Yupo wapi CAZ-T mwana wa Komba

aisee yule chibonge aliyeimba nae 'Nakuhitaji' alikuwa ana lips kali kwenye ile video dadeki!
 
wisanga wengure..wisanga wengure....njoo kwangu unachotaka ntakupa, NTAKUPA...hii song ilibamba kinyama
 
Ni jinsi gani
Nijinsi gani tutawini maishani
 
Ni jinsi gani
Nijinsi gani tutawini maishani
mpaka siku tunasema buriani.Ilikua jumapili nikamuona rafaeli amekaa ni juu ya nini, ni juu ya baiskeli, namuliza anaenda wapi, kanambia anaenda feli huko feli ni kwanani, ni kwa lile jitu tapeli,,asa utamuona wapi atakua kwenye meli ndio wapi ndio huko huko feli, tena nikamuona huyo huyo rafaeli anacheza na nani, anacheza na yule dada mary,,namuliza rafaeli hapa ndio feli,,anasema sio hivyo mwenzio unajua nimeharibikiwa na ile baiskeli nategemea kwenda kule ostabei nako huko ntamkuta braza Mtei yeye ndie atakayenipunguzia bei ya spea za baiskeli
 
[emoji106] [emoji106] [emoji2] [emoji2]
 
Na yule Jamaa aloimba "masawe alikuwepo, daud alikuwepo, na huyu mtoto wa hapa nyuma nani huyu,naye alikuwepo.
Yupo wapi?
Nadhani ameshiriki kuingiza sauti ktk kipindi cha tbc1 ubongo kids sina uhakika.
 
Dah, huyu jamaa kitambo sana mwaka 2000. Nimekumbuka mbali sana enzi hizo RFA inanasia FM! Mtu akikuuliza unasikiliza radio gani? Unamjibu "FM". Kwenye geto langu hapakosi mlingoti mrefuuuu niliounga waya ili kutengeneza antenna ya kunasia mawimbi ya FM! Ama kweli zamani (vijijini) raha!
 
Enzi zake hakukua na wakali ndio maana hata nyimbo za kibwege bwege kama hizo zilikua zinapata airtime kubwa
Kila enzi na wakali wake. Ukiiipata album yake na kusikiliza nyimbo zake ndo utajua kama huyo jamaa alikuwa bwege ama lah!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mpaka sasa hakuna mdau aliyeaema uyu jamaa anapatikana wapi
 
Kuna yule mpare alimba sisi ndiyo baba dhao na mama dhao

Sijui yupo wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…