Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,503
- 6,415
Jamaa yupo hapa Iringa anajihusisha na biashara mbali mbali nyingi zinahusiana na vyakula....mambo ya muziki siku hizi hafanyi kajikita kwenye biashara.
Kwanini hatengenezi tena mziki ni suala dogo tu kuwa mziki wakati wake ulikuwa haulipi kivile, ilikuwa ni kupoteza muda na hasara tu wakati ule...hata sasa sidhani kama maproducer wanatengeneza pesa kivile
Ndipo hapa tunapokosea WaTZ wengi, muziki haulipi basi atumie hiyo fursa ya umaarufu kupitia muziki kufanya mengine yatayomlipa zaidi!!
Mfano! Angetumia jina lake lililojijenga kwenye sanaa yake ya kuzalisha muziki kuhakikisha anauza mikate kwa wingi nchini!! "Mikate ya Amba ndiyo habari ya mjini" nani angeacha?? Ingeweza kumpeleka level nyingine kimaisha!!
Angeweza kabisa, kupata kazi za muda mfupi zinazolipa kama mwenzie Mchagga yule alivyojishikiza kwenye Bongo Star Search na Salama!!
Ni mawazo yangu na akili za pilau la Eid!