basi tukaagiza masafa pale na kitimoto,tulianza kupata moja baridi moja moto, wakati tunaendelea kidogo tu huyooo akatokea Mzee Urassa,,na ile Land Kruza yake new model ya kisasa power engine 2.4 filling system ya kisasa unaambiwa, ni automatic kuanzia kiti hadi vitasa, basi alikua na laki 3 mfukoni, akajishika kiunoni akatuangalia akatudharau akaingiza mkono mfukoni akatoa pesa akaweka pale mezani kisha akaenda chooni, sisi basi tukaanza kulewa, tukalewa tukalewa Yesu wangu , tulilewa tulilewa tulilewa tumelewa wakaanza kuongezeka ndugu zetu kutoka sehemu mbalimbali za kilimanjaro, marangu, machame,uru,,kishimundu, kibosho, mwika vunjo, mpaka kiboroloni unaambiwa tarakea mpaka huko sehemu za rombo wote pale wakawa wamemiminika,masawe alikuepo, mariale alikuepo, shirima alikuepo, mange alikuepo, lema alikuepo, ndossi alikuepo, mtei alikuepo, asei alikuepo, mama priska alikuepo,,mama manka alikuepo, minja alikuepo, kilua alikuepo, na huyu mtoto anakaa mtaa wa pili nani huyu...chuwa, haha eti chuwa nae alikuepo