Yuko wapi Rais wa China Xi Jinping?

Duuuu unajua kwanini aliacha madaraka????
 
kama wachina hawaogopi, kwa nini walienda kupiga mabomu maji halafu wakaondoka pamoja na kutoa kitisho cha kuanzisha vita yule spika alipotua taiwan??
unadhani wa vietnam wangeshinda ile vita bila sapoti ya wa communist?
 
Nini Zacharia Hanspope? Baba yao mwenyewe nilikuwa namfahamu. Ngoja nikupe usichojuwa.

Hans Pope (senior) alikuwa Regional Police Commander, Iringa, kabla ya kupelekwa Mkoa wa Ziwa Magharibi (West Lake Region) ambao sasa ni Kagera. Nakumbuka picha yake ilipochapishwa magazetini hapa nchini, 1972, baada ya kuuawa na askari wa Amin waliomteka Mutukula.

Katika picha ile, mwili wake ulivimba sana. Amin alisema jeshi letu lilikuwa na Wachina na Hans Pope ulikuwa ndiyo ushahidi huo. Hans Pope alikuwa na damu ya Kijerumani, siyo ya Kichina, ingawa sura yake katika picha ile ilikuwa kama ya "Kichina" kwa sababu ya kuvimba sana. Naikumbuka sana picha ile. Ilikuwa ukurasa wa kwanza magazetini.

Watoto wake ndiyo hao wawili Zacharia na Harry (wote marehemu sasa) waliohusika na mpango wa kumpindua Nyerere, 1982, pamoja na wanajeshi wengine.

Zacharia alikuwa captain kikosi cha mabomu na Harry (RIP) alikuwa rubani wa Airwing. Walishawishiwa kuingia kwenye uhaini kwa hisia kuwa Nyerere kumsababisha kifo cha baba yao kwa kumpeleka kuwa RPC West Lake Region
 
Ndiyo ss tunajua siyo kila kitu kusifia tu,,, baba wa africa ni mmoja tu (NELSON MANDELA) tu
HAKUNA NELSON MANDELA BILA NYERERE:

Dogo King klax tulia nikupe shule ya Bure;

Katika bara zima la Afrika kwa muda wa takriban miaka 100 iliyopita simuoni kiongozi yeyote ambaye alijitoa kwa maslahu ya bara la Afrika kama Julius kambarage Nyerere kuanzia waswala ya ukombozi wan nchi mbalimbali. Mwalimu alisema uhuru wan chi moja ya Afrika hauna maana ikiwa sehenmu moja ya bara inakaliwa na wakoloni.
Mwaka 1960 wakati wa Serikali ya Madaraka ya Tanganyika, Mwalimu aliwahi penyeza barua kwa Mwenyekiti wa kikaocha jumuiya ya Madola kilichokuwa kinafanyika pale London. Katika kikao hicho kulikuwa na wajumbe kama Indira Gandhi wa India, Nnamdi Azikiwe wa Nigeria na Kwame Nkrumah wa Ghana wakiwakilisha nchi huru za bara la Afrika kwa wakati ule. Katika waraka huo aliwaambia wajumbe wa Afrika kuwa kama angekuwa miongoni mwao basi asingikaa pamoja na mjumbe wa Afrika Kusini kaburu Verword ambaye ombi lake la kujiunga na Jumuiya hiyo lilikuwa linajadiliwa baada ya Uingereza kuyachia makoloni matano ya Afrika kusini kwa pamoja.
Waraka wa Nyerere vilevile ulinakiliwa kwenye bgazeti la The observer la London na ukachapwa. Matokeo ni kwamba Afrika Kusini ilinyimwa uanachama wa Jumuiya ya Madola kutokana na sera zake za kibaguzi. Pata picha ya mtu ambaye si mwanachama wa kikao lakini ana influence maamuzi ya kikao akiwa nje na wajumbe wanafanya kadri ya maono yake.
Unapomwongelea Mandela lazima ukumbuke kuwa hakuna Mandela bila Nyerere, yaani Nyerere ndiye aliye ongezea umaarufu wa Mandela ambaye anaenziwa sana. Passport ambayo Mandela alisafiria kwa Mara ya kwanza kwenda mkutano wa PAFMECA kukutana na akina Haile Selassie, William Dubois, Nyerere, Nkrumah, Azikiwe, Sekou Toure nk ilikuwa ya Tanzania. Hata mipango ya kutoka SA Iilipangwa na Nyerere. Kikubwa utakachokiona kwa Mandela ni kwamba yeye ndiye mfungwa wa kisiasa aliyekaa jela kwa muda mrefu (miaka 27) akiwa amesimama kwenye msimamo wake kwa kile anachokiamini na kwamba alipotoka hakulipa kisasi kwa wale waliomfunga. Hilo tu ndilo Mandela analo mzidi Nyerere
Mwalimu vilevile alikuwa ndiyo kiongozi wa kwanza wa nchi ya Afrika kuvunja uhusiano wa kiuchumi na kisiasa mara moja baada ya Ian Smith mlowezi wa Southern Rhodesia (sasa Zimbabwe) kujitangazia Uhuru mnamo mwaka 1966 baada ya Waingereza kuiachia. Na vikwazo hivyo ndivyo vilivyopelekea wapigania Uhuru wa Zimbabwe kujitangazia uhuru mnamo mwaka 1980 na Robert Mugabe akiwa Raisi wao.
Mwalimu alitoa raslimali ya nchi maskini ya Tanzania kwa kuwapa makambi wapigania uhuru wa Namibia (SWAPO), Angola (MPLA na NFLA), Afrika Kusini (PAC na ANC), Zimbabwe (ZAPU na ZANU) na Msumbiji (FRELIMO). Bila sacrifice ya Mwalimu na maamuzi mahsusi basi historia ya nchi zote hizo ingeandikwa vinginevyo.

Sasa wanaosema Nyerere kafanya nini katika duru za kimataifa sjui wana maanisha nini? Kama unaweza kutoa mchango wa kuikomboa nchi inayogandamizwa kwa ubaguzi wa rangi au ukoloni mkongwe au ukoloni mamboleo je kuna tukio linazidi hilo kimataifa
 
Bro nimekuwa naenda vietnam ndan ya miaka 2 sasa aisee huwez kuamin kuwa walikuwa na bifu na marekan. Kwasasa hiv hawa jamaa wamewakumbatia wazungu kuliko mchina. Sema walichonishinda ni boda boda. Nyingi Mno pale Rangoon

Ni kweli VietNam imebadirika sana - lakini kumbuka Rangoon haipo VietNam, ni kweli wanashirikiana na Merikani kwenye baadhi ya mambo lakini hawa amini sana Wamerikani au kusema WavietNam wamekwisha sahau ukatiri wakati wa vita na Wamerikani, hivi sasa Wachina ndio wamewekeza kwa wingi nchini VietNam - Merikani inajaribu sana sana kuirubuni VietNam ifarakane na Uchina lengo hasa la Merikani ni kutaka mataifa yote yaliyo jirani na Uchina waitenge Uchina kutokana na fitina zinazo enezwa na Merikani kuhusu ubaya wa Wachina - wanatumia mbuni zile zile ambazo Merikani ilizitumia kuhadaa viongozi wa EU wawachukie Warusi, ili mwisho wa siku nchi za Ulaya zilazimike kushirikiana na US kupigana vita na Urusi lengo hasa ni kutaka kuisambaratisha Urusi yote for Uncle SAMs vested interest, hata kama katika kutekeleza malengo yao dhidi ya Urusi yanaweza kusababisha Dunia nzima kuangamizwa hilo wao hawajali kabisa.

Mchezo huu huu ndio Merikani inataka kuutumia kwenye mataifa ya mashariki ya mbali yanayo pakana na Uchina - anataka yashirikishwe kwenye vita baina ya Merikani na Uchina akitumia Taiwan kama kisingizio cha kuanzisha vita - lengo hasa ni kutaka kuihujumu Uchina kiuchumi na kuidhoofisha kijeshi ili hisiweze kuwa tishio tena kwa maslahi ya Merikani - ni hilo tu hakuna jingine.
 
Kifupi ni kwamba,hili lilikuwa ni jaribio la 3 na la mwisho la kutaka kumpindua Nyerere.
 
Kifupi ni kwamba,hili lilikuwa ni jaribio la 3 na la mwisho la kutaka kumpindua Nyerere.

Alikuwa jaribio Bali mpango wa kumpindua. Jaribio lilikuwa moja tu enzi za KAR basi, maana wale walifika mpaka ikulu.
 

Asante Sana.
 
Kipande hiki nilitoka draw nilivyoona umekinukuu nikafurahi labda ningeelewa lakini nimetoka draw tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…