Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Aisee......mimi nilikuwa nachezea timu ya Lion uwanja wetu ulikuwa pale ilipojengwa hospitali ya mwananyamala baada ya kuitanua.

Pale chini palikuwa na timu ya Ajax ya akina Joseph Katuba na Mwangata.

Kitambo sana bwashee!
dah kweli kitambo... sie tulikuwa madogo kiasi so tulikuwa sana sana tunashabikia.. maana mpira ule zaman wa kihuni sana... yaani mpira kuisha mtu kapasuliwa kitu cha kawaida...

mechi zetu za chandimu tunachezea msisiri uwanja wa msufini karibu na kwa fundikira

enzi hizo watoto wa kina fundikira waliotoka ulaya wazungu wa meli .. wanakuja na wachumba wa kizungu pale mtaani
 
Zile mechi zilikuwa nomaaa
Nmezicheza sana,uhuni ulikuwa mwingi

Kulikuwa na mhuni mmoja jamaa mfupi alikuwa anaitwa regan, mara nyingi mm nlikuwa nacheza full beki,sasa jamaa muda wote anapita na convoy lake anasema mtu na mtu,man 2 man,asikatize mtu[emoji23][emoji23][emoji23]
Ahh sema kila game kabla kuisha ni vurugu tu maana zile timu wahuni walikuwa wanazitawala sana,ila kama vipaji vingi vilipotea

Ova
 
Siwetu fundikira tulikuja kucheza naye sana badaye team za maveteran leaders
Mh msisiri napo kulikuwa na wahuni lkn

Ova
 
Dodoma -mbeya kuna basi lilikuwa linaitwa URAFIKI huyu mh simbachawene alikuwa kondakta wa hilo basi balaa lake sio poa nakumbuka lilituacha comfort tukapanda matema mabichi ngoma imefukuzwa tumeikuta mbeya imetulia [emoji1430]
Huyu huyu Simba chawene?
 
Daah tayasar satelite chali

Narudia tena biashara ya mabasi waliotoboa mpaka leo hata kumi hawafiki na ukichunguza sana kutoboa kwao aidha wana malori au wanamiliki sheli ili kubusti basi zao.....
 
Duuuh na utajiri ukaongezekea hapo ila cha ajabu zikafa
 
Mbeya ligi hazijawahi kuisha we hebu fikiria sasa ivi tochi kama zote lakini sauli anachakaza iyo njia vibaya mno
 
umemsahau saibaba
 
Siwetu fundikira tulikuja kucheza naye sana badaye team za maveteran leaders
Mh msisiri napo kulikuwa na wahuni lkn

Ova

yeah kulikuwa na wahuni kama ambao pia walikuwa wacheza boxer, na wahuni wengine wa kawaida kama kina shamba la bangi na wenzie kina dame.... enzi hiyo mitaa ya kino na mwananyamala huwakosi mabondia wengi wa kipindi hicho.. na vitasa vilikuwa vinafanyika ukumbi wa ccm vijana mwananyamala ... na michezo ya nyoka KIBISA
 
Daah tayasar satelite chali

Narudia tena biashara ya mabasi waliotoboa mpaka leo hata kumi hawafiki na ukichunguza sana kutoboa kwao aidha wana malori au wanamiliki sheli ili kubusti basi zao.....
Hii biashara kufilisika ni dk 0 tu!
Ndomana sumry alingia kwenye
Kilimo

Ova
 
Mzee unapapata sogodo [emoji38][emoji38]

Ova
 
Huyu bwana anaendesha Gari kwa mdogo wa KT Abri waarabu wa iringa, kuna mtu kasema hapo alisababisha ajali ni kweli yeye na marehemu ally kilaweni alikuwa anaendesha basi la Zainabs VOLVO B7, ndio waliisababishia basi ya Shabby ilikuwa inaendeshwa na marehem ROSHI ilipata ajali baada ya mashindano makali pale kona za kukutamisha mkoa wa ruvuma na wilaya ya Njombe, wakati huo sisi Scandanavia tulikuwa tunakuja nyuma pole pole na hiyo ruti nilikuwa nimempokea mzee Okala mzee wa mliyayoyo. Giriki ni halfkast wa kigiriki na kingoni, alipigwa marufuku kabisa kuendesha mabasi na liseni yake alifungiwa miaka 2 na kutangazwa ktk Gazeti la serekali.
 
Huyo jamaa yupo iringa anafanya Nazi kwa waharabu,

Bus LA kistaharabu lilikuwa ni lupelo (kuna picha ya yahane poul ii) upendo na safina ,hekima, nakumbuku tukiwa wadogo kuanzia SAA saba tuko barabaran kushuudia league ,
Scandinavian alikuwa wa kishua tu

Route: dar to mbeya,
 
Uzi ttajir Sana huu, heshima kwa wakongwe wote hapa mmeonyesha kwa kina sana kumbukumbu mlizo nazo za enzi hizo hasa Yohanne mbatizaji mimi sikuwa najua bwana Mbowe ana nyota nyingi hivyo kwakweli
Sasa tuleteeni uzi wa mbabe wa kaskazini enzi hizo
Heshima yenu!!
 
Okalla bado yupo bwashee?
 
Mzee unapapata sogodo [emoji38][emoji38]

Ova


hahahaha Sogodo... vichochoro vya mitaa ya msufini hivyo... ukitoka msufini uwanjan... unapitia kinjia cha kwa bibi kimwaz mwaz utaibukia sogodo kama unataka kwenda kino b basi ukatize vichochoro vingine mbele uvuke bwawa uibukie Kino B.... kwenye ile barabara ya ben pub kwenye mtaa mmoja enzi hizo walikuwa wanauza ice cream wanapaita majoka... au karibu na ilipokuwa baa ya mzee fambo kama sikosei
 
Hahaha aise hivi unajua kuna watu wamezaliwa dar hata kino lakini sogodo
Hawapajui,haha pale kuna kila aina ya pombe,malay,wahuni wa kila aina,wakabaji
Washnz wote wapo [emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…