Yuko wapi Raila Odinga wa Tanzania?

Yuko wapi Raila Odinga wa Tanzania?

Viongozi wa upinzani kuacha kubomoana ni ngumu, sababu hawabomoani kwa kupenda ni njaa!. Kumbuka kuna mtu anajua kusimama kwa vyama vya upinzani ndio kifo chake, hivyo kazi aliyonayo ni kuhakikisha havipatani na kutugeukia wananchi kutuambia "unaona wenyewe kwa wenyewe hawapatani wataweza kuongoza". Tukifikiri kuwa ni mpaka tupate viongozi safi upinzani ndio tutaweza kuwachagua tunajidanganya, kwa vyombo vya habari vyetu hawataweza kuwa safi hata siku moja. La msingi ni kuazimia moyoni kuwa ssm basi, kama huyo tutakayemchagua ni safi si safi lakini ssm waondeke. Kama hatakuwa safi angalao tutakuwa tayari tumejifunza na kuweza jinsi ya kuwaondoa kama hawafai, bila hivi ssm watakuwa wanacheza mchezo wa kuwapaka matope viongozi wote wa upinzani nasi tunabaki kuwaona hawafai. Hatuwezi kutoka hapa mpaka tuamue kuwa hawa mabwana basi!.
 
Njabu Tha Dude;

Nashukuru sana kwa mtizamo wako na fikra zako njema, hapa tunajaribu kuona ni jinsi gani ya kujinusuru na na mikono ya hawa mafisadi, sasa mimi kama mimi nikawa nadhani ni kanjia gani kanaweza kutuponya na hawa mafisadi, chukulia mfano wa panya ndani ya nyumba, mara anakurupuliwa, panya yule atafanya kila njia ili aweze kujinuru na si vinginevyo, kwani akichelewa basi hapo atashambuliwa hadi umauti umfike.

Njabu Tha Dude;najua unaweza kuwa na jibu lenye tumaini, wewe kama wewe unadhani tuanzie wapi? usisahau kuwa muda nao unajongea!!

issayamwita

Jibu langu ni kwamba Wapinzani waungane na kuunda umoja wa vyama vya upinzani. Hiyo ndiyo hatua pekee ambayo inaweza kuleta matumaini ya mabadiliko ya kweli ya kisiasa kutoka. Wenzetu wa Kenya wame-experiment na suluhisho la Upinzani kuunda umoja dhidi ya vyama tawala na hatimaye wakashinda mara mbili (kwanza ilikuwa KANU vs NARC na mara ya pili PNU vs ODM). Waswahili wanasema: Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
 
Nimekuwa nikijiuliza maswali lukuki, wako wapi watanzania(wapiganaji) wanaoweza kutukwamua hapa tulipo? tumekwama, hatuna mwelekeo, Spika wetu Samwel sitta amekiri kuwa upinzani ndiyo chachu ya bunge lake, lakini.

Maswali ya kujiuliza:

(a) je ni kweli hatuna watu wazalendo kama akina Odinga wa pale Kenya?

(b) Ni nini mtizamo wa vyama vya upinzani siku za usoni hapa Tanzania?

Wana JF naomba tutafakari ni nani mkombozi wa taifa letu hili kwa siku za usoni? je yawezekana akatoka ndani ya CCM? ama anaweza akatoka ndani ya vyama vya upinzani?

IsayaMwita,

Kutafuta mtu mmoja na kumfanya suluhisho la Matatizo ya Tanzania ni kosa kubwa sana.

Ni kosa hilo lilifanyika 2005 na matokeo yake yanaonekana sasa!

Kinachohitajika ni mfumo mpya wa kuleta maendeleo ambao hautahusisha chama au mwanasiasa!!
 
Mchungaji,

Pole sana Mkuu, nadhani hautaelewa mpaka utakaporudi hapa nyumbani, unajua ninio kinaendelea hapa nyumbani? kwa taarifa yako ni hivi kwa yeyote atakayesaliti ule muungano wa vyama vya upinzani ni kichapo tu.

Tumeanza jana kwa kumshikisha adabu Dr. Mvungi na sasa tuna mngojea Lipumba na miwani yake, haiwezekani tukaendelea kuyumbishwa na hawa wapuuzi wanaopenda sifa na kujipendekeza kwa CCM.

Jana ilikuwa shika nikushike Dr. Mvungi hana hamu hata kidogo, nataka tueleweke hivi hapa TARIME hatutaki ujinga, na hii ni CHACHU TU nafikiri tukimaliza tarime nguvu zetu tutahamishia Mkoa wa MWANZA, NA KISHA SHINYANGA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

UNGU INUSURU TANZANIA
 
JF nashukuru sana kwa kuhihamisha hii thread mpaka hapa ilipo, nataka kuwauliza kweli hapa ndiyo mahali pake? Naomba muirudishe kule kwenye upande wa JUKWAA LA SIASA
 
issayamwita

Jibu langu ni kwamba Wapinzani waungane na kuunda umoja wa vyama vya upinzani. Hiyo ndiyo hatua pekee ambayo inaweza kuleta matumaini ya mabadiliko ya kweli ya kisiasa kutoka. Wenzetu wa Kenya wame-experiment na suluhisho la Upinzani kuunda umoja dhidi ya vyama tawala na hatimaye wakashinda mara mbili (kwanza ilikuwa KANU vs NARC na mara ya pili ODR vs NARC). Waswahili wanasema: Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

Siku zote utasikia watu wakisema wapinzani waungane, sasa waunganeje? kama leo vyama vingine vikiona chama kimoja kimeanza kupata nguvu hao hao wajipanga kukibomoa? nadhani hata sisi watanzania let we play our rule, hakika bila hivyo ni ndoto, kwani, CCM nao kila kukicha wanajipanga jinsi ya kijiimarisha na si vinginevyo.

Tunaweza, tusubutu basi, taabu yetu sisi wanaJF tunaishia hapa hapa jamvini na wala hatupati kuelimisha ndugu zetu kule vijijini.

Sisi wana Tarime sasa kazi ya kuelimisha mama zetu, babu zetu, watoto wetu, mabinti zetu hakika tumeimaliza, tunaelekeza nguvu zetu mkoani(msoma mjini)

Endeleeni kututakia mema vita hii haijalishi kama tutakua kafara, najua itatughalimu tu, vita dhidi ya mafisadi ni ngumu ILA SISI NI WASHINDI WATARAJIWA.
 
Do not talk about Raila and his politics kama humjui vizuri. Do not believe everything you see or hear in the news.

Raila is the only bigshot in Kenya who tells the wanainchi about what is going on. Raila is the only Dume who can withstand the heat of kenyan rotten politics.

Believe me Kenyan politics is ROTTEN. We need twenty more Railas to get the system to change.

Thank you very much.
 
JF nashukuru sana kwa kuhihamisha hii thread mpaka hapa ilipo, nataka kuwauliza kweli hapa ndiyo mahali pake? Naomba muirudishe kule kwenye upande wa JUKWAA LA SIASA

Ninauliza ni kwanini mmehihamishia hii post yangu hapa ilipo? naomba muirudishe kule ilipokuwa (jukwa la siasa)
 
ninavyoamini raila odinga wa tanzania angeweza kuwa hayati sokoine....ni imani yangu
 
Siku zote utasikia watu wakisema wapinzani waungane, sasa waunganeje? kama leo vyama vingine vikiona chama kimoja kimeanza kupata nguvu hao hao wajipanga kukibomoa? nadhani hata sisi watanzania let we play our rule, hakika bila hivyo ni ndoto, kwani, CCM nao kila kukicha wanajipanga jinsi ya kijiimarisha na si vinginevyo.

Tunaweza, tusubutu basi, taabu yetu sisi wanaJF tunaishia hapa hapa jamvini na wala hatupati kuelimisha ndugu zetu kule vijijini.

Sisi wana Tarime sasa kazi ya kuelimisha mama zetu, babu zetu, watoto wetu, mabinti zetu hakika tumeimaliza, tunaelekeza nguvu zetu mkoani(msoma mjini)

Endeleeni kututakia mema vita hii haijalishi kama tutakua kafara, najua itatughalimu tu, vita dhidi ya mafisadi ni ngumu ILA SISI NI WASHINDI WATARAJIWA.

Wapinzani wakiungana nakuhakikishia wataibwaga CCM on the very first attempt. Halafu CCM ikibwagwa mara moja tu, basi nadhani itasambaratika na kupoteza nguvu na mwelekeo kama ilivyotokea KANU kwa Kenya na UNIP kule Zambia. Hata watu kama Anna Kilango na Mwakyembe na Wanasiasa wengineyo wa CCM wenye uchungu na nchi yao watapata sababu na mwanya wa kuihama CCM na kujiunga na Upinzani.
 
naomba mtu mwenye simu ya huyu mama kilango anipe, kwa jinsi anavyopambana na mafisadi kama akina kingunge nahitaji kumpongeza na ikiwezekana nimchangia hata lita 100 za dizeli ili aweze kufika mbali zaidi kwa maisha aliyoamua
 
Wana JF nimepitia michango yote toka kwa wadau. Ni mizuri na challenging!! Upinzani kama wa Rail Odinga kwa Tanzania ni ndoto sana kwa sasa, labda waibuke viongozi wengine wa upinzani na wala si tulio nao kwa sasa. For instance, Mrema hajazitambua nyakati na amekwisha kisiasa. Wengine ni uchu tu wa madaraka na vijisenti na ndiyo maana tunaona mara leo kahamia Chadema, mara TLP mara ssm sasa yote ya nini? Kwa visingizio kuwa mara ukabila, mara ruzuku ya upendeleo, mara vile. Kwa namna hii ni kujiyumbisha kuhama. Ni sawa na kumhamisha mtoto shule kila wakati mwishowe anapoteza dira kabisa!!!

Kushinda kwa wapinzani Tanzania kutatokana na watanzania wenyewe tena wale wapiga kura? Majority voters wapo vijijini ambao hawajui demokrasia bali ni vitisho toka kwa chama ssm. Unajua wananunuliwa kwa hadi shs. 500 na wanatishiwa kuwa usipomchagua fulani wa ssm utahamishwa kijiji? Yaani hawaelewi kabisa kuwa si zoezi rahisi sana kutambua aliyekupigia kura, na pia hakuna lolote litatokea kama hukumchagua. Ni lini basi tutajitosa kutoa mass education kwenye eneo la uchaguzi haswa? Wasomi wa nchi hii na ambao wanapiga kura ni minority na hatuwezi kabisa kuiangusha ssm kwa midomo tu, vitendo ni lazima. Halafu nimegundua kuwa wasomi wengi hawapigi kura jamani. So katika sensitization nao wahamisishwe wakapige kura. Their one vote will mean a lot in Revolution.

Sasa tuangalie yule Maalim Seif tuanayesema ndiyo Chachu ya Upinzani?????!!!! Je umemsikia mara ngapi siku hizi?????!!! Unaifahamu ssm????? Amelelewa na ssm na kamwe hawezi kuwa mpinzani wa kweli. Narudia tena Raila Odinga wa Tanzania bado hajajitambulisha, yawezekana yupo ila anasoma nyakati au bado hajazaliwa. Ukitaka kujua ukweli subiri 2010. Kawa mantiki hiyo basi wana JF tujipange tuanzishe kamati ya kuratibu uhamasishaji Tz na ikiwezeshaji tuanze na fund rasing kabisa. Siasa inahitaji pesa, tusije tukakuta tunatafuta njia za mkato kupata fedha kama zile za 2005. Let us fight for a change, hata Obama alijipanga ndiyo maana akaweza kufika hapo alipo, hata kama hatakuwa rais but ameitingisha historia ya Amerika. Let us have a dream like that of Martin Luther King Jr katika mkutano wake Wincolin, in 1963!! However, tusikate tamaa.. Long live JF members and visitors.
 
Maane,
Luther King ni mmoja wa viongozi naowaheshimu sana waliowahi kutokea. Lakini hata ile 1963 kwenye his famous I have a dream, alisema kuwa ndoto yake ilikuwa siku moja watoto wake wangehukumiwa kutokana na matendo yao na si rangi ya ngozi. Sasa huyu alikuwa by far better kuliko any Raila you know. Hakuna anayedai kuwa watanzania muda wetu wakujikomboa haujafika, tunachosema ni kuwa tukisubiri atokee Raila wetu atukomboe,tumekwisha. Ukombozi wa kweli huanzia kwa mtu binafsi na hii inawasumbua CCM huko Tarime sasa hivi kwa kuwa wameshindwa kusoma alama za nyakati.
 
Hakika watanzania ni lazima tuwe na lengo na dhamira njema kwa taifa letu, haiwezekani kuwaachia hawa Mafisadi wa Taifa hili, napata shida kuona kuwa bado hatujampata Raila wa Tanzania, bado tuna vidudu watu, wanaojijali na wasiotutakia mema sisi
 
Wana JF nimepitia michango yote toka kwa wadau. Ni mizuri na challenging!! Upinzani kama wa Rail Odinga kwa Tanzania ni ndoto sana kwa sasa, labda waibuke viongozi wengine wa upinzani na wala si tulio nao kwa sasa. For instance, Mrema hajazitambua nyakati na amekwisha kisiasa. Wengine ni uchu tu wa madaraka na vijisenti na ndiyo maana tunaona mara leo kahamia Chadema, mara TLP mara ssm sasa yote ya nini? Kwa visingizio kuwa mara ukabila, mara ruzuku ya upendeleo, mara vile. Kwa namna hii ni kujiyumbisha kuhama. Ni sawa na kumhamisha mtoto shule kila wakati mwishowe anapoteza dira kabisa!!!

Kushinda kwa wapinzani Tanzania kutatokana na watanzania wenyewe tena wale wapiga kura? Majority voters wapo vijijini ambao hawajui demokrasia bali ni vitisho toka kwa chama ssm. Unajua wananunuliwa kwa hadi shs. 500 na wanatishiwa kuwa usipomchagua fulani wa ssm utahamishwa kijiji? Yaani hawaelewi kabisa kuwa si zoezi rahisi sana kutambua aliyekupigia kura, na pia hakuna lolote litatokea kama hukumchagua. Ni lini basi tutajitosa kutoa mass education kwenye eneo la uchaguzi haswa? Wasomi wa nchi hii na ambao wanapiga kura ni minority na hatuwezi kabisa kuiangusha ssm kwa midomo tu, vitendo ni lazima. Halafu nimegundua kuwa wasomi wengi hawapigi kura jamani. So katika sensitization nao wahamisishwe wakapige kura. Their one vote will mean a lot in Revolution.

Sasa tuangalie yule Maalim Seif tuanayesema ndiyo Chachu ya Upinzani?????!!!! Je umemsikia mara ngapi siku hizi?????!!! Unaifahamu ssm????? Amelelewa na ssm na kamwe hawezi kuwa mpinzani wa kweli. Narudia tena Raila Odinga wa Tanzania bado hajajitambulisha, yawezekana yupo ila anasoma nyakati au bado hajazaliwa. Ukitaka kujua ukweli subiri 2010. Kawa mantiki hiyo basi wana JF tujipange tuanzishe kamati ya kuratibu uhamasishaji Tz na ikiwezeshaji tuanze na fund rasing kabisa. Siasa inahitaji pesa, tusije tukakuta tunatafuta njia za mkato kupata fedha kama zile za 2005. Let us fight for a change, hata Obama alijipanga ndiyo maana akaweza kufika hapo alipo, hata kama hatakuwa rais but ameitingisha historia ya Amerika. Let us have a dream like that of Martin Luther King Jr katika mkutano wake Wincolin, in 1963!! However, tusikate tamaa.. Long live JF members and visitors.

Maane,
Lengo si kuing'oa ssm kama unavyosema, lengo liwe kuwang'oa MAFISADI. Kumbuka ssm kama chama ni kizuri na ndani ya ssm kuna 'PARTRIOTIC FIGURES' ambao wapo mbele kupigania maslahi ya Taifa. Nani asiyejua michango ya wana ssm kama Anna Kilangho, Dr. Mwakyembe, Bw. Seleli na wengine wengi? Tutafute ni namna gani ya kupenya na kuingia ndani ya kiini cha ssm (to penetrate into the inner most core ya ssm) ili tuwatoe na kuwasafisha hao mafisadi ambao kwa kweli ni wachache. Angalia wengi hapo juu wamesema TZ hatujapata mtu kama RAILA, sasa wapinzani wenyewe ndio hao tunaowajua kazi migogoro isiyoisha, sasa 'we need to use the already existing structures of ssm to clean dirty figures and to change inhumane and domant policies of ssm for the benefit of all Tanzanians'. God bless Tanzania and its people.
 
Thanks Gagnija and FUGWE,
Kwa Gagnija, ssm imeshahukumiwa kwa matendo yake tayari, ya kukandamiza upinzani, kutenga wanassm wenye moyo wa kitaifa ambao wanaichallenge ssm, na kulea mafisadi ndani ya chama. Tunajaribu kujitafutia ukombozi binafsi ila vikwazo ni vingi sana, na ambavyo vinaletwa na system ya uongozi tulionao. Wote kwenye campaign wanatudanganya sana kwa maneno ya mgongo wa chupa, na watanzania tunakubali, walishajua tu kwa maneno matamu kwa watz hata kama hayatekelezeki basi kura umepata. Huko Tarime kunafuka Moshi sasa, juzi NSSR walivamiwa, sijaelwa Chadema itakuwaje? CUF ndo niko bubu kabisa!! Kwa hapo huoni kuwa ssm kwao ni advantage? Sasa ukombozi binafsi ni upi au ni fujo tuu? Ndiyo maana nimesema upinzani ni tabu kupata madaraka makubwa TZ kwa sasa.

Kwako Fugwe,
Kweli tunao wanamapinduzi na wasiogopa na ssm ni kama chama hakina matatizo kama ulivyosema. Wasiwasi wangu ni kuwa ssm ikishaona hivyo inajaribu kutafuta namna ya kuwanyamazisha wapiganaji kama hao, na si ukashangaa kuona 2010 wanaenguliwa wasigombee. Na kwa sababu ssm inakumbatia mafisadi wanao finance election basi ni heri waondoke hao wapiganaji, na nguvu ya kuwanyamazisha inafadhiliwa na haohao mafisadi. Majority wa ssm ukianzia uvccm na uwt wote wanafadhiliwa na mafisadi, kuna kijana mmoja katika kinyang'aniro cha uvccm majuzi tu RA alimfadhili 20 mil na atahakikisha atapita. Hivyo basi kupata rais au PM mwana mapinduzi toka ssm ni ngumu sana, sana sana ssm kama suala la mtandao na makundi llitaendelea basi litokee kundi lenye nguvu la wapiganaji ndani ya ssm then ssm yenywe ijigawe ssm 1 and ssm2 then wadau tuelismishe umma ubaya wa makundi hayo then tunaweza kung'oa ule upande haswa unatumikia mafisadi. At the same time tusubiri 2010 si wenyewe wamesema watu watenganishe biashara na siasa? Fisadi anaweza kutokuwa kiongozi wa kisiasa au mwenye madaraka but akafinance uchanguzi ili kulinda interest zake na kuwa na power fulani fulani kama afanyavyo RA kwa sasa japo ameshakuwa mpole kidogo. Sasa naomba wale ambao mko karibu na akina Mwakyembe, Kilango Seleli, na wengineo kama hao mpeane mawazo ya kishujaa tuone cha kufanya hata kama haitawezekana 2010 then 2015 tufanikishe. Long live JF.
 
Napata shida sana tena sana, Mbona sisi watanzania hatujawa na mikakati ya 2010, mbona bado tumefunikwa na blangeti zito
 
Maane,
Lengo si kuing'oa ssm kama unavyosema, lengo liwe kuwang'oa MAFISADI. Kumbuka ssm kama chama ni kizuri na ndani ya ssm kuna 'PARTRIOTIC FIGURES' ambao wapo mbele kupigania maslahi ya Taifa. Nani asiyejua michango ya wana ssm kama Anna Kilangho, Dr. Mwakyembe, Bw. Seleli na wengine wengi? Tutafute ni namna gani ya kupenya na kuingia ndani ya kiini cha ssm (to penetrate into the inner most core ya ssm) ili tuwatoe na kuwasafisha hao mafisadi ambao kwa kweli ni wachache. Angalia wengi hapo juu wamesema TZ hatujapata mtu kama RAILA, sasa wapinzani wenyewe ndio hao tunaowajua kazi migogoro isiyoisha, sasa 'we need to use the already existing structures of ssm to clean dirty figures and to change inhumane and domant policies of ssm for the benefit of all Tanzanians'. God bless Tanzania and its people.

Unachekesha kweli Mkuu,

Yaani unaweza ukapenya mpaka pale kwenye kiini? utatumia njia gani? hawa ccm ni watu wenye akili timamu kwelikweli, acha mchezo mkuu wangu, labda tuujiundie kaumoja ka upinzani hapo tunaweza tukawa na nguvu za kukididimiza chama hiki na si vinginevyo
 
Wale tulio waamini wameingia mitini, sijui tunafanya nini? hii 2010 itakuaje? hapa ni kizungumkuti jamani
 
mfumo walojiwekea mafisadi kumpata odinga ni heri ngamia apite tundu la sindano.
wamejaa na kujazana kila mahali labda tu watanzania wajitoe wenyewe si viongozi hawa hakuna amjuaye mlalahoi wote wamejaa ufisadi tu
 
Back
Top Bottom