Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Aisee......mimi nilikuwa nachezea timu ya Lion uwanja wetu ulikuwa pale ilipojengwa hospitali ya mwananyamala baada ya kuitanua.

Pale chini palikuwa na timu ya Ajax ya akina Joseph Katuba na Mwangata.

Kitambo sana bwashee!
dah kweli kitambo... sie tulikuwa madogo kiasi so tulikuwa sana sana tunashabikia.. maana mpira ule zaman wa kihuni sana... yaani mpira kuisha mtu kapasuliwa kitu cha kawaida...

mechi zetu za chandimu tunachezea msisiri uwanja wa msufini karibu na kwa fundikira

enzi hizo watoto wa kina fundikira waliotoka ulaya wazungu wa meli .. wanakuja na wachumba wa kizungu pale mtaani
 
ooh kumbe... basi dah tulikuwa hatukatiz usiku ukiwa peke yako...

dah shayawena.. umenikumbusha mbali.. kuna siku ilipigwa mechi pale sikumbuki ilikuwa shayawena na nani... basi ulikuwa mpira wa kihuni kishenz mashabiki tuko pande mbili... watu wana silaha na mawe kila upande ushamuapia refa mpira ukiisha shughuli anayo... basi goma limekole mpira dakika za jion ... wachezaji wanaonyeshana undava ndani... tunasikia filimbi inalia kupuliza mpira kuisha refa haonekani kumbe kapulizia filimbi upande wa pili wa barabara.. barabara ya kuelekea mtaa wa itaga au ukinyoosha unatokea kanisa la walokole.. yeye kasimama pale karibu na ghorofa la wasomali anapuliza filimbi anatoa ishara mpira umeisha...

regards
Zile mechi zilikuwa nomaaa
Nmezicheza sana,uhuni ulikuwa mwingi

Kulikuwa na mhuni mmoja jamaa mfupi alikuwa anaitwa regan, mara nyingi mm nlikuwa nacheza full beki,sasa jamaa muda wote anapita na convoy lake anasema mtu na mtu,man 2 man,asikatize mtu[emoji23][emoji23][emoji23]
Ahh sema kila game kabla kuisha ni vurugu tu maana zile timu wahuni walikuwa wanazitawala sana,ila kama vipaji vingi vilipotea

Ova
 
dah kweli kitambo... sie tulikuwa madogo kiasi so tulikuwa sana sana tunashabikia.. maana mpira ule zaman wa kihuni sana... yaani mpira kuisha mtu kapasuliwa kitu cha kawaida...

mechi zetu za chandimu tunachezea msisiri uwanja wa msufini karibu na kwa fundikira

enzi hizo watoto wa kina fundikira waliotoka ulaya wazungu wa meli .. wanakuja na wachumba wa kizungu pale mtaani
Siwetu fundikira tulikuja kucheza naye sana badaye team za maveteran leaders
Mh msisiri napo kulikuwa na wahuni lkn

Ova
 
Dodoma -mbeya kuna basi lilikuwa linaitwa URAFIKI huyu mh simbachawene alikuwa kondakta wa hilo basi balaa lake sio poa nakumbuka lilituacha comfort tukapanda matema mabichi ngoma imefukuzwa tumeikuta mbeya imetulia [emoji1430]
Huyu huyu Simba chawene?
 
mambo ya tanga na satellite coach alikua ameandika basi zake tatu maneno tofauti ya kwanza aliandika .. "makorora wadeka", ya pili akaandiak "waache wadeke" ... ya tatu akaiandika "makorola ni yao"... pia kulikuwa na basi za tayasar, ngorika, tashrif, na mengine kibao tu... trip dara tanga na

ila mwendo wa mabasi zaman hatari sana... nakumbuka tashrif iliua watu wote kwenye kijiji kimoja karibu na segera.. dereva alipita kwenye daraja liliofunikwa na maji kwa ubishi basi likabebwa...

angalia huyu mzeee hapa chini anavyoponda madereva wa sasa... anakwambia dar - moshi kona ni mbili enzi hizo za dereva uweka mguu kati .. kona ya kwanza segera ya pili chalinze.. kwingine kote unafunika
Daah tayasar satelite chali

Narudia tena biashara ya mabasi waliotoboa mpaka leo hata kumi hawafiki na ukichunguza sana kutoboa kwao aidha wana malori au wanamiliki sheli ili kubusti basi zao.....
 
Hekima ilikuwa inawasha moto haswaa. Nyuma ilikuwa na picha ya Albert Nyirenda anasimika bendera ya Taifa kwenye killer Cha mlima Kilimanjaro.

Hekima kipindi Cha machafuko South Africa enzi za JK zilikodiwa kwenda kuwabeba watanzania walikuwa kule na kuwarudisha bongo.
Duuuh na utajiri ukaongezekea hapo ila cha ajabu zikafa
 
Ile ligi mkuu acha kabisa mbele ilikua Sumry Nissan Diesel ikifuata Hekima halafu Mohamed Trans
Gari zilikua zinatembea hatari Chalinze tulipita kama hakuna kituo vile sasa shughuli pevu ikawa kile kipande cha kutoka Chalinze kuitafuta Ruvu Darajani
Pale ndio nilipoikubali Hekima maana yule wa Simry tulifika sehemu mbele kulikua na lorry halafu kule kuna gari inakuja,wa Sumry akapunguzs kidogo mwendo kwa sababu ya lile lorry,dah Hekima akatanua kulia na mwendo ule ule,Mohamed Trans nae akafuata mwendo ule ule
SUMRY ikabaki nyuma huko.
Hatukuiweza kuipita Hekima mpka tumefika picha ya ndege tulaingia petrol station

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
Mbeya ligi hazijawahi kuisha we hebu fikiria sasa ivi tochi kama zote lakini sauli anachakaza iyo njia vibaya mno
 
Daah we jamaa umenifanya nimekumbuka mbali sana, enzi za akina Scandinavia, Ruvuma line, Tawaqal, Zainabu bus, safari ilikuwa fupi sana enzi hizo pamoja na kwamba muda wa kupanda na kushuka kitonga ulikuwa unakaribiana kutokana na hali upana wa barabara Kuwa mdogo johnthebaptist

Ukiachana na enzi za akina kiswele
umemsahau saibaba
 
Siwetu fundikira tulikuja kucheza naye sana badaye team za maveteran leaders
Mh msisiri napo kulikuwa na wahuni lkn

Ova

yeah kulikuwa na wahuni kama ambao pia walikuwa wacheza boxer, na wahuni wengine wa kawaida kama kina shamba la bangi na wenzie kina dame.... enzi hiyo mitaa ya kino na mwananyamala huwakosi mabondia wengi wa kipindi hicho.. na vitasa vilikuwa vinafanyika ukumbi wa ccm vijana mwananyamala ... na michezo ya nyoka KIBISA
 
Daah tayasar satelite chali

Narudia tena biashara ya mabasi waliotoboa mpaka leo hata kumi hawafiki na ukichunguza sana kutoboa kwao aidha wana malori au wanamiliki sheli ili kubusti basi zao.....
Hii biashara kufilisika ni dk 0 tu!
Ndomana sumry alingia kwenye
Kilimo

Ova
 
yeah kulikuwa na wahuni kama ambao pia walikuwa wacheza boxer, na wahuni wengine wa kawaida kama kina shamba la bangi na wenzie kina dame.... enzi hiyo mitaa ya kino na mwananyamala huwakosi mabondia wengi wa kipindi hicho.. na vitasa vilikuwa vinafanyika ukumbi wa ccm vijana mwananyamala ... na michezo ya nyoka KIBISA
Mzee unapapata sogodo [emoji38][emoji38]

Ova
 
Huyu bwana anaendesha Gari kwa mdogo wa KT Abri waarabu wa iringa, kuna mtu kasema hapo alisababisha ajali ni kweli yeye na marehemu ally kilaweni alikuwa anaendesha basi la Zainabs VOLVO B7, ndio waliisababishia basi ya Shabby ilikuwa inaendeshwa na marehem ROSHI ilipata ajali baada ya mashindano makali pale kona za kukutamisha mkoa wa ruvuma na wilaya ya Njombe, wakati huo sisi Scandanavia tulikuwa tunakuja nyuma pole pole na hiyo ruti nilikuwa nimempokea mzee Okala mzee wa mliyayoyo. Giriki ni halfkast wa kigiriki na kingoni, alipigwa marufuku kabisa kuendesha mabasi na liseni yake alifungiwa miaka 2 na kutangazwa ktk Gazeti la serekali.
 
Huyo jamaa yupo iringa anafanya Nazi kwa waharabu,

Bus LA kistaharabu lilikuwa ni lupelo (kuna picha ya yahane poul ii) upendo na safina ,hekima, nakumbuku tukiwa wadogo kuanzia SAA saba tuko barabaran kushuudia league ,
Scandinavian alikuwa wa kishua tu

Route: dar to mbeya,
 
Uzi ttajir Sana huu, heshima kwa wakongwe wote hapa mmeonyesha kwa kina sana kumbukumbu mlizo nazo za enzi hizo hasa Yohanne mbatizaji mimi sikuwa najua bwana Mbowe ana nyota nyingi hivyo kwakweli
Sasa tuleteeni uzi wa mbabe wa kaskazini enzi hizo
Heshima yenu!!
 
Huyu bwana anaendesha Gari kwa mdogo wa KT Abri waarabu wa iringa, kuna mtu kasema hapo alisababisha ajali ni kweli yeye na marehemu ally kilaweni alikuwa anaendesha basi la Zainabs VOLVO B7, ndio waliisababishia basi ya Shabby ilikuwa inaendeshwa na marehem ROSHI ilipata ajali baada ya mashindano makali pale kona za kukutamisha mkoa wa ruvuma na wilaya ya Njombe, wakati huo sisi Scandanavia tulikuwa tunakuja nyuma pole pole na hiyo ruti nilikuwa nimempokea mzee Okala mzee wa mliyayoyo. Giriki ni halfkast wa kigiriki na kingoni, alipigwa marufuku kabisa kuendesha mabasi na liseni yake alifungiwa miaka 2 na kutangazwa ktk Gazeti la serekali.
Okalla bado yupo bwashee?
 
Mzee unapapata sogodo [emoji38][emoji38]

Ova

hahahaha Sogodo... vichochoro vya mitaa ya msufini hivyo... ukitoka msufini uwanjan... unapitia kinjia cha kwa bibi kimwaz mwaz utaibukia sogodo kama unataka kwenda kino b basi ukatize vichochoro vingine mbele uvuke bwawa uibukie Kino B.... kwenye ile barabara ya ben pub kwenye mtaa mmoja enzi hizo walikuwa wanauza ice cream wanapaita majoka... au karibu na ilipokuwa baa ya mzee fambo kama sikosei
 
Hahaha aise hivi unajua kuna watu wamezaliwa dar hata kino lakini sogodo
Hawapajui,haha pale kuna kila aina ya pombe,malay,wahuni wa kila aina,wakabaji
Washnz wote wapo [emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Back
Top Bottom