana.
Upo sahih kwa sabab tangu msukuma atutangazie kuwa wamemletea moshi sidhan km alimaliza hata miez miwili tukaanza kupiga ramli yupo wap
 
Kama Mtanzania mpenda Viongozi wangu na Utendaji wao mzuri naomba Kujulishwa yuko wapi Makamu wangu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Nikimwona Uwanja wa Uhuru Keshokutwa ( Alhamisi ) katika Siku ya Uhuru wetu GENTAMYCINE nitakuwa ni mwenye Furaha na nitajitahidi 'nipenyepenye' mpaka nikamsalimie Mtani wangu wa Kiha kutoka kwa 'Washamba' Mkoani Kigoma.

Au kama yupo ( tunae hapa JamiiForums ) tafadhali naomba ajitokeze tu anijibu kuwa yuko na anaendelea na Majukumu yake ili tu Roho yangu iridhike kwani 'nimemmisi' sana Makamu wangu wa Rais Dk. Philip Mpango.

Waha niambieni Ndugu yenu yuko wapi?
Yuko Ikulu anapiga kazi!
 
Back
Top Bottom