Yule aliyemjibu rais Magufuli kwenye ile video ya jana ni nani?

Eti mama janet hana sauti, wabongo mnapenda kuteseka sana hata kwa vitu visivyowahusu[emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia inaonyesha alikuwa amezibugia za kutosha
 
Yule hakukataa kushangilia ila,alikuwa anakataa kupigwa au kuchukuliwa video
Mkuu yule ni mtumishi wa IKULU..kilichotokea pale ni Mhe Rais alikuwa na furaha sana na alitaka kuwashirikisha furaha yake watu wengine na watu pekee waliokuwepo pale ni wale wasaidizi wa jikoni. Kiutaratibu watumishi hasa wa serikali hata kama bosi wako hupaswi kupeana nae pongezi ile ya kugongeana au kupeana tano au kushangilia kwa kujisahau.
Hivyo basi yule mtumishi alikuwa anakimbia ili hilo la kugongeana na bosi lisitokee, ni masuala tu ya Kiitifaki hayo.
 
Ha
Zile raba aliyemnunulia Pepo hataiona walahii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahah Raba za Anko Magu mbona mnazidiss wakati sikuhizi mnavaa raba za ajabu kuliko zile. Angalia mi raba anayovaa diamond ukiacha ile ya pepsi. Shapeless!
 
Kaka ile kofia mimi haijanishangaza sana, ila ULE MRABA ALIOVAA, ha ha, halafu mwenyewe anajiona ametokelezeeeeea, kumbe ni kituko.
Bujibuji kaongea lugha inayokaribiana na ukweli.Simba pamoja na kufika robo fainali,ujue kuna wachezaji wa nje.Jana Taifa Stars ndio picha halisi ya soka la Tanzania.Taifa Stars ikiwezeshwa ukiuwekezaji wa nguvu,timu itatisha sana.Lakini hizi timu kongwe Yanga na Simba kila mara ni migogoro na mitafaruku tu hasa Yanga.Uchaguzi wa viongozi haufanyiki kila mara migogoro tu.Wanachama wapo wengi lakini "contribution" katika timu ni zero.Timu ina hali ngumu kiuchumi,wanachama luluki hawaichangii timu chochote kwa madai kuwa timu ni ya wanachama.Kwa hiyo mifumo ya uendeshaji wa timu ni vyema kubadilishwa ili timu zijiendeshe kwa malengo ya ushindani na kuiletea nchi sifa na fursa za kiuchumi.

Kwa hiyo hizi timu na migogoro yao haina tija kwa nchi bali kwa baadhi ya viongozi na matumbo yao.Hata hiyo Simba unayoisema imekuwa jibwa koko,kaa ukijua kuwa nayo ikiwekewa mfumo mzuri zaidi wa uendeshaji,itafanya vizuri zaidi ya hapa ilipofikia.Wakiguswa na Serikali tu,utasikia tutafungiwa na CAF/FIFA kwa sababu Serikali haitakiwi kuingilia masuala ya Michezo.Lakini huwa wakikwama katika matukio ya kimichezo utasikia Serikali iwasaidie,sawa na msemo usemao baniani mbaya kiatu chake dawa.Tuwaze nje ya box kwa masilahi mapana ya nchi yetu badala ya kujisudujia wenyewe/viongozi na mitumbo yetu mara zote.

Mkuu,hahahahahaha!!!Au unadhani kuwa chakula tunachokula kina uhusiano au hakina uhusiano na harufu ya KINYESI???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu matatizo yote yanga yanaletwa na mzee akili mali
 
Kaka ile kofia mimi haijanishangaza sana, ila ULE MRABA ALIOVAA, ha ha, halafu mwenyewe anajiona ametokelezeeeeea, kumbe ni kituko.
Angevaa gunia,ngozi,bukta,singlendi,kandambili na iwayo vyovyote l vile,lakini yeye ndio kiongozi wetu mkuu kuanzia baba yako,mama yako,shangazi yako,mchepuko wako,binamu yako,mjomba wako,kaka yako,wewe,mimi,wale,yule n.k na yeyote ambaye ni RAIA wa Tanzania hii.Kwa hiyo kuvaa kwake haina uhusiano na ujumbe uliotakiwa kutufikia Watanzania.Tutakosoa mpaka visivyo na tija hata tukiona anakunywa maji.Ya family tuyaache hukooo hayatuhusu kwani kila binadamu(kikatiba) anatakiwa awe na ufaragha wake.

Raba,raba,raba,raba,kofia,kofia,kofia.Huenda ukiambiwa kampuni iliyotengeneza na bei yake utashangaa na usimpo/zilivyo hivyo hutaweza kununua,lakini humu jamvini bla blaa kibaoooo!!!!

Yote ya yote,Taifa Stars itaenda Afcon 2019 Cairo,Misri au haitaenda?Jibu ni kuwa itaenda,zingine blabla tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu, wabongo wana majungu sana, raba zile, nguo zile wao zinawahusu nini, wao wanaweza kuona za kawaida lakin ukienda dukan bei yaor haishikiki, wanadhan amenunua karume
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…