Naam, ni kutoka kwenye Biblia, pia yasema " Wema watawalapo watu hufurahi ila waovu watawalapo, watu huugua. Katika kutafakari neno hili nami nikaona si watu linalougua bali wapenda haki ndio wanaougua, yaani kuteseka. Wale waovu , wanaonufaika na uovu na wale wajinga ambao hawafaidiki chochote isipokua kushabikia wenye haki watendewapo maovu, hao hufurahi.
Imani ya Bwana ikawe nawe katika utafutaji wako wa mtake wa kila siku, ujiweke mbali na dhulma kwenye haki za wengine, kwani kutenda hivyo, ni chukizo kwa Bwana.