Yuko wapi Mchizi Mox?

Yuko wapi Mchizi Mox?

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Huyu jamaa alivuma sana na ngoma alizoshirikiana na ngoma na Marehemu Ngwair kama vile demu wangu na Mitungi.

Kuna muda wakawa na mgogoro ambapo ilisemekana Mchizi mox ndiye aliyeandika wimbo wa mitungi, Ngwair akaupenda akamwachia kwa makubaliano flani ambayo Ngwair hakutimiza.

Ngoma yake peke yake iliyohit ni chupa nyingine ambao aliutengeneza Ramar na baada ya hapo sikumsikia tena.
 
Hilo swala la mikasi kuwa ni nyimbo ya mox kuwa alimpa ngwea kwa makubaliano flani sio sahihi bali idea ya nyimbo alikuja nayo mox geto akiwa ametoka kukesha kwenye bata then akawa anaimba-imba baadhi ya mistari ngwea akashauri waiandike wote then ngwea akaandika karibu sehemu yote ya nyimbo hiyo wakiwa na mox ambaye ndiyo mwenye idea na wakaenda kurekodi kama washkaji na hawakua na makubaliano yoyote ambayo yalikiukwa.

By the way Mox yupo hapo Dar ana kampuni yake ya kukodisha na kutengeneza matents kwa ajili ya events pamoja na kutengeneza, mwenyewe anaita "Kivuli cha Mox"
 
Yupo na bongo hoodz pitchaz wanafanya harakati upande wa muvs.tafuta tapeli dotcom,wauni wakubwa na fisi weusi utamuona humo.
 
Back
Top Bottom