Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?
Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?
rmashauri,
Ebu nikumbushe kidogo baadhi ya maneno ya nyimbo zake, namkumbuka pia, sema wimbo unakuja unaondoka. Natamani pia kujua whereabouts zake. Alikuwa mwimbaji mzuri sana wa nyimbo za injili
Ewaa,
Sasa nimekumbuka nyimbo zake, nakumbuka namna ambavyo uimbaji wake ulikuwa wa kipekee. Ilikuwa ni upako tu, mwenye wherebaouts zake tafadhali! Nakumbuka kununua sana audio cassettes zake miaka hiyo. Sijui zilipotelea wapi jamani
Nafikiria kuwasiliana na wale jamaa wa Redio Habari Maalum, hope wanaweza kuwa na kanda za huyu mtumishi. Watu bwana na huduma zao. Nikipata habari zake ama nyimbo zake nitakujulisha mkuu.
jamani tunaomba update za ng'winamila ni muda mrefu sana nyimbo zake zilikuwa zinanibariki sana
Hii post najua ni ya zamani kidogo. Nimekuwa nikitafuta habari za Timothy Ngw'inamila au nyimbo zake pia. Nimefanikiwa kupata nyimbo zake hapa: Timothy Ngw Inamila unaweza kudownload pia. Barikiwa sana!Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?
Yaani kumbe alikuwa mwanza? Ni mwalimu? Ngoja niulizie pale mwanza secUmenikumbusha mbali kwakweli, Timothy amenifundisha uimbaji nilipokuwa Mwanza sekondari alikuwa ni storekeeper wa shule lakini pia alikuwa ni mwalimu wetu ktk kwaya ya Ukwata. Miaka ya mwanzoni ya 2000 nilisikia yuko Dar lakini sijawahi sikia habari zake tena zaidi ya kumbukumbu ya kaseti zake alizoimba
Zinapatikana wapi album zake? Album ya mwana mpotevu ilikuwa balaaa sanaNdugu yangu Gashle,
Huyu mtu ni mwimbaji mzuri sana na nyimbo zake zilikuwa zuri za kutia moyo na kuhubiri injili. Baadhi ya nyimbo zake ni:
1. Mwana mpotevu aliomba urithi wake kaenda nchi za mbali.......
2. Ni jambo la kutisha, mtu kuanguka katika mikono ya MUNGU aliye hai....
3. Yote ni Ubatili
4. Lengo moja, kumtangaza YESU
5. Utajakumbuka
6. Ombeni kwa bidii, lazima mtapata jibu