Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

Maisha ni kama maji ukiziba huku yanapita huku. Story ya dada cleopatra ina mafunzo mengi, kuna muda unapitia magumu sana kiasi cha kuona kama duniani umekuja kuteseka tuu.

Lakini kamwe Mungu wetu ni mkuu hawezi kumuacha mja wake aibike milele.

Nipo najiuliza hivi kama dada Cleo asingepitia haya mazito leo angekua huyu wa kujaza passport kwa umri huo mdogo aliokuwa nao? miaka 26 passport imejaa mie nina 31 hata passport sina😂😂😂 nikisafiri sana nimeenda hapo NAIROBI na likaratasi la Emergency travel document.

Story hii ina mafunzo mengi mno, tusikate tamaa haijalishi unapitia nini kwenye maisha mengine yanakuja kukufunza na kukujenga.

Cleo asingenyanyaswa kingono sidhani hata shauku ya kumiliki pesa nyingi ili alipize kisasi angekuwa nayo.

Imagine, baba angemtunza kila hitaji angepata kwa wakati, mama angefanikiwa huko South sijui Kenya alipoenda akamrudia mwanae na akaishi kama yai la kuku wa kizungu sidhani kama angekuwa Cleo huyu wa leo.

Napenda sana kusoma kisa cha YUSUPH kwenye biblia " Yusuph alinyanyaswa na kuuzwa utumwani tena na nduguze, cha kustajabisha huko utumwani nako akasingizia na mke wa bosi amembaka akatupwa jela, jela akakutana na watafsiri wa ndoto ambao mojawapo baadae alim-recomend kwa mfalme na ndio ukawa mwanzo wa Yusuph kuwa waziri mkuu"


Maisha yana mengi, mazuri,mabaya na ya kawaida muda wote tuamini katika njia zetu tunazopitia njia za Mungu ni za kushangaza.

Natamani siku moja nikutane na Cleo nipige nae story kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake.
TUISHI!
Ujue nini mkuu.

Huwa naamini naamini ya kwamba Mungu ana uwezo wa kuzuia tusipatwe na lolote baya hivyo lolote baya linapotupata yeye kwa sababu anazozijua huwa anakua ameruhusu litupate akijua tunaweza kuyashinda na pia huhakikisha no mata wat roho zetu haziguswi na huwa anatuandalia tuzo mwishoni.Nadhani unafahamu kuwa ni Mungu aliyeruhusu Ayubu ajaribiwe ila akatoa sharti kuwa roho yake isiguswe.

Mungu wetu ni mwema,anatupenda na kutuwazia mema hata wakati tunapodhani yuko mbali nasi ila ukweli hajawahi kukaa mbali nasi.

Dhahabu ili ing'ae shurti ipitishwe kwenye moto mkali.
Namshukuru Mungu kwa yote,vicheko na hata machozi pia.

Tufanye mchakato nikubless japo visa stamp ya debunga mkuu.🙏
 
Watu wanaandika upuuzi sana
Mizagamuano na mapenzi vimejaa mpaka kero hata tafsida hawatumii
Wale waliokuwa wanafanya kuvutie hawaandiki tena baada ya kuvamiwa
Mada nzuri hawajibu inapelekea watu kuanzisha ujinga ili thread zisonge
Gily
Daah yaani.
Hasa hapo kwenye tafsida very shameful kwa kweli.
Watu makini wamesepa☹️
 
Watu wanaandika upuuzi sana
Mizagamuano na mapenzi vimejaa mpaka kero hata tafsida hawatumii
Wale waliokuwa wanafanya kuvutie hawaandiki tena baada ya kuvamiwa
Mada nzuri hawajibu inapelekea watu kuanzisha ujinga ili thread zisonge
Gily
Naona unamsimanga Johnnie Walker 🤣🤣🤣

Una mada nzuri ushawah weka🤣🤣🤣 hebu nitag kweny hizo mada
 
Mzee Kipipa aliendeleza ufirauni wake hatimae aliondoka kuiona familia yake Dar hakurudi kwa muda mrefu,

Mama wa Kambo alipata ugonjwa wa kupooza, mateso ya Clepatina yaliisha lakini aligeuka kua muuguzi na kuacha shule akiwa darasa la tano,

Baba yake alirejea ila hakukaa sana aliondoka sababu alianzisha familia nyingine huko alipokua,

Mzee Kipipa amerejea ila amekonda sanaaa,

Clepatina amekua binti mzuri, mrefu, umbo namba nane, chuchu konzi, ngozi laini ya kuteleza, macho malegevu, sauti ya kumtoa Nyoka pangoni,
[emoji3][emoji3]

Aseee big up ban mkalimani wangu
 
Back
Top Bottom