Yupo anayepewa bila mizinga wala masharti, anakula mpaka anaikinai na anapelekewa bila kuomba. Usilazimishe, wewe sio chaguo lake!

Yupo anayepewa bila mizinga wala masharti, anakula mpaka anaikinai na anapelekewa bila kuomba. Usilazimishe, wewe sio chaguo lake!

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Hali ndivyo ilivyo, hata kwenye urafiki wa kujuana na watu kawaida tu kuna yule mtu hata akijenga nyumba porini bado atatembelewa ila kuna yule aliejenga sehem ya karibu ila hatembelewi mpaka labda kuwe na party na watu hapo wamekuja kwajili ya vinywaji na si kwajili ya mtu. Kuna mtu akikupigia simu utasema upo bize lakini kuna mtu hata ukiwa bize akitaka kukuona utapangua ratiba.

Basi ndivyo ilivyo na kwenye mapenzi, ukiona unalazimisha unatumia kitu flani kimlete badala ya kuja kwajili yako upo katika hali hatarishi endapo huyo mtu una mipango nae ya muda mrefu ukiamini kwamba ndie chaguo sahihi, amini usiamini ile hali ya kumlazimisha sana tena kwa kutumia vitu badala ya utu wako kuna kipindi itakushinda.

Tafuta mnaeendana wote mnatakana ndipo penye raha hapo, hata kama ni vimizinga basi viwe vya kum-spoil kodogo ila bado nafasi ya utu wako iwe pale pale.
 
Vipi ambao hatupewi lakini ni marafiki zetu wa kutupwa kiasi kwamba nikiumwa atakuja kuniangalia mpaka ninapona...just tu ule ushikaji wa karibu sana yaani mnapiga mpaka zile stori na umbea wa ndani kabisa?

Utu...

Ubinadamu....

Upendo....

Is sex everything in a relationship?
 
Yes it is
 
Sawa ila sema scenario hizo ndo rare cases. Maisha fanya unachokiweza Kwa raha zako. Ikiwa kulazimisha haikupi tabu endelea na maisha yako
 
Back
Top Bottom