Yuko wapi Prof Lipumba, hajui kama mikutano imeruhusiwa?

Yuko wapi Prof Lipumba, hajui kama mikutano imeruhusiwa?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Wasalaam JF,

Baada ya kipenga kupulizwa cha kuruhusu mikutano ya kisiasa, ni matumaini yangu kwamba viwanja vya matukio vingekua vinarindima nchi nzima.

Ni mategemeo yangu kuona ratiba tight kabisa, hapa Lissu, pale Prof Lipumba, kule Hashim Rungwe (mzee wa ubwabwa) Zitto Kabwa katikati basi ilimradi tafrani, nchi ijae watu na kelele zipigwe kutoka mashariki mpaka magharibi na kaskazini mpaka kusini.

Hii ni nafasi ya nchi kuchangamka, magazeti kujaa vichwa habari chochezi na gombeshi, wanachi wasio na kazi na wale wenye muda kuongeza heka heka, basi ilimradi nchi inachangamka.

Kwa wale wanasiasa ambao hamjaanza heka heka, tafadhali sana tunaomba nchi ichangamke.
 
Huyu alizoea kununuliwa na mama alisema hatanunua mwanasiasa Bali mwanasiasa atashindana kwa ubavu wake na hoja. Hata wabunge CCM alisema ataacha wapambane kwenye fair ground. Hivyo wanasiasa uchwara kama Lupumba ni lazima watapotea kabisa. Karma inakula taratibu.
 
Mama anaupiga mwingi siyo?
 
Lipumba alikua ndio kiongozi wa kwanza kuanza mikutano ya Adhara, alifanyia pale Manzese tarehe 7/1/2023
 
Back
Top Bottom