Yupi ni mke bora kati ya hawa?

Yupi ni mke bora kati ya hawa?

nadhani mke bora ni yule mwenye subra na ustahilivu, yule asie na kiburi bali utii, upendo wa kweli na heshima kwa mumewe, ndugu, jamaa, marafiki na majirani,

mke bora ni yule ambae anaejitolea kwa moyo wake wote katika kuilinda na kuitunza familia yake kwa kwa wivu mkubwa na kwa hali na mali bila kuchoka wala kukata tamaa,

mke bora yule ambae ana moyo wa msamaha, hajivuni wala kuzira au kukimbia hali ngumu za kifamilia mathalani maradhi, umaskini, madeni n.k
bali hushirikiana na mume wake kwa upendo mkubwa na bidii katika kutafuta suluhisho, urahisi wa malezi na ugumu wa maisha ya kifamilia,

mengineyo ni ya ziada tu gentleman 🐒
 
1. Mke anayekaa nyumbani: Huyu anajitolea muda wake wote kuhudumia familia, kulea watoto, na kuhakikisha nyumba iko sawa kila siku.

2. Mke mwajiriwa: Huyu anafanya kazi na anaingiza kipato cha kusaidia familia. Anaendelea na ndoto zake za kikazi lakini pia anajaribu kusawazisha kazi na maisha ya Familia.

3. Mke aliyeanzishiwa biashara: Huyu anapata uhuru wa kifedha huku akiwa na nafasi ya kujipangia muda wa familia.

Kwa maoni yako, yupi ni bora zaidi na kwa nini?
Naamini kila mmoja ana maoni yake,
Mke bora niyule wanyumbani pekee
 
Mwanafunzi:mwalimu ety kati ya kondoo, mbuzi, na swala kipi kina protein nyingi
Mwalimu:mbona jibu liko wazi kabisa si wote😅
Mwanafunzi:mi naona kama ni kufuga swala nyumbani itakua poa sana
Mwalimu:Simba, Chui, fisi, mamba wakimuon swala wako, atapona kweli? Hivi unajua kibali cha kuchukua swala ni kikubwa sana

Kondoo(mwanamke wa nyumbani)
Mbuzi (mwanamke wa kazini)
Swala(mwanamke mfanyabiashara)
Chaguo ni lako🥶
 
1. Mke anayekaa nyumbani: Huyu anajitolea muda wake wote kuhudumia familia, kulea watoto, na kuhakikisha nyumba iko sawa kila siku.
Huyu ni bora isipo kua bodabda na vijana wahovyo wanaweza wakamla kama atajirahisisha ila ni bora sana na hana changamoto yoyote ngumu ila tuu hakikisha ukikosa hela asiwe na tamaa na awe teyari kulala njaa

2. Mke mwajiriwa: Huyu anafanya kazi na anaingiza kipato cha kusaidia familia. Anaendelea na ndoto zake za kikazi lakini pia anajaribu kusawazisha kazi na maisha ya Familia.
Huyu ni mwanaume mwezako ila ni mke kwa wafanyakazi wenzake na hakuna kitu utafanya hata ukigundua

3. Mke aliyeanzishiwa biashara: Huyu anapata uhuru wa kifedha huku akiwa na nafasi ya kujipangia muda wa familia.
Huyu hana tofauti na madanga yale ya high classic, akijiweza hana haja ya mwanaume na unakua siyo type yake.

Nb.. kama kweli unataka mke oa huyo namba 1
 
Bora ni namba moja.
Hao mbili na tatu huwezi kuona faida ya ndoa hasa kama mwanaume upo vizuri kiuchumi.

Ila yote kwa yote ndoa haina faida kwa mwanaume.
Ndoa inafaida mkuu, hasa ukimpata unaeendana nae/ mnaesikilizana.. ndoa ni tamu sana ukiondoa ubinafsi kichwani
 
1. Mke anayekaa nyumbani: Huyu anajitolea muda wake wote kuhudumia familia, kulea watoto, na kuhakikisha nyumba iko sawa kila siku.

2. Mke mwajiriwa: Huyu anafanya kazi na anaingiza kipato cha kusaidia familia. Anaendelea na ndoto zake za kikazi lakini pia anajaribu kusawazisha kazi na maisha ya Familia.

3. Mke aliyeanzishiwa biashara: Huyu anapata uhuru wa kifedha huku akiwa na nafasi ya kujipangia muda wa familia.

Kwa maoni yako, yupi ni bora zaidi na kwa nini?
Naamini kila mmoja ana maoni yake,
Hapo wote ni wazuri kikubwa ni namna wewe utakavyosimamia sheria au kanuni za familia yako mlizojiwekea ili mwishowe ufurahie ndoa yako.
 
Back
Top Bottom