Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Baadhi yetu tuna kumbukumbu fulani za mpenzi yule ambaye unajuta hadi mtondogoo kwanini hamkuoana. Mlipendana, mlipeana, mliliwazana, mliinuana hadi familia ziliweka alama za tiki. Kila mtu mtaani alijua nyinyi ni wenza.
Mara puu!! Hamkufunga ndoa si kwa kuachana au kugombana yaani hadi kesho mnashindwa kuhalalisha kwanini hamkuzaa hata katoto ka mfano!
Mlivyo na wazimu wa mapenzi mmekutana ukubwani na wengine na ndoa zenu lakini mnakumbushiana. Kuna wengine wamefikia hatua ya kuacha ndoa zao na kulirejesha libeneke.
Unamkumbuka yupi na kwanini hamkuishia kufunga ndoa na kuishi na majuto...