PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Alishamaliza, kifungo alipotoka alibadili majina, mara ya mwisho alipanda basi kwenda dar ambako alikuwa anashinda studio akiandaa albam yake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alishamaliza, kifungo alipotoka alibadili majina, mara ya mwisho alipanda basi kwenda dar ambako alikuwa anashinda studio akiandaa albam yake
Aliwahi kuandika haya;Wakuu.
Nimemkumbuka Sana huyu mwamba,,.
Nina muda mrefu sijamuona jamvini ..
Mwenye taarifa zake tafadhari.
Salaam wapendwa katika Malaika wa Mungu na Mungu Mkuu mwenye nguvu.
Wengi wamekuwa wakiniuliza Sana kuhusu ubini wa KISANDU inbox, naomba leo ni jibu.
Baba yangu Mzazi alipoondoka kurudi kwao Marekani alinikabidhi kwa rafiki yake Abdalah Kisandu pale Kahama, SHINYANGA na hivyo Ukoo wa Abdalah Kisandu wakamshauri mama yangu na NDugu zake kuniwekea ubini wa KISANDU kwakuwa wamepewa jukumu la kunilea DJ. DON NALIMISON maana baba yangu hayupo Tena Nchini.
Hivyo tukawa NDugu na Ukoo wa KISANDU pale KAHAMA. Abdalah yeye alikuwa fundi radio tu. Iliibuka mgogoro mwaka 1988 Bwana Abdalah akilaumuwa kupokea mtoto wa mnegro bila IDHINI ya Ukoo wa KISANDU. Kutokana na Hilo nilihamishiwa kijijini kwa baba wa mama yangu na huko nikaanza shule ya msingi 1990 huku nikitumua jina la ubini wa Ukoo wa KISANDU.
Hata hivyo baada ya kumaliza elimu ya msingi jina(Mashaka Kisandu) nililokuwa natumia shule ya msingi akapewa NDugu wa Ukoo wa KISANDU. Nanikazuiwa kulitumia kwa kuwa Mimi sio Ukoo wao. Ndipo nikaanza kutumia jina la ubatizo(DEOGRATIUS, yaani DEOGRATIUS Kisandu) nikiwa Magu Secondary 1997 Walimu wakanizuia kabisa kutumia jina la Kisandu, niliwaambia Ni jina Langu wao wakaniambia tumia jina la baba yako Mzazi achana na Ukoo wa watu watakutaifisha Hilo jina. Nilimwambia Mkuu wa shule baba yangu ndio Ni Raia wa Marekani akija nitamwambia.
Mwaka 1998 baba yangu alirudi TANZANIA nikamweleza kuhusu navyo pata shida ya Ukoo alioniacha. Wakati huo baba yangu nilimjua kwa jina moja tu Curtis. Mzee aliniambia kwakuwa umeandikishwa shule kwa ubini wao wa KISANDU hamna shida hivyo endelea na asikutishe mtu Ila jina Langu liko kwenye Cheti chako Cha Clinic siku yako ya kuzaliwa.
Ukimaliza sekondari takuja nikuchukue uhamie nyumbani(Marekani USA) na nitakuapisha mahakamani na utaanza kutumia jina la Ukoo wako Sasa. Nilipotoka kwa Padre Ricardo Morogoro April 1999 ambako niliishi utawani kwa takribani miezi 8tu nikaingia Kishimba Secondary school KAHAMA SHINYANGA. Ndipo nikaweka jina "Pio" katikati yaani DEOGRATIUS PIO KISANDU nikiwa na lengo baadae nije niwaachie majina yao Ukoo wa KISANDU na Mimi kuwa Pio iliniepuke mgogoro wa majina. Bahati nzuri Padre mmoja alikuwa Mzee Sana (Padre Manoja) akaniambia tumia jina la baba yako akimanisha "NALIMI" ili uachane na hiyo Kisandu yao pia hiyo Pio, mapadre wa fransisikani watakuvurugia maana Ni jina la mtakatifu wao wa Italia (Padre Pio).
Niligoma kabisa. Nilimaliza shule mpaka vyuo kwa jina Hilo. Kumbe Ukoo wa wenye jina la Kisandu wakaunda NDugu yao wakamwita DEOGRATIUS Kisandu hasa kipindi nilipotangaza kugombea Urais wa Tanzania Aug-sept 2012. Nikiwa Katibu wa Bavicha(CHADEMA) mkoa wa Tanga. Lengo ikiwa nikunizima nisitumie ubini wao huo. Tanga nilikuwa mgeni na walipojua huo mgogoro nao wakaona ndio njia yakujipatia vyeo.
Niliwasiliana na Mzee wangu nikamwambia nikaape mahakamani akanikubalia kuondoa Kisandu tu. Sasa nikawa najiuliza jina nimelipromoti halafu nimesomea then niwaachie? Baba yangu aliniambia nisijali. Mimi nikaapa nikaondoa Pio nikaweka jina la baba "NALIMI", (DEOGRATIUS NALIMI KISANDU),Mzee nilipomueleza aliniambia toa kabisa hiyo Kisandu maana ameshajua Kuna mchezo mchafu unachezwa na Ukoo wa KISANDU ili kuniharibia kwa kuwa naonesha njia ya kwenda pa zuri. Mimi sikusikia.
Mwaka feb 2017 baada ya kutoka lokapu ya Polisi Mwanza nilipokamatwa kwa tuhuma ya kuzusha ushoga. Nilipotoka nilimpigia baba kwa laini maalum isiyo trakiwa. Akaniambia achana na jina lao kata passport ya kusafiria njoo nyumbani USA uungane na wenzako na ukifika takupeleka kwa Wanasheria kuapa. Nilimwambia sawa.
Bahati mbaya nikafungwa mwaka 2018 na nilipotoka gerezani Juni 2020 nilibadili jina Mara moja na kuachana kabisa na jina linaloitwa Kisandu. Ndipo nikajibatiza mwenyewe " NALIMISON" nikitohoa kutoka jina la baba yangu la NALIMI. Hivyo nikaua jina utotoni(Mashaka) na nikaua jina la ubatizo (DEOGRATIUS) na Mimi nikatengeneza jina moja(DON NALIMISON). NDugu zangu USA nilipowapa taarifa walifurahi Sana hasa walipoipata Deed Poli ya wakili nilipofanyia marekebisho.
Walinipongeza na kusema Sasa "simamia hapohapo na wakikuvurugia tutatumia CIA kukuokoa maana Hilo ndilo jina lako rasmi". Ukifika Marekani utaendelea hivyo hivyo. Niliwafahamisha NDugu upande wa mama yangu hapa Kahama SHINYANGA, wengine waliunga mkono na wengine walipinga. Mama aliambiwa anipinge lakini NDugu zangu Nchini Marekani waliniambia niwapuuze wote wanaonipinga.
Kwa kifupi kila Jambo Langu nalotumia Ni hili jina Langu DJ. DON NALIMISON. Hivyo, NALIMISON sio baba yangu Bali Mimi ndio jina Langu. Don niongezeko la kunyambulisha jina Langu na kuliboresha kuwa na hadhi ya Kimataifa. Baba yangu Ana baki kuwa "NALIMI" Kazi yangu Ni Mwanamuziki. Sitegemei kupokea baba wa kubumba TANZANIA Wala kutumia Tena majina ya Kitanzania kwani yamenidharirishia utu wangu.
DJ. DON NALIMISON
14 OKT, 2021.
Aksante kwa kunielewa
View attachment 1973973
Yule jamaa nyuzi zake zilikuwa zinachekesha sanaNimemkumbuka huyu jamaa ,Kuna kipindi nilidhani anajielewa nikamfuata PM ili tufanye biashara kwenye mziki wake ,Sasa kwenye maongezi nikaona hamna kitu .
Si siku moja jioni sana asinicheki aanze kunichimba biti kunipeleka mahakamani eti nimemtesa kisaikolojia na kihisia kisa kumpa ahadi isiyotimia 😃😃
Nikamlima block kubwa Ila alikuwa anapiga kwa namba ngeni kila akinikumbuka nikawa sipokei na mwisho akapotea mazima
🙄😌🤓🤓🤓 mbona nilikuwa sijui kuwa kuna thread ya amito bàngo na john makinginya hahahaaa.
Deo alikuwa ni burudani tosha sana, ila baadaye ikawa ni masikitiko kadili siku zilivyoenda🙄😌🤓🤓🤓 mbona nilikuwa sijui kuwa kuna thread ya amito bàngo na john makinginya hahahaaa.
Tutafutie habari zake kama yu-hai au ndo ivo Mwenyezi Mungu kampenda zaidi...Ntaulizia taarifa zake kwao Nyihogo-Kahama.Huyu home boy wangu.
Mbona JF hawana hizo taarifa? Au umeamua kumuua?Deo mbona amefariki mwaka juzi, tumemzika Mwanza Mkolani kwa wazee wake
Namfahamu vizuri, ulizia pale kwao NyahangaChai
Sikujua nape ni mnaijeria.
Ha ha haSikujua nape ni mnaijeria.