Yuko wapi Stephen Masele, Mwanasiasa machachari aliyefanyiwa figisu na Ndugai?

Yuko wapi Stephen Masele, Mwanasiasa machachari aliyefanyiwa figisu na Ndugai?

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Hayati Magufuli akiwa kwenye Kampeni Shinyanga aliahidi kumpatia huyu jamaa nafasi kwa kumshawishi amuunge mkono Katambi ambaye kama isingekuwa vile sidhani kama angekuwa hapo alipo sasa.

Je, Mama yetu Samia anakumbuka alivyoahidi mtangulizi wake kuhusu huyu bwana?

Je, ndiyo mwisho wa Masele umetimia?

Mnaojua za chini ya kapeti kuhusu huyu bwana labda mtupe stori yake angalau tufurahi na kumbwombea kipenzi chetu Masele.
 
Kama siku nne au tano zilizopita nilimuona Hotel maarufu iliyopo karibu na bahari ya Hindi, Posta, Dar es salaam na ilikuwa ni mida ya wenzetu kufuturu akiwa na sahani yake akielekea kujihudumia chakula.

Ila kama una maana yupo wapi kishughuli na kisiasa kwa hilo sijui kwa sasa labda kwa wanaomjua zaidi.
 
Si ajabu alikuwa kavaa kanzu pia!
 
Stephen Masele atulie tu muda wake ushapita,sasa ni zamu ya watu wengine,kama fedha aliwekeza chini basi ni muda wa kupay the price.
 
Hayati Magufuli akiwa kwenye Kampeni Shinyanga aliahidi kumpatia huyu jamaa nafasi kwa kumshawishi amuunge mkono Katambi ambaye kama isingekuwa vile sidhani kama angekuwa hapo alipo sasa...
Sasa sisi wana mageuzi anatuhusu nini?
 
Hayati Magufuli akiwa kwenye Kampeni Shinyanga aliahidi kumpatia huyu jamaa nafasi kwa kumshawishi amuunge mkono Katambi ambaye kama isingekuwa vile sidhani kama angekuwa hapo alipo sasa...
Naunga mkono hoja.

P
 
Naunga mkono hoja.

P
"Mkuu salama - toshesha basi ujumbe wako! Kaundika P tu haileti maana!
 
Masele alinyanyaswa sana, mimi nilimshauri ahamie Chadema sijui yeye bhana.
kwa wakati ule isingewezekana, angebananishwa nafikiri sasa hivi angekuwa ndani na kesi ya uhujumu uchumi au inayofanana na hiyo... kwa wakati huo kwenda tofauti na kauli ya mwendazake ilikuwa ni kujipatia makaa!!

kwa sasa yes he can weigh out this option.
 
Back
Top Bottom