Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

Ujue nini mkuu.

Huwa naamini naamini ya kwamba Mungu ana uwezo wa kuzuia tusipatwe na lolote baya hivyo lolote baya linapotupata yeye kwa sababu anazozijua huwa anakua ameruhusu litupate akijua tunaweza kuyashinda na pia huhakikisha no mata wat roho zetu haziguswi na huwa anatuandalia tuzo mwishoni.Nadhani unafahamu kuwa ni Mungu aliyeruhusu Ayubu ajaribiwe ila akatoa sharti kuwa roho yake isiguswe.

Mungu wetu ni mwema,anatupenda na kutuwazia mema hata wakati tunapodhani yuko mbali nasi ila ukweli hajawahi kukaa mbali nasi.

Dhahabu ili ing'ae shurti ipitishwe kwenye moto mkali.
Namshukuru Mungu kwa yote,vicheko na hata machozi pia.

Tufanye mchakato nikubless japo visa stamp ya debunga mkuu.[emoji120]
for sure sista [emoji1478]Tukimuabudu yeye hatumuongezei chochote, na tusipomwabudu hatumpunguzii chochote, YEYE ambaye hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ile YEYE, Yu hai na ni wa kudumu, halali wala kupatwa na usingizi. haelezeki kwa ukamilifu kwa sababu hata sisi tunaojarbu kumuelezea hatujakamilika, tunaelezea kwa kadiri ya imperfection zetu

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
EP. 4

Kwa mliosoma story yangu ya Mzee Kipipa Ep. 3 kuna mahali nilieleza kuwa nilimsumbua sana mzee Kipipa mpaka akataka kukimbia nchi.

Nitakuja kueleza kwa kirefu ila kwa kifupi ni kwamba kuna siku chuki dhidi ya mzee Kipipa na uncle ikawaka na kiu ya kisasi ikawa kali kiasi nikatamani nione wakilipa kwa waliyonifanyia.Kuna nurse fulani wa hospital ya mission aliyenitibu wakati nimepata ile infection na mmoja wa aliyekua akinibembeleza nitaje anayeniingilia ila kama mnakumbuka nilikataa kutaja lkn siku hii roho ya kulipa kisasi ikanijaa na mbio nikaenda hadi pale hospitali kumtafuta yule nurse.

Nilipofika kwa nurse nikamwambia niko tayari kutaja watu wanaoniingilia ila nikamuomba aniambie kwanza kama nikiwataja watafanywa nini?

Nurse akanitizama kwa muda akinisoma kujua lengo la swali langu kisha badala ya kunijibu akaniuliza"Wakipewa adhabu kali utawaonea huruma au utafurahi?".
Nikajibu nitafurahi kisha akasema"Ikidhibitika kuwa ni kweli wanakufanyia hivyo watafungwa jela"
.Nikajikuta naropoka "Hata wakifungwa jela bado sitakua na furaha".
Nurse:Wakifungwa jela hawataweza kukubaka tena wewe au watoto wengine
Mimi:Sawa lakini natamani wapate adhabu ambayo itanifanya niwe na furaha!
Nurse:Kwa hiyo Clepatina mwanangu unafikiri adhabu gani itakufurahisha wakiipata mbali ya jela.

Baada ya yule Nurse kuniuliza lile swali nilisimama nikatizama chini kwa muda kisha nikanyanyua kichwa kumtizama na kwa upole nikamjibu"Kusema ukweli sista kwa sasa sijui adhabu inayowafaa ila ninachokijua kwa hakika ni kuwa adhabu ya jela haiwatoshi" kisha nikapiga alama ya msalaba kisha nikageukia mlango nikaanza kutoka kuelekea nyumbani kwetu.

Sista yule alinikimbilia,akanishika na kunibembeleza niwataje wanaonibaka na kuniahidi mambo mengi mazuri iwapo nitawataja ila nikagoma na kurudi zangu home.

Nilipofika home nikaenda hadi kitandani kwangu nikajitupa nikaliaaa kisha nikajifuta machozi nikakaa nakuwaza ni nini kikifanyika kwa mzee Kipipa kitanifurahisha.

Nilitamani niwafungie sehemu halafu kila siku nikiboreka niwe naenda kuwatesaaa waumiee walieeee waniombe msamaha halafu siwasamehi.Nilitamani wapate wapate mateso hadi watamani kufa ila wasife.

Niliwaza na kuwazua mpaka usiku ukaingia na kukacha ila sikupata jibu la adhabu ipi ni kali kuliko jela ila moyoni mwangu kuna sauti (nina hakika ni ya shetani) ilikua inanipa moyo kuwa nisijali adhabu ya kuwafaa itapatikana tu cha msingi nisiwasamehe,nisikate tamaa na nihakikishe hawaendi jela.

Hakuna siku iliyopita bila kufikiria adhabu ya kumpa mzee kipipa na siku moja nikiwa naangalia filamu ya kimarekani kuhusu mafian cartel of mexico kwenye tv aliyonunua step maza kwa pesa za mzee Kipipa na pamoja na kuwa sikua najua kiingereza ila kwa vitendo tu nilipata wazo la nini cha kumfanyia mzee Kipipa.

Hawa Mexican mafian cartel waliku a wanafanya maasi kujipatia pesa zisizohesabika kiasi kwamba hata serikali haikuweza kuwagusa.

That movie Inspired me to be a mafia.I wanted money too sababu niliamini kama sio umasikini nisingepitia niliyopitia na niliamini nisipokua na pesa nitaendelea kunyanyasika maisha yangu yote na moyo wangu haukua tayari kuendelea kuteseka zaidi ya nilivyoteseka.

I hated umasikini sbb huo ndio uliosababisha nipitie niliyopitia.Hivyo nilitaka umafia wangu niutumie kumuadhibu mzee Kipipa kwa style itakayonitoa kwenye umasikini.

Hapa nilikiwa na kama 14 yrs hivi na tayari nilikua nawaza vitu ambavyo watu wengi mpaka wanazeeka wanakufa hawaviwazi na mawazo yangu mengi yalikua ya kishetani.Nilikua mtoto wa shetani.Nilikua na roho ngumu na mbaya.Sikua na huruma wala roho ya kusamehe.

Mara nyingi nilikua nakaa peke yangu na ikitokea unanikuta naongea na mtu basi atakua ni mtu mzima na itakua kuna jambo namdadisi.

Nilitaka kumfanya mzee Kipipa awe anaishi kwa kufuata amri zangu mpaka siku kifo kinamuondoa mmoja wetu.Nilitaka kila akinifikiria aogope.Nilitaka akiota ndoto mbaya jina au sura yangu viwepo kwenye hiyo ndoto.Nilitaka kila anapopumua ajutie kosa la kunibaka.Nilitaka alilaani dushe lake lililomponza kuniingilia.

Pamoja na u teenager wangu nilijua bila pesa kisasi kwa mzee Kipipa kitabaki kuwa matamanio daima hivyo nilipanga niwe na pesa na watu wazito nyuma yangu.

Tajiri pekee niliyemjua na niliyetaka kumfanyia umafia ili nijipatie pesa alikua ni mzee Kipipa.

Mtaji pekee niliokua nao katika project yangu ya umafia ilikua ni urembo na akili na mpango wangu wa mwanzo ilikua ni kum seduce mzee Kipipa kimapenzi lakini niligonga mwamba.Kwanza kabisa Mzee Kipipa hakua bwege,alishajua simpendi na hata chakula alikua anapata kutoka nyumba nyingine kwani nilikataa kuendeleza hiyo huduma na kwa mkwara niliomcjimba siku anarudi tena kijijin vilifanya kujisogeza kwangu kwake anione nyoka.

Mbali ya hivyo pamoja na miaka yangu 14 mzee yule alishanikinai na kuniona mbibi na alikua na katoto kengine ka miaka 9 hivi kanakompelekeaga chakula.

Mpango wangu huo ukafeli na nikawa sijui cha kufanya ila ile sauti ya kunitia moyo wa kutokata tamaa juu ya kulipa kisasi ikaendelea.

Kitendo cha mzee Kipipa kuniona simfai tena baada ya kunichezea
kiliongeza kiu ya kisasi na siku moja kwenye uzinduzi wa ile shule yake akiwa mgeni rasmi ni mzito mmoja serikalini huku waandishi wa habari,wafanyabiashara wakubwa wa Dar na vigogo mbalimbali wakiwa ni wageni waliohudhuria nilipata Plan B ya mpango wangu.

Viongozi wa wilaya,kata na kijiji walikuwepo kushuhudia ufunguzi wa shule kubwa ya boarding ya wasichana.Mzee Kipipa na mkewe na watoto wao walikuwepo.

Yule mjukuu wa ulaya niliyeambiwa nimefanana nae alikuwepo na nilimtambua baada ya kila aliyekuwa karibu yangu kusema tumefanana sana sura kasoro umbo yeye ni flat screen.

Kabla ya kukaribishwa mgeni rasmi mzee Kipipa alitoa hotuba fupi iliyonichefua sana.Alikemea vikali na kuiomba serikali itunge sheria kali dhidi ya watu wanaowanyanyasa watoto kingono.Nilikasirika hadi nikaapa huyu mzee pumzi yake ya mwisho lazima niikatishe mimi.

Katika mkusanyiko ule mimi ndio nilipendeza kuliko ke wote waliokuwepo pale.Wanawake wa Dar waliniangalia kwa wivu huku wanaume zao wakiniangalia kwa uchu na mpaka ule uzinduzi unaisha nilijipatia namba nne za watu wazito kutoka Dar mmoja wao akiwa rafiki na connection nzito ya mzee Kipipa.

Miezi mitatu baadae nilienda Dar kwa kwa ufadhili wa wanaume hao ila kwa kutumia hela zao nilijitafutia makazi na kisha kuwadanganya kuwa nimefikia kwa mjomba na nilifanya hivi kwani nilijua wananiita wanitumie kingono nami sikutaka kutumika.

Kila mmoja bila kujua kuwa kuna wenzie alifadhili maisha yangu mapya ya Dar na kwa vile nilijua wakishanivua nguo sitakua tena na nguvu juu yao nikawa nawachezea mchezo wa sitaki nataka mara nisamehe nimeshindwa kuja mjomba kanikataza nisitoke mara kesho vile mradi tu nilinde mbususu yangu huku nikipanga mipango ya kumuadhibu Kipipa.

Kupitia kigogo na rafiki ya mzee Kipipa nilifanikiwa kumjua mzee Kipipa vizuri.Niliujua uimara na udhaifu wake ulipo na kikubwa nilifanikiwa kujua njia zao za kupiga deal chafu.Nilichofanya ni kuwagombanisha yeye na rafiki yake Kipipa.Devide and rule thing kisha taratibu nikajitoa kwenye hali ya kuonekana ninafaa kwa ngono tu na kujipatia nafasi ya kuwa kwenye business lunches and teas na kupata heshima ya beauty with brain.

Pamoja na kuishia la nne nilipata ofa ya ajira ila nilikataa.Nishaona kuna pesa nzuri zaidi ya mshahara na ndizo nilizozitaka.

Kupitia huyu mzee Kigogo nilipata connection nyingi kubwa na kupitia uadui kati ya huyu mzee nikaanza rasmi kumuadhibu Kipipa.

Baada ya kumsumbua sana Kipipa akaona suluhisho ni kuniua na alifanya jaribio la kuniua mara mbili ila akashindwa.Aliposhindwa kuniua akajaribu kuhamishia miradi yake nchi jirani ila haikua rahisi na mwishowe akanifata tukae mezani tuyaongee.

Akaniomba nihamie nchi za nje na akaniahidi kufadhili kila kitu cha hiyo safari.Kwa ushamba wangu nikadhani ulaya ukishafika tu kule na kuvuta ile hewa yao unakua tajiri.Na pia nilikubali kwenda kuishi ulaya nikiamini kwamba siku nikimuua sitakuwepo nchini kukamatwa.Nikakubali na akanipeleka Sweden katika mji uutwao Göteborg.

Hata hivyo baada ya kukaa kule kwa miezi minne na kuelekezwa mchakato mzima wa maisha ya pale ikiwa ni kutafuta kibabu kinioe ili nipate uppehåltillstånd(resident permitt) au nijipe ukimbizi na pia kwenda kufanya kazi za usafi na kusambaza magazeti asubuhi asubuhi nukaona huyu mbabu Kipipa kaniingiza cha Kike.

Nikawaza deal za hela ndefu wanazopiga kina mzee Kigogo na mzee Kipipa halafu nikalinganisha na future yangu pale Göteborg nikasema huu ni ungese.Narudi bongo.

Mzee Kipipa baada ya kujua nimepanda ndege tu kuelekea Sweden hakutaka tena kunijua kwa heri wala kwa shari na mara chache alizopokea simu yangu alinijibu shit.Nikasema hiiiiiiii kwani huyu mbabu anazani hapo bongo ni ahera siwezi kwenda.?

Siku ya siku nikarudi zangu TZ na kutoka airport moja kwa moja nikaenda aliko mzee Kipipa.Mzee Kipipa alikua kwenye conference fulani kwenye hotel moja kubwa yuko mbele pale anaongea.Nikamuingilia pale huku natembea kisela natafuna big g nimepiga cape ya cardet ya kijani,miwani mikubwa,jeans tight,shati na chini safari buti.

Ma gentlemen waliokuwepo pale walikua wakinishangaa hili lisichana lihuni lihuni kama livuta bangi limefata nini hapa lakini mzee Kipipa yeye alionekana akiniangalia akiwa ameishiwa nguvu asiamini kama jipu lake la kwapa limerudi tena bongo.

Mi sikuwajali wale wavaa suti pale ila nilienda mpaka kama hatua sita na alipo mzee Kipipa kisha nikamwambia kwa sauti ya juu " We gat to talk" akaniambia kanisubiri kule restaurant ila nikamuonyeshea saa then nikamwambia "Kama huna muda naweza hata kuongelea hapa" then nikavuta capelo karibu ya pua then nikaweka mikono mfukoni nikawa namuangalia.

Bila kusema chochote mzee Kipipa alitoka na mie nikamfuata kwa nyuma.Tulivyofika rastaurant kabla hajasema chochote nikamwambia "Hivi wee mzee mbona unapenda sana kucheza na maisha yangu?"
Akatikisa kichwa kisha akasema"Kwanini umerudi Tanzania mapema hivi?".

Nikamwambia"Nikae ulaya kufagia barabara za wazungu halafu kazi ya kukuua nimuachie nani?,

Hakunijibu kitu bali akanitizama tu kisha nikamwambia "Kesho nakuja ofisini kwako kuna kazi nataka mimi na wewe tufanye na sitegemei usumbufu wala janja janja".

Akasema"Niambie unataka kiasi gani cha fedha nikulipe haya mambo yaishe niwe na amani".

Mimi:Huna uwezo wa kunilipa mimi wewe mzee!Hapa ni tufanye kazi tupate
hela hayo ya kukosa amani uliyataka mwenyewe ulivyokua ukinibaka".

Nikasepa zangu na kumuacha pale akiwa anakuna kuna kidevu chake kipana ka sahani ya mama lishe.

NB:Mbali ya kusoma historia yangu ili uburudike nataka ujifundishe kitu hasa wewe mwenye tamaa ya utajiri wa haraka.Ukisikia mtu anakwambia umlipe akuunge freemason huyo ni tapeli.Wanachama wa freemason ni watu ambao tayari ni wazito kwenye jamii.Wanasiasa wakubwa,wana michezo wakubwa,wanamuziki n.k.Hayo mabango ya freemason ni utapeli,hata mimi ukinifata DM kuhusu freemason nitakutapeli.Freemason is by connection na uwe mzito.
Nimejisikka tu kutoa somo ila usitake kujua ni kwa nini wewe jifunze tu usitapeliwe.

Sisy Joannah darling bro Half american wifi ake Leejay49 big broh Gily bestie Equation x Analyse cocastic Dr. Mariposa mshamba_hachekwi Depal Dejane Lucha Darlin Shunie To yeye Glenn Mad Max Lovie Lady an alpha male Unique Flower Chizi Maarifa Palina mshamba_hachekwi dronedrake




My daddy .....
Hii tag list yako ongeza jina langu
 
Nitamega vyote usijali mkuu.
Wewe dada malizia stori kuna mengi nimejifunza ambayo sikuyajua katika umri wangu huu,hasa namna ubakaji unvyoweza kuumiza mwili na saikolojia natamani kujua hatima ya wabakaji wale hasa mzee kipipa,huwezi amini nimesoma mstari kwa mstari stori nzima na nimeanza leo.
 
Kwanza ni mwandishi mzuri, msimulizi mzuri, stori tamu mno mno

Nilichokiona tu imekatishwa sana na najua ni uvivu tu ama unakata tamaa kuona wanasoma wachache. Kwa hili utuwie radhi.

Ila tunasoma wengi, na unavyokawiza ndio watu wanakawia kujaa. Huwezi amini mimi nimeiona since day one ila huwa sisomi stori kipande kipande naboreka kusubiri so huwa nangoja ijae episodes kwanza.

Sasa hapa utaona jinsi ulivyochelewa ndio nimechelewa kusoma[emoji28][emoji28]tangu april nimesoma leo.

Keep it up, ukinirihusu n'taomba nije Pm
 
Niko nimejilaza zangu kitandani nikiwaza na kuwazua huku nikifurahia mvua na radi zinazoendelea huko nje.

Katika kuwaza na kuwazua nikamkumbuka Clepatina wa umri wa miaka saba au nane hivi aliyekua akiishi na baba na mama yake wa kambo huko kijijini.

Mvua hizi zimenikumbusha mbali utotoni ambako kumbukumbu zangu 91% ni za majonzi lkn mapito yaliyotengeneza kumbukuku hizo ndio yamefanya niwe huyu Clepatina niliye leo.Leo hii nikoje?

Leo hii nina miaka 26,nina nyumba 8 Dar za kupangisha na moja Mwanza.Yenye kuleta kodi ndogo ni ile ya 450,000 kwa mwezi.Ni mhitimu wa darasa la 4..Ninaongea kiingeraza kizuri kuliko degree holders wengi(sijatukana ni uhalisia)..Ninapenda tough cars mojawapo ni Jeep..Nina vitabu 6 vya passport vilivyojaa mihuri ya nchi mbalimbali duniani..Ninamiliki shepu halisi la kiafrika na sura nzuri ya upole..Ninamiliki roho mbaya(kwa wanaume na kundi fulan la wanawake)Nina mashamba,viwanja na majengo ya biashara,ninaishi kwenye appartment ya kupangisha..Nina mchumba ninayempenda sana ila ninampenda Yesu zaidi yake.(Ashukuru hili).

Clepatina ni moja ya wanawake wachache duniani wanaojua kwa hakika namna ubongo wa mwanaume unavyofanya kazi.Ukimuona kaka yako au jamaa yako yeyote wa kiume anamrushia manati Clepatina mwambie aache au aendelee at his own risk mana kabla ya kumpokea Yesu moja ya fantansy ya Clepatina ilikua ni kuhakikisha siku moja kabla siku ya kurudi kwa muumba wake haijafika awe amekunywa supu nzuuri isiyokosa ndimu na pilipili na chumvi ya kutosha ya nyama ya DUSHE la mwanaume atakaejipendekeza kwake at the wrong but right time.Moyo wa Clepatina ni mweusi sana juu ya wanaume.

Baba wa Clepatina ni memba mkongwe hapa JF.Ana ID maarufu inayojulika a na wengi.Ni miongoni mwa members wanaochangia madini ya maana humu na kamwe humkuti kwenye nyuzi za upupu. Very cool guy na hakwaruzani na mtu na wengi wenu humu mmetokea kumpenda na kumuheshimu ila JE CLEPATINA ANAMPENDA BABA CLEPATINA?

Hivi nilikua naongelea mvua na radi eeh?Basi bwana jirani na nyumba ya faza tulikokua tukiishi kule bush kulikua na nyumba moja ya mzee mmoja tajiri lililokua likiishi Dar ila alikua akijenga shule kubwa ya boarding kijijini kwetu.Nyumba hiyo alikua akiitumia anapokuja kijijini kusimamia ujenzi wa shule yake.

Familia yetu ndio iliyokua ikiitunza nyumba hiyo anapokua hayupo na anapokua yupo alikua akimpa mama yangu wa kambo pesa kwa ajili ya huduma za kupikiwa na kufuliwa.Step maza alikua anapika kisha anakiweka vizuri kwenye kapu na kunipa nimpelekee uncle mzee Kipipa.

Mchana nilikua nampelekea kule site kunakojengwa shule na jion nilikua nampelekea nyumbani kwake.

Siku moja jion kwenye saa moja kasoro hivi kukiwa bado kuna mwanga kama kawaida mama yangu wa kambo alinipa kapu la chakula nimpelekee mzee Kipipa.

Nikiwa njiani mvua kubwa ikanyesha na kunilowesha chapachapa na kufanya kigauni changu king'ang'anie mwili na kulichora umbo langu kisawasawa.

Nilipofika nyumban kwa mzee Kipipa niligonga hodi akatoka nikanyoosha mkono huku nikipiga magoti kwa heshima ili nimkabidhi kapu la chakula kisha nikimbie kurud nyumban lkn badala ya kupokea chakula aliganda pale mlangoni akiniangalia huku akijilambalamba ulimi na baada ya muda macho yake yakageuka kuwa mekundu na taratibu nikaona suruali yake sehemu ya zipu ikifutuka mpaka ikawa kama mtu ameficha bastola pale.

Hali ya suruali yake ikanikumbusha mjomba wangu wakati naishi na shangazi.Nilikumbuka kuwa suruali au boxer ya mjomba ilikua inakuwaga vile siku alizokuwa akinibaka kule kwa shangazi.
Kengele ya hatari ikalia na sikutaka kupata tena maumivu kama niliyokuwa nayapata wakati mjomba alivyokua akinilalia kunibaka lkn sikuwa na uhakika kama hali ile ya suruali kutuna ni kwa watu wabaya kama mjomba tu au hata wababa wema hupatwa na hali hiyo.

Wakati nawaza hayo huku nikitetemeka kwa baridi na woga wa nilichokiona kwenye ile suruali nikamuona mzee Kipipa akiangalia huku na huko kisha akanishika mkono na kuniingiza ndani kwake.

Sikutaka kuingia ndani kwake ila niliogopa nikikataa atanisemea kwa mama kuwa sina heshima.

Tulivyofika ndani akanipa ishara nikae kwenye kiti,nikakaa huku nikizidi kutetemeka.Muda wote huo ananiangalia huku akijilamba midogo na kutoa tabasamu pana.

Akachukua kapu lenye chakula akaweka mahot pot mezani,akapakua ubwabwa wa mchuzi wa nyama uliopikwa kwa nazi na ufundi wa mama yangu wa kambo.Harufu nzuri nzuri ya kile chakula ikajaa mle ndani.Akanisogezea sahani ile ya ubwabwa iliyojaa minofu ya kuku na kunipa ishara nile.

Kwa njaa niliyokua nayo nilitamani sio kula tu bali kumeza ile sahani nzima nzima ila nilivyokumbuka nilivyochapwa kama mbwa koko siku watoto wa step maza walivyonidaka nakula kwa jirani na jinsi step maza alivyoniambia eti nakula kwa watu ili wamuone mbaya hanipi chakula uroho wote ukaniisha nikakataa kwa kutikisa kichwa.

Nilivyokataa mzee Kipipa huku akitumia tone na na tabasamu la kirafik akaniuliza asubuhi umekula nini?Nikamwambia uji na ndiz za kuchemsha.Akatikisa kichwa kwa masikitiko kisha akaniuliza tena mchana umekula nini?Sikumjibu kuwa sijala kitu bali niliinamisha kichwa changu chini.Akaniuliza mama na ndugu zako wamekula nin mchana?Nikamjibu sijui maana nilitumwa sokoni nikauze ndizi.Akatikisa tena kichwa mithili ya mtu anayenihurumia kisha akaniuliza tena "jion hii umekula nin au utakula nin?' sikutaka kumjibu kuwa sijala bado na sina uhakika kama nitakula au la mana siku mdomo uliponiponza nikamhadithia mtu kuwa mama ananinyimaga chakula nilichofanywa achen tu so nikainamisha zangu kichwa chin mambo yasiwe mengi.

Yule mzee akaniuliza tena mama na ndugu zako wamekula nin jion hii?Nikamwambia mama alivyokupakulia wewe kilichobakia wakala wao chote.

Mzee akatikisa kichwa kwa masikitiko tena kisha akaniambia"Najua mama yako wa kambo sio mtu mzuri na ninajua anavyokutesa hivyo kula usiogope kamwe siwez kumwambia".

Nikayaamin maneno ya mzee Kipipa nikavuta sahani karibu nikaanza kupiga msosi bila hofu.Mzee Kipipa akatoa soda mbil za makopo,moja coca na moja fanta orange akanipa huku akitabasamu.Nikaipokea na kupiga fundo moja refu na nilipoweka kile kikopo chin kilikua tupu,mzee akatabasamu ,nikaendelea na wali kuku na huku akiendelea kunikodolea macho akaniambia"Unafanana sana na mjukuu wangu anayeishi ulaya"
.Niliposikia nafanana na mtoto anayekaa ulaya nilitoa tabasamu moja kubwa la furaha na hapo hapo mzee Kipipa akasema"sijawahi kukuona ukitabasamu ,kumbe ukitabasamu ndo unakua mrembo hivi kama malkia ?

Kusikia nafanana na malkia nikatoa kicheko cha furaha sbb hadithi zote alizonihadithia mama yangu mzazi enzi naishi nae zilimuongelea malkia kuwa ni mwanamke mrembo asiye na mfano.Na moja ya udhaifu wangu ni kusifiwa,napenda kusifiwa.Napenda kusikia watu wakimtukuza Mungu kwa ufundi alioufanya kwangu.

Basi nikaendelea kula na mpaka hapo nilimuona mzee Kipipa ni rafik nikawa nakula huku tukipiga story.Ananiuliza maswali najibu,namuuliza maswali ya kijinga ananipa majibu mazuri yaliyonifurahisha na kisha ikafika wakati akaniuliza "huwa unasali usiku?"
Nikamjibu ndio.Akatabasamu kwa furaha kisha akasema"Vizuri,Huwa ukisali unamuombaga Mungu akufanyie nini?"
Nikamwambia kila siku huwa namwambia Mungu "nataka kwenda kuishi na mama yangu mzazi.".Nikatabasamu kwanza kisha nikaendelea kumwambia,unajua ni siku nyingi sijamuona mama lakini siwez kusahau jinsi alivyo mrembo halafu unajua mama yangu alikua ananipenda sana?.Nakumbuka kuku walikua wakitaga ananikaangiaga mayai...(kufikia hapa machozi yakaanza kunilengalenga.Nikakumbuka nilivyokua kama mboni ya jicho la mama yangu,alivyohakikisha hali kwanza mpaka anibembeleze nile nishibe,alivyokua akinisuka vizuri na kuniogesha na kunivalisha vizuri kila siku.Nikalinganisha na jins mama yangu wa kambo anavyoishi na mim kama anaish na kijbwa koko,nanyimwa chakula,hakuna anayejal nimeoga au sijaoga,nakula peke yangu makombo,na vikiwa vitamu hata makombo sipewi.Nikiumwa wkt mwingine mpaka majiran waingilie kat ndo nipelekwe hospital na nguo navaa chafu zimechoka na mengi mengine).

Kumbukumbu za mama yangu kipenzi zilifanya nilie kwa kwikwi na mzee Kipipa alivyoona hivyo akanisogelea,akanifuta machozi na kunikumbatia nami nikamkumbatia huku nikizidi kulia. .Kumbato la mzee Kipipa lilinipa faraja ya kumbato la baba hasa ukizingatia sikumbuki kama baba yangu keshawahi kunikumbatia au japo kuwahi tu kuongea na mimi kwa upendo kama vile.

Huku akiwa anaendelea kunipa maneno ya faraja,mzee Kipipa alinibeba nikiwa nimemkumbatia na kwenda kunilaza kitandani kwake kisha na yeye kupanda.Nilikuja kujua mzee Kipipa ni mtu mbaya pale alipoanza kuingiza ulimi wake mdomoni mwangu kwani hicho ni moja ya vitendo alivyokuwa akinifanyia mjomba.wangu alipokua akinibaka.

Nikajua wali kuku umeniponza.Nikaparangana nijinasue nikimbie lakini sikuweza,nikataka kupiga yowe akaniziba mdomo,nikamuomba anisamehe aniache asiniumize ila hata hakua anasikia ninachosema sbb mdomo aliuziba.

Basi mzee Kipipa akamaliza jambo lake akawa ananiangalia kwa furaha kisha akaniambia kwa tone na uso wa kikatili"mama yako mzazi najua anapokaa!Ukimwambia mtu yeyote naenda kumuua!Sasa niahidi!!Utasema au hautasema".Akaniachia mdomo huku nikitetemeka nikatikisa kichwa kuwa sitasema.Akasema kwa ukali"toa sauti!!" nikajibu "sitasema".

Akaniangalia kwa muda huku akitabasamu then akasema "Hakika wewe ni malkia,hakuna binti niliyebahatika kumjua aliyeniburudisha kama wewe" kisha akachukua shati lake akanifuta sehemu za siri kisha akaniamuru ninyanyuke anisindikize nyumbani.

Tulipofika nyumbani tukamkuta step maza akitoka jikoni (liko nje) kuelekea ndani.Alipotuona akasimama na bila kuchelewa mzee Kipipa akasema "naona huyu mmemtuma muda mbovu leo hivyo nikaona ni vyema nimsindikize mana na giza na mvua hiz asije akakutan na watu wabaya njian".

Step maza kusikia hivyo akang'aka kwa hasira.'Yaani kaka huyu mtoto ni ana tabia chafu hujapata kuona.Huwez kuamin ameondoka hapa jua bado linawaka halafu saa hiz kwel ndio anafikisha chakuka?!Natama watu wangejua jins huyu mtoto alivyo na tabia za ajabu labda wangepunguza kusema namnyanyasa!"

Mzee Kipipa akasema" Ni mambo ya watoto tu hayo dada,michezo mingi njiani"

Step maza akanikwapua kwa hasira anipige lakini mzee Kipipa akamzuia asinipige kisha akatoa kibunda cha hela nyingi na kumpatia step maza.

Baada ya kuona zile hela step maza mimacho ilimtoka kwa mshangao kisha akauliza'Hela zote hizi za nin kaka?"
Mzee Kipipa huku akijikuna kuna kitambi akajibu"Unajua dada kwa namna familia hii imenipokea na kunihudumia bila kuchoka nataman kutoa hata zaid ya hiyo kuonyesha jins ninavyowashukuru".

Step maza kusikia hivyo akawa anashukuru mfululizo huku akicheka cheka kama chiz aloona jalala jipya na mzee Kipipa akaaga huku akisisitiza nisichapwe.

Mzee Kipipa alivyopotelea mbali step maza akanitia kwenzi moja safi kisha akanisukumiza nikalale huku akiniambia"Kalale huko mbwa wewe usiyeweza kufika ulikotumwa mpaka upitie kwa wachawi wenzio ukadowee chakula.Na ndio mana hata sijisumbuagi kukupa chakula mana najua unakulaga huko unakoendaga kunisema!Ila waambie hata sijali"

Nikaingia chumbani kwangu kulala.Chumba changu kwa sasa nikiambiwa niingie sitaweza kwa jinsi kilivyokua kinanuka mikojo.Nilikuaga kikojozi.Nikilala lazima niharibu godoro,hasa siku za mvua ndo usiseme.Nilikua nikikojoa hamna wakuniambia nitoe godoro nje wala nini.Nilichokua nafanya ni nikikojoa upande huu kesho nalala upande huu na kesho narud upande ule unakua umenyauka kidogo.

Kile chumba kilikua kinasafishwa siku wakija wageni. tu.Watoto wa step maza walikua wanalala chumba kingine.Siku dingi akiwa kasafiri kama siku hii wanalala chhmban kwa baba na mama.

Ilipofika usiku wa manane mvua iliyokua imetulia ikaanza tena kunyesha ikiambatana na radi na vimulimuli.

Nikaamka na kujikunyata kwa woga maana siku chache radi ilipiga ikaua bibi na mjukuu nyumba ya sita kutoka kwetu.

Nikataman na mim niende kule chumban kwa baba na mama na mim nikalale nao lkn ningeenda na nilivyo mchafu na harufu yangu ya mikojo ningefukuzwa kama mbwa na kipigo juu.

Nikakumbuka enzi naishi na mama yangu,usiku wa radi kama ule nikishtuka na kuogopa alinikumbatia kisha kuniambia nisiogope maana hivyo vimulimuli ni macho ya Mungu yanatupa ishara kuwa tusiogope anatuona atatulinda.

Wakati nawaza haya ghafla nikaisikia sauti ya step maza akiongea kwa ukali akisema huku anahema kwa tabu kwa harufu ya mle chumbani kwangu"Hivi ulijaza maji kwenye mapipa?"
Nikamwambia wakati nataka kujaza uliniambia niende kwanza mashineni nikanunue pumba.Akaniambia" kwa hiyo mapipa hayana maji".
Nikamwambia ndio.Ana mwanae mkubwa wa kiume miaka 11 ila hata kufua nguo zake hawez mim mdogo wake ndo namfulia.Huyo alikua ni prince Chibonge,hawez chochote zaid ya kula na kunisemelea na yeye ndo expert wa zinakopatikana fimbo nzur za kunichapia.Mdogo mtu rika langu alikua akinipenda na mie nilimpenda ila step maza hakutaka kabisa anipende wala tuwe karibu.Na akitukuta tunacheza nae nilikula fimbo nakuambiwa naendekeza michezo wkt kuna kaz kibao za kufanya.)

Baada ya kusema ndio mapipa hayana maji mama akasogea pale nilipo.Akavuta shingo ya gaun langu kisha akaninyanyua kutoka kitandan na kuniburuza mpaka mlango mkubwa wa kutokea nje ya nyumba kisha akaufungua mlango.Alipofungua tu mlango ikapiga radi kubwa na kwa woga wote tukakimbilia ndani na kufika ndani tu mim nikadondoka chini kwa kutetemeka.Ile radi ikawaamsha wanae huko chumban wakaja wakilia na kumkumbatia kwa woga.Akawatuliza kisha akaniambia ninyanyuke pale chini.Nikanyanyuka kisha akaniambia nitoke nje nikajaze maji kwenye mapipa.Nikamwambia"nitajaza kesho mama".
Hakusema kitu bali alinifata niliposimama akanivuta na kunitoa nje kwa lengo la kunisukumizia huko then afunge mlango arud chumban na wanawe wakalale.

Ila kwa woga wa kufa kama yule mbibi nikamng'ang'ania utadhan nimeng'ang"ania pindo la Yesu.Kila akijaribu kunisukumia nje anakuta nimemganga.Mwishowe kwa hasira aliniwasha kibao nikamuachia ila kila akitaka kufunga mlango arud ndan mim huyu hapa na mim nataka kurud ndani.Radi zinapiga na zinavyopiga ndo nazid kuogopa kuachwa pale nje peke yangu.

Alivyoona namsumbua akaniambia"Wewe si jeuri.Sasa utachagua kujaza maji kwenye mapipa au uondoke hapa uende ukaishi kwa shangazi yako!"Tone na sura ya step maza viliniambia anamaanisha.Kuishi kwa shangaz nilishasema ni bora kufa kuliko kurudi kule ambako mjomba alikua ananibaka halafu nikimsemea kwa shangazi ananichapa.

Unabakwa leo unaumizwa,kesho bado kidonda kibichi unabakwa tena huku mwili umejaa makovu ya fimbo za shangazi.

Nikachagua kujaza mapipa maji nife kwa kupigwa na radi kuliko kwenda kuishi kwa shangazi.Taratibu nikaenda jikon kunakokaa ndoo na mapipa nikatoa ndoo nje,nikazipanga yanakodondoka maji ya bati na kwa vile mvua ilikua kubwa ndoo zikajaa haraka.Nikanyanyua moja nikajitwisha lkn wkt natembea kuelekea jikoni nikayamimine kwenye pipa nikateleza,ndoo ikadondokea kule,maji yakamwagika nikabaki pale chin naugulia maumivu
ya kudondoka.

Step maza ambae muda wote huo bado alikua kasimama pale mlangoni akinitizama kwa chuki akasema"Endelea kujikalisha hapo mvua iishe kabla mapipa hayajajaa ndo utanitambua" kisha akafunga mlango akaingia chumbani kulala na wanae.

Nikiwa bado nimekaa pale chini radi zilizokua zimetulia zikaanza kupiga tena.Safari hii hazikua zinapiga na kulia kama zinavyoliaga kama baruti bali zikawa zinanguruma kama simba mkubwa mwenye hasira halafu zikawa kama zinaenda na kurudi ktk anga ambalo mim niko chin yake halafu kuna saa nikawa nasikia kama ule muungurumo unashuka chini huku vimulimuli vinapiga na kutoa mwanga kama jua la saa saba mchana.Kwa woga kikojozi mie nikajikojolea ila safari hii sio kwenye godoro.

Vimulimuli vilivyozid kupiga nikakumbuka mama yangu aliniambia"Huo mwanga ni macho ya Mungu yanatupa ishara kuwa anatuona tusiogope anatulinda".
Nikapata ujasiri nikasimama huku nikilia nikanyanyua uso wangu mawinguni
nikasema"ASANTE MUNGU..NAJUA UNANIANGALIA .USIACHE KUNILINDA".

Nikanyanyua ndoo yangu ilomwagika maji nikaipeleka ikajae kisha nikachukua iliyojaa,nikajitwisha na kazi ya kujaza mapipa ya maji ikaendelea.

Kila radi zilivyopiga niliogopa lkn vimulimuli vilipowaka nikapata faraja kuwa Mungu ananiangalia na ananilinda.Mapipa yalijaa maji nami nikaingia ndani nikaenda kulala lkn kabla hata usingizi haujanishika vizuri nikaisikia sauti ya prince chibonge ikisema "Mama anasema unalala mpaka saa hiz unaumwa!?Kisha akavuta shuka langu akalitupa chini halafu akasema unapenda kulala lala ndo mana kikojozi iloooh!.Unaitwa huko!"
+++++++++++++++++++++
Jamani eeh mimi sio muandishi,leo ndo mara ya kwanza naandika story,sijioni muandishi ila natamani siku moja kuwa muandishi kama kina Analyse UMUGHAKA DeepPond na wengine wengi humu.
Im just doin this for fun.
Nategemea kukosolewa.
Na kama kuna atakayeburudika itakua poa.
My sis Joannah darling bro Half
american
my friend
Equation
x
Ulipomtaja TU Baba yako nikamkumbuka mshanar Jr!sijui kwanini!?

"Ilikua ya mama mkwe"!! Nahisi kinyaa kinachotokana na ladha ya chumvi mdomoni!!!
 
Kwa nini wanawake ni wanyanyasaji sana wa watoto wasio wao au watu wanaoishi makwao ambao sio ndugu zao wa damu?
 
Back
Top Bottom