Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Cpt Tamim
RodrikRoshan Robart
Metusella seleman kamando
Eugen Maganga
Badru Rwechwengura kajaja
Harry Hans Pope
Zakaria Hans Pope
Hawa ma Luten ndio wahusika na wengineo.nilisoma kitabu Cha uhaini miaka hiyo.wakili wao alikuwa Murtaza Lakha
Kama utakuwa na hicho kitabu naomba link nikisome ama kama utakuwa unajua library yenye hicho kitabu naomba nielekeze.

Shukrani
 
Historia ya serikali ya nchi hii ina Mengi na Mengi hayo hatuyajui.
Kina Hanspope, Maganga, Tamimu na wengine wengi walipanga kumuua na kuipundua serikali ya Mwl Nyerere.

Inadaiwa dereva teksi aliyekuwa akiwasafarisha wapanga mapinduzi kuhudhuria vikao vyao vya Siri alibaini mpango wao na kuripoti kwa vyombo vya usalama.

Muda umeenda Sasa, huyu dereva teksi ni nani? Yupo wapi Sasa? Alilipwa nini na serikali Kama shukurani ya kuinusuru nchi?
Mkuu hapo kwenye Nerere futa andika Nyerere
 
Miaka ya 80 nilikuwepo. Haya yanayovuma leo wapo ambao hawajui
Kwa sasa kuna uhuru wa vyombo vya Habari na taarifa zinasambaa haraka sana na kwa upana kuliko wakati ule. Hivi sasa kijana wa kijijini akiwa na TECNO akapata bando kikitokea kitu mjini atawasimulia wenzie kijiweni, ama wakitoka shambani, na habari ikasambaa kijiji kizima. Wakati ule ulikuwa unasubiri wiki kwa gazeti la Uhuru kufika katika baadhi ya makao makuu ya Wilaya, hivyo ni inawezekana ulikuwepo lkn kutokana na changamoto za upatikanaji wa taarifa hukuweza kujua kilichoendelea huko mjini.
 
Lakini pia tusingekuwa na amani hii.
Kwani nchi zote zenye amani Nyerere alizaliwa humo?. Hata asingezaliwa Tanzania huyo nyerere, nchi hii ingekuwa imesimama ilivvyo, pengine ingekuwa bora zaidi. Inawezekana kuwepo Nyerere ktk nchi hii ndio chanzo cha matatizo yote tuliyonayo Leo. Alizima ndoto/mawazo mbadala ya akina Tuntemeke Sanga, Oscar Kambona, Edwin Mtei etc. Mawazo ya hawa wazalendo na wengineo yangepokelewa, yawezekana leo Tanzania ingekuwa mbali. Ila kwa udikteta/uroho wa madaraka wa Nyerere hawa waliishia kizuizini au kutoroka nchi.
 
Nilikuwa pale Katumba Bar napata Supu na hata ile gari la breweries lilikuwa limemaliza kushusha Bia pale 😂😂🐼
Hongera Mwamba Mimi mjomba mkbwa wangu alikuwa kapten wa ndege za jeshi so najua kila kitu, na uncle mdogo yeye ni retired Komandoo, blessed is the family we thank you God JWTZ is our family hadi sasa, Mimi ndio mjeuri nimepiga kozi Kisha nikawaambia umaskini sitaki dadeki wakaniona chizi sasa hivi wao ni mabubu mi ama free to talk.
 
Ingesababisha ombwe la uongozi pengine Ingekua mapinduzi Kila kukicha na isingetawalika Tena.
"pengine" pengine nikioa sitapata watoto, pengine nikisafiri nitapotea, pengine nikiajiriwa nitaishi masikini, pengine......pengine......achana na hizi pengine pengine vinginevyo tungegoma kujitawala, ona sasa yametukuta.
 
Cpt Tamim
RodrikRoshan Robart
Metusella seleman kamando
Eugen Maganga
Badru Rwechwengura kajaja
Harry Hans Pope
Zakaria Hans Pope
Hawa ma Luten ndio wahusika na wengineo.nilisoma kitabu Cha uhaini miaka hiyo.wakili wao alikuwa Murtaza Lakha
Nadhani wanamtandao walikuja kuwatoa kimaso maso miaka ya 2005 walipoingia kivingine na kuleta maisha bora KWA watz!!!!

Adhma ya wajeda kushika chama ikafanikiwa KWA mgongo wa demokrasia!

Huwa najiuliza hawa wanamtandaor wasingeshika hatam hali ya maisha ya mtz ingekuaje aiseh coz ujamaa ulikua msoto sana kiasi chake!!!
 
Back
Top Bottom