Yuko wapi Timothy Ng'winamila?

Yuko wapi Timothy Ng'winamila?

rmashauri

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
3,011
Reaction score
456
Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?
 
RMASHAURI,
Umenikumbusha mbali sana.
Mwaka 1996, nilikutana na Timothy kule TARIME akifanya huduma ya uimbaji.
Kwa sasa sijui aliko.
Nami nitafurahi kupata taarifa zake.
 
Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?

Umenikumbusha mbali kwakweli, Timothy amenifundisha uimbaji nilipokuwa Mwanza sekondari alikuwa ni storekeeper wa shule lakini pia alikuwa ni mwalimu wetu ktk kwaya ya Ukwata. Miaka ya mwanzoni ya 2000 nilisikia yuko Dar lakini sijawahi sikia habari zake tena zaidi ya kumbukumbu ya kaseti zake alizoimba
 
rmashauri,

Ebu nikumbushe kidogo baadhi ya maneno ya nyimbo zake, namkumbuka pia, sema wimbo unakuja unaondoka. Natamani pia kujua whereabouts zake. Alikuwa mwimbaji mzuri sana wa nyimbo za injili
 
Ndugu yangu Gashle,
Huyu mtu ni mwimbaji mzuri sana na nyimbo zake zilikuwa zuri za kutia moyo na kuhubiri injili. Baadhi ya nyimbo zake ni:

1. Mwana mpotevu aliomba urithi wake kaenda nchi za mbali.......

2. Ni jambo la kutisha, mtu kuanguka katika mikono ya MUNGU aliye hai....

3. Yote ni Ubatili

4. Lengo moja, kumtangaza YESU

5. Utajakumbuka

6. Ombeni kwa bidii, lazima mtapata jibu
 
Last edited:
Ewaa,

Sasa nimekumbuka nyimbo zake, nakumbuka namna ambavyo uimbaji wake ulikuwa wa kipekee. Ilikuwa ni upako tu, mwenye wherebaouts zake tafadhali! Nakumbuka kununua sana audio cassettes zake miaka hiyo. Sijui zilipotelea wapi jamani
 
Mimi mwenyewe nilikuwa na audio zake za matoleo kama matatu hivi lakini zikachakaa zingine zikapotea. Nikawa nazitafuta hazipatikani, tafuta CD hazipatikani.
 
Nafikiria kuwasiliana na wale jamaa wa Redio Habari Maalum, hope wanaweza kuwa na kanda za huyu mtumishi. Watu bwana na huduma zao. Nikipata habari zake ama nyimbo zake nitakujulisha mkuu.
 
Asante rafiki nitashukuru sana.
Barikiwa na BWANA YESU.
 
rmashauri, et al

Nimeongea na jamaa wa Redio Habari Maalum. Kwa haraka hawakuweza kunipa jibu, ila wamenishauri kuwaandikia email wanisaidie kufanya utafiti maabarani kwao. Nikipata jibu jema nitakujulisha.

Shalom.
 
jamaana tunaomba update za ng'winamila ni muda mrefu sana nyimbo zake zilikuwa zinanibariki sana
 
Ina sikitisha sana kumpoteza ndugu yetu kwenye ulingo wa nyimbo za injili. nina kanda moja hapa huwa inanifikisha mbali sana. " NI HERI UAMINI YA KWAMBA MUNGU YUPO NA USIMKUTE KULIKO KUTOKUAMINI NA UKAMKUTA". HATA NYIMBO ZAKE KWA YEYOTE ALIYE NAZO ATUTUPIE KWENYE MTANDAO INAWEZA KUTUFARIJI SANA
 
Siri ya Ushindi nimekwishaipata mmh, Mungu upendo umenirehemia, kanuni zenyewe faida nimekwishazipata mmmh, Mungu wa upendo umenirehemia! Nipe Rehema.....afichae dhambi zakeee hatafanikiwa Bali atubuye na kuziacha rehema ni
 
Rehema ni yake......imba kwa sauti ya Timothy, nilipata taarifa kwamba yuko Dodoma au mpwampwa nadhani, kilichonisikitisha Timothy alishaacha uimbaji amekuwa mtu wa mataifa
 
duh! real nami nimekumbuka mbali, pamoja na waimbaji wengine kipindi hicho shari martin, john chavulimo,ibrahimu ng'umba wote hawasikiki tena wengine wameasi so sad
 
Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?
Hii post najua ni ya zamani kidogo. Nimekuwa nikitafuta habari za Timothy Ngw'inamila au nyimbo zake pia. Nimefanikiwa kupata nyimbo zake hapa: Timothy Ngw Inamila unaweza kudownload pia. Barikiwa sana!
 
Umenikumbusha mbali kwakweli, Timothy amenifundisha uimbaji nilipokuwa Mwanza sekondari alikuwa ni storekeeper wa shule lakini pia alikuwa ni mwalimu wetu ktk kwaya ya Ukwata. Miaka ya mwanzoni ya 2000 nilisikia yuko Dar lakini sijawahi sikia habari zake tena zaidi ya kumbukumbu ya kaseti zake alizoimba
Yaani kumbe alikuwa mwanza? Ni mwalimu? Ngoja niulizie pale mwanza sec
 
Ndugu yangu Gashle,
Huyu mtu ni mwimbaji mzuri sana na nyimbo zake zilikuwa zuri za kutia moyo na kuhubiri injili. Baadhi ya nyimbo zake ni:

1. Mwana mpotevu aliomba urithi wake kaenda nchi za mbali.......

2. Ni jambo la kutisha, mtu kuanguka katika mikono ya MUNGU aliye hai....

3. Yote ni Ubatili

4. Lengo moja, kumtangaza YESU

5. Utajakumbuka

6. Ombeni kwa bidii, lazima mtapata jibu
Zinapatikana wapi album zake? Album ya mwana mpotevu ilikuwa balaaa sana
 
Back
Top Bottom