Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

EPISODE 3

Kabla sijawaeleza namna nilivyoya terorise maisha ya mzee Kipipa hadi kufikia kupoteza fahamu kwa presha na jinsi nilivyomuwashia moto kwa kutumia pesa na connections zake hadi akafikia wakati fulani kufanya jaribio la kuikimbia nchi ili awe mbali na mkono wangu ningependa kwanza kumtambulisha kwenu mama yangu mzazi.

Mama yangu mzazi, Sophia ni binti wa kisambaa aliyezaliwa katika familia ya watoto 18.

Babu yangu mzaa mama alikua ni mzee tajiri wa kiislam aliyeishika dini ya kiislamu hasa hasa hasa.

Babu yangu aliyekua na wake wanne alikua anaheshimika sana na kuna msikiti mpaka leo una jina lake ambao yeye babu yangu aliujenga.Mbali ya kujenga misikiti babu yangu anakumbukwa kwa kutoa misaada kwa wasiojiweza.

Wake na watoto wote wa babu yangu waliishi kwa kufuata maadili na misingi ya dini ya kiislamu isipokua mtoto wake mmoja tu,Sophia.

Sophia alikua tofauti na alivyotamani baba yake kwani pamoja na kuzaliwa kijijiji tena katika familia bora ya kiislamu yeye alitokea tu kuwa na tabia za ki slay queen.Mambo ya kuvaa majuba na ushungi yalimshinda Sophia.

Sophia alijijua ana umbo na sura nzuri na alipenda dunia ilione umbo lake hivyo vimin na visuruali vya kubana ndo zilikua pigo za Sophia.

Mbali ya uslay queen wa kuzaliwa nao Sophia pia alizaliwa na roho ya kijasiri.Ukimzingua ndugu yake yeyote Sophia alikua anakufata na kukuzingua na wewe.Pamoja na ufupi wake ila Sophia alikua haogopi kupigana na wanaume na alikua ana kauli yake anasema "mimi napigana na wanaume wanawake wenzangu sipigani nao bali nawapiga" .
Baada ya babu na wazee wengine wa kiislamu kumuonya Sophia bila mafanikio babu akamfukuza Sophia nyumbani kwake.

Sophia akaenda kuishi nyumban kwa kina rafiki yake aitwae Hosana.Huyu Hosana alishaondokaga na kwenda kuishi Dar ambako alikua anafanya kazi za ndani lkn wakati Sophia alipoenda kuomba hifadhi pale alikua amekuja mara moja kusalimia wazazi wake na kuwaeleza kuwa ni mjamzito na kwamba kwa sasa kuna mwanaume wanaishi nae huko Dar na wana mpango wa kuoana.

Hosana akamaliza siku zake pale kijijini na kuondoka kwa ahadi ya kumtafutia kazi Sophia.

Sophia aliendelea kuishi na mama wa Hosana na baaada ya muda Hosana akampatia kazi ya u housegirl huko Dar na nauli ilipotumwa Sophia akaingia Dar na kwenda kuish kama housegirl.

Hata hivyo Sophia hakuwa anadumu kwenye kazi sbb ya kushindwa kuvumilia manyanyaso na kubaguliwa.Kuna siku alimchamba mama mwenye nyumba ambae alikua mchoyo na mwenye roho mbaya ya kutaka Sophia ale viporo hata vilivyo chacha.Sophia alivumilia kidogo ustaarabu ukamshinda siku ya siku akamwambia yule mama"Baba yangu ana uwezo wa kukulisha wewe,mumeo,watoto wako na koo zenu zote mpaka siku mnakufa!Usinione hapa kwako ukadhani nimekimbia njaa kwetu!".

Kwa hiyo Sophia alikua ana kazi ya leo ni housegirl nyumba hii kesho nyumba ile lkn wakati wote huo Hosana ndie shoga ake mkuu hapo mjini Dar.Kitendo cha Sophia kwenda kumtembelea Hosana mara kwa mara kikafanya Sophia atambulike kwa shem wake mume mtarajiwa wa Hosana.

Umbo namba 6 la Sophia na weupe wake wa kisambaa ukamchanganya mume mtarajiwa wa Hosana.Akamtongoza na kumuahidi kumpangishia chumba na kumpa mtaji wa biashara aachane na kazi za u housegirl.Sophia akapiga mahesabu akachekecha akaona hata yeye anatamani kuishi kwa bata kama shogake Hosana, akakubali.

Baada ya kupangishiwa chumba na kuanza kuhudumiwa Sophia akatamani ampindue kabisa shogake abaki yeye lakini kila alivyojitahidi kumtoa Hosana alishindwa.Badae akagundua Hosana ana thaminiwa na yule mwanaume wao sbb amemzalia mtoto hivyo miaka miwili na kitu hivi baadae na yeye akashika ujauzito na hatimae akazaa katoto kake kazuri ka kike akakaita Clepatina.

Mpaka Clepatina anazaliwa ndio Hosana ambae ndie mama yake na Prince Chibonge alipopata majibu ya kwanini mipango ya kuolewa na baba Prince Chibonge ilivurugika ghafla na ndipo alipojua kumbe Sophia ndiye sababu ya baba Prince Chibonge kupunguza mapenz yake kwake na ndio alipojua ya kwamba kumbe na Sophia amezaa na baba Prince Chibonge.

Urafiki wao ukazikwa rasmina uadui wa kuapizana na kutamkiana kutoana roho ukazaliwa kati yao na kila mmoja wao akawa anatumia kila mbinu aolewe yeye.Mama Prince Chibonge yeye kila siku alikua anaenda kwao kuloga na mama Clepatina yeye kazi yake ilikua kumuonyesha mwanaume wao madanga ya Hosana ili tu aonekane sio wife material.

Amani ikatoweka kwenye nyumba za wanawake zake wote.Akienda kwa mama Prince Chibonge anatuhumiwa hivi,akirudi kwa mama Clepatina anatuhumiwa hivi.Alivyoona makelele yamezidi akawabwaga wote.

Baada ya kuwaacha hawa wanawake haikuchukua muda mrefu faza akasimamishwa kazi.Akawa choka mbaya anashinda Bar na vijiwe vya madalali.

Hawa wanawake nao kila mmoja akawa anahangaika kivyake kupata hela ya kulisha mwanae.Mama Prince Chibonge yeye akajikita kwenye biashara ndogo ndogo na mama Clepatina yeye akaangukia kuwa muhudumu wa Bar.

Hata hivyo mama Clepatina hakuwa muhudumu wa Bar wa kawaida na hakwenda kuomba kaz ya kuuza Bar bali kuna mwenye Bar alimuona alivyo akajua huyu binti akikaa kwenye Bar yangu wanaume watakua wanapanga foleni hivyo akamshawishi akafanye hiyo kazi kwa dau kubwa.

Kwa Kweli Sophia alikua Bar maid mwenye viwango.Alikua slay queen kweli kweli na msambaa yule ni ana maringo mpaka leo hii.Mama yangu ilifikia level akawa ana drive kwenda kazin kwake Bar kuhudumu na alikua anaishi kwenye bonge ya jumba ila la kupangisha na alikua na housegirl wa kumlelea Clepatina wake.

Hichi ndo kipindi Siphia alikua Sophia kweli.Mweupeee,softiii,sura sasa na ukija kwenye hilo umbo la namba 6 halafu ujumlishe na midhahabu aloijaza mwilini plus mavazi ya gharama na uchanganye na zile nyodo zake weeuwee!

Mama Clepatina akapata dili ya kwenda Afrika kusini ila haikuwa safari ya kuweza kwenda na mtoto.Ikabidi tusafiri kwenda mpaka usambaani kwa lengo la kwenda kuniacha kwa babu na bibi ili yeye akatafute maisha South.Mpaka wakati huo babu alishafulia na maisha yake yalikua yakutegemea watoto na katika watoto wake wote mama yangu Sophia ndo alikua na pesa kuliko wote.

Basi tulifika pale nyumbani kwa babu na pick up ikiwa imejaa mazagazaga kama yote ya zawadi.Viroba vya michele,vya sukari,ndoo za mafuta,mabox ya sabuni na kila takataka.Watu wa kijijini pale wakawa wanamshangaa mama yangu jinsi alivyokua kajiweka weka minywele na visuruali vyake vya kubana nakwambia alikua anajiona kama mzungu mapozi kama.yote.

Kwa mshangao mkubwa babu alivyotoka pale uwani mama alininyanyua kwa lengo la kumpa babu anibebe lakini babu alikataa kunipokea kisha akamwambia anaingia ndani kuswali ila akitoka tena nje asimkute yeye Sophia wala chochote alichokuja nacho kikiwa kimebaki pale nje kwake.

Mama alilia sana,kina bibi wakaongea na babu lkn haikusaidia na mwishowe ile pick up ikaenda kupaki kwenye nyumba ya mzee fulani ambae alikua rafiki kipenzi wa babu na mama akaomba aombewe msamaha.Tukiwa pale babu akapita akielwkea sehemu na swahiba wake akamsihi sana amsikikize Sophia hata kwa dakika moja.Baada ya kuombwa sana babu akakaa kusikiliza.

Katika kusikiliza maelezo ya mama babu akamwambia mama kwa sababu lengo lako la kuja halikua kuomba msamaha bali umekuja kutubwagia mwanao ili ukahangaike na anasa zako kwa uhuru ondoka na mwanao na siku ukiona haja ya kuomba msamaha funga safari nyingine uje uombe msamaha.Na siku utakayokuja unijie kama binti wa kiislamu.

Babu akaniita,nikaenda akanibeba akaniuliza unaitwa nani?Nikamwambia naitwa Clepatina.Akaniambia la hasha!wewe unaitwa Yusra!Nimesema unaitwa nani?Ninaitwa Yusra.Akasema naam!Yusra! Yusra ukue na uwe mashuhuri na mwenye mafanikio uendane na jina lako.Akanibusu kwenye paji la uso kisha akanisomea dua na mwisho akanipa na hela yakununulia biskuti.

Alipomalizana na mimi babu yangu akamuaga jamaa yake akasimama bila kumwambia mama chochote na polepole akaanza kuondoka kuendelea na safari yake.
Maza akabaki pale huku machozi yakimlengalenga lkn mwisho wa siku tulirudi Dar huku maza akiwa hajui akaniache wapi maana ndugu zake wote waliogopa laana ya babu iwapo wangenipokea wakati yeye alikataa.

Tulirudi Dar maza akiwa na ma stress kama yote.Alinipenda sana na hakutaka kuniacha kwa mtu asiye na uhakika.Siku ya siku nikaona maza kafungasha nguo zangu na vikolokolo vyangu vyote kisha akaniambia "Utaenda kukaa na baba halafu nitarudi kukuchukua".
Basi tukaingia kwenye gari yake akawa anapita kwenye vijiwe vyote ambavyo dingi anakaaga lakin hatukumkuta lkn baada ya kuzunguka zunguka tukafika kwenye ki statinery fulani ambayo ni moja ya vijiwe vya dingi.Ile kufika tukamuona faza anatokea ndani ya ile stationary akielekea ilipo paki gari fulani ya rafik yake na dingi,alikua kapata lift ya kumsogeza mpaka sehemu fulani.Ile dingi kuingia tu na kukaa kabla hata hajafunga mlango maza akaninyanyua fasta na kwenda kunibwaga mapajani kwa dingi.Kabla faza hajaelewa nini kinaendelea maza akawa anakuja na vimfuko anavirushia mle ndan ya ile gari,wanadaka anakuja na vingine anamtupia faza usoni,mwishowe akachukua kibegi changu akamtwishwa faza kichwani huku anamkandamizia lile begi kama anataka kumvunja shingo,dingi hasira zikampanda akawa anataka kutoka akampige maza lkn maza fasta akarudi kwenye gari yake akatutimulia vumbi akapotea.Yule mshikaj wa ding alotoa lift alikua anajjzuia kucheka wakat anadaka viatu na vimfuko anavyokua akirusha maza.

Maza alivyoondika Faza na yule rafik yake wakaangaliana kwa muda kisha yule rafik akampa pole kisha akamuuliza nikakuache wapi.

Baada ya hapo dingi akatafuta mpaka akaipata nyumba tuliyokua tukiishi na maza lkn kufika akaambiwa Sophia haishi tena hapa.Dingi akanitangisha tangisha wee mara leo aniache kwa mama Ntilie mara leo aniache kwa binamu yake mara leo aniombee kwa nani sijui na mwishowe akapata wazo la kurudiana na mama Prince Chibonge.

Wakarudiana na mama Prince Chibonge akawa step maza wangu rasmi.

Step maza alirudiana na dingi wakati dingi akiwa kafulia choka mbaya kwa hiyo step maza ndo alikua anatulisha sote kuanzia mim,dingi na prince Chibonge wake.

Muda mfupi baada ya faza na step maza kurudiana faza akalipwa hela walizokua wakidai huko kazin kwao walikosimamishwa na alipopata hizo pesa akaamua kurudi bush kwenye nyumba ya urithi ya baba yake kwa lengo la kuwekeza kwenye kilimo.Step maza akaacha mishe zake alizokua akifanya Dar na kuambatana na faza na sisi watoto wao.Huko kijijini ndo kule tulikoishi jiran na nyumba ya mzee Kipipa.

Siku za mwanzon tulivyohamia bush na wakati huo dingi alikua pia yuko, step maza hakuwa akionyesha kunichukia.Alitulea sawa kwa upendo.

Shida ilianza dingi alipoanza kuzingua, maana tuliingia bush dingi akiwa na mshiko.Basi dingi akawa na michepuko kibao na muda si muda akafulia na malengo ya kuwekeza kwenye kilimo yakafifia.Hapo ndo step maza akaanza gubu.Hasira za dingi ananitolea mim,kosa kidogo tu utasikia "we si mbwa tu kama baba yako"!Mara usikie ",mtoto wa nyoka ni nyoka tu,nahangaika na wewe hapa ila kuna siku utakuja kuning'ata tu kama mama yako wewe!"

Huku na huku faza akaona pale kijijin haiwezekan tena,ktk kuongea ongea na jamaa zake akapata kaz ya mkataba wa mwaka mmoja Dar.Mwanzoni akawa anatutumia matunzo na akawa anakuja mara moja moja kutuona ila badae ikawa hatumi pesa wala salamu.

Mara ya mwisho dingi kurudi,ukiachana na ile alivyorudi wakat step maza anaumwa(ep. 2).
ilikua ni wakati ambako step maza alisema ana ujauzito.Na dingi anadai habari za hiyo mimba ndo zilifanya amuache step maza kwani mtoto sio wake na kwa maana hiyo ilimaanisha step maza alikua akimsaliti dingi.Step maza analazimisha watu kuwa Tide anafanana na dingi ila ukweli Tide hafanani na dingi wala mama yake.Prince Chibonge na mim ndo tunafanana na faza etu kuanzia sura mpaka u giant.Mim na Prince chibonge tumeenda hewan kama dingi etu.

Basi ndo hivyo step maza akatelekezwa pale na wanae na mwana wa kambo na maisha yakawa yakuunga unga mara ajaribu kulima mara ajaribu vibarua mradi shida tupu.

Mama yangu Sophia nae kwa upande wake.Ile safari yake ya south haikufanikiwa bali alikwenda Kenya ambako huko mambo hayakua kama ilivyotarajiwa.Ikabidi arudi bongo lkn alivyorudi hakuwa yule Sophia aliyetikisa jiji bali alirud amechoka hana gari wala uwezo wa kupangisha mansion kama mwanzo.Akawa Bar maid kama Bar maid wengine tu.

Jeuri ya kunichukua akawa hana na dingi nae kwa upande wake alinasa kwa mwanamke aliyemwambia hataki kulea watoto wa kambo hivyo nika stack na step maza.

Mama yangu mzazi Sophia ni kama alisahau kama ana mtoto na kuna wakati nilifikiri amekufa wananificha.

Baada ya juhudi za kumtafuta mama yangu kugonga mwamba nilikuja kukutana nae nikiwa na miaka 17 huku nikionekana kama dada wa miaka 25 sbb ya urefu.Hapo tayari nina nyumba yangu ya kwanza.

Siku nakutana na mama yangu Sophia ilikua nimeenda kuoneshwa Bar yenye guest house ambayo mmiliki wake alikua anaiuza.Pamoja na kuwa ilikua inauzwa lkn bado ilikua ikifanya kaz japo biashara ilikua inapumulia mashine.

Mtu aliyenishaur niinunue aliniambia niinunue niikarabati then niigeuze hostel coz haikua mbali sana na chuo fulan kikubwa.

Tulipofika eneo hilo tukiwa tunatafuta sehemu ya kupaki gari ghafla akatokea mwanamke na mwanaume wanapigana.Mwanaume alionekana anataka kuondoka lakin mwanamke akawa anamdhibiti asiondoke.

Mwanamke alikua ni kadada keupe kafupii kamevaa kaptura.Kanarusha vichwa balaa na kuna saa kalirusha kichwa cha pua hadi mwanaume damu za pua zikaanza kumtoka.Mwanaume alivyoona damu akawa kama tembo aliyejeruhiwa. Akajiweka sawa kisha akatuma ngumi moja ambayo haikua na lengo la kuumiza bali kuua lkn yule dada akainama ikapita.Ile ngumi ilivyopita mwanaume akawa anamsogelea mdada kwa jazba amkamate lkn dada akacheza na timing ya hatua za yule kaka akamtegea mguu na kaka akayumba na
kudondoka.

Yule mwanaume alivyodondoka ndo wanawake wenzake wakaja kumsaidia kumtaitisha yule mwanaume wakamsachi na kumpora hela zote kisha wakaondoka huku wanasema "mshenzi kweli huyu kwa hiyo alijua tutamjacha aondoke bila kulipa".

Tukapaki gari na kwenda mapokezi ambako tulimkuta yule dada aliyekua akipigana akijisugua na barafu usoni mana alipata ngeu.

Mimi na yule dada aliyekua akipigana macho yetu yalivyokutana tukabaki tunaangaliana kama masanamu kisha tukarukiana na kukumbatiana huku tukilia kisha tukaanza kucheka kisha tukalia tena.

Alikua ni Sophia mama yangu mzazi.Pamoja na miaka mingi kuisha hakuna aliyemsahau mwenzie.

Pale mahali nilipanunua na mama Sophia ndie msimamizi wa hiyo investment.Yupo vizuri kazini na huwa namtaniaga kuwa akileta uzembe kazini kaz hana.Siku hiz ana drive tena,nyodo kama kawa na anapenda bata na ukimuina utadhan yuko 30s kumbe ni mid 40s.

Step maza na mama yangu kwa sasa wote nawapenda.Nimewasamehe wote ila shida iko upande wao.

Mpaka leo eti bado wanamgombea dingi😂.
Yaani nina kazi ya kuwapatanisha kila siku na watajifanya wamepatana bla bla sasa hv sisi ni watu wazima lakin ikitokea tu siku wamekutana kwangu halafu ukawaacha peke yao hata nusu saa tu lazima walianzishe waanze kutukanana kisambaa.

My cute sisy Joannah darling broda Half american my guy Equation x bestie cocastic dokta Dr. Mariposa Gily Analyse Watu8 Glenn Depal Shunie InvisibleTarget Chizi Maarifa bitimkongwe len Lovie Lady Unique Flower

meaganita NALIA NGWENA wao ni wao Nkundwe Sr makwega7 Grahams @notfeyk Urban Edmund To yeye Lexus SUV Darlin Dr. restart dadapesa Zabron Hamis Doctor G Mwanagenzi Mgibeon


atlas copco Jogoo wa Shamba II TUMBOO Wagumu Tunadumu Omulasil Palina Rashid jololo Mubby777 Aaliyyah @makwenga aker2011 Mnyamb o HOPECOMFORT Sir Carter Ironbutterfly Angel Nylon Winnone Walas Ba
 
Huyo kipipa nahisi unanizungumzia mimi Hata mimi ni kipipa😬
 

Nmefika japo kwa kuchelew kipind, ngoj nitulie sas tuendlee tulipoishia
 
Pole sana mkuu[emoji22][emoji120][emoji120]
Nimesoma hii simulizii zaidi ya mara 20 siku 5 tofauti ikijumuisha na leo.
Kila nikisoma inanitonesha madonda ya makovu niliyowai kutendwa na wapendwa wangu[emoji24][emoji24]
Maisha ya dunia hii yanamambo mengi sana yanayofanyika huko sirini
Mungu atusaidie[emoji120][emoji120]
 
Pole sana mkuu.
Maisha yana siri nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…