Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Muda umeenda Sasa, huyu dereva teksi ni nani? Yupo wapi Sasa? Alilipwa nini na serikali Kama shukurani ya kuinusuru nchi?

Hatibu Gandhi, au Hatty MacGhee, alikuwa dereva teksi aliyefichua njama ya jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982 nchini Tanzania.

Alizaliwa huko Zanzibar mwaka 1948 na alihamia Dar es Salaam mwaka 1970 ambapo alianza kufanya kazi ya uchukuzi wa umma.

Mwaka 1982, alikuwa akiwasafirisha wapanga mapinduzi kuhudhuria vikao vyao vya siri. Alisikiliza mazungumzo yao na kugundua kuwa walikuwa na mpango wa kumuua Rais Julius Nyerere na kuipindua serikali.

Alichukua hatua ya kishujaa ya kuripoti kwa vyombo vya usalama na kusaidia kuwakamata wahusika na kuzuia jaribio la mapinduzi. Kwa kutambua ujasiri wake, serikali ilimpa tuzo ya cheti cha heshima na gari jipya.

Baada ya tukio hilo, alibadili kazi na kuanzisha biashara yake mwenyewe. Alikufa mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 61.
 
Tofautisha mapinduzi na chaguzi, tunaongelea muktadha wa Nyerere kupinduliwa sio CCM kuondolewa madarakani.
Hakuna njia moja ya kuondosha tawala za kishenzi nimekupa mifano ya U.S.A, France, China, Russia kwa hiyo akili zako za kijinga unafikiri tawala ovu zinaondoshwa kwa sanduku la kura pekee ? Safari ndefu bado kama ndio vichwa vya hivi vimejaa
 
Mapinduzi yakitokea Kila mtu anataka kuwahi fursa ndio maana JPM alivyofariki wakatamani wachukue kiti ila hawakuweza sababu katiba ndio ilikua inafuatwa ila yangekua mapinduzi ungesikia Bashiru kajitangaza Rais, mara Mabeyo naye kapindua, ghafla Samia naye anaunda jeshi la waasi inakua vurugu tupu.

So mapinduzi sio ya kushabikia hata kama tulimchoka Nyerere hali ingekua mbaya zaidi maana madaraka yangebaki bado CCM ila Kwa Wezi zaidi.
Dogo unaendelea kuonesha namna gani ulivyo mpumbavu.

Mabadiliko hayafanywi na watu waoga siasa za kujipendekeza ni za kishenzi
 
Mkuu hii ndio principle kwenye intelligence kwamba haondolewi mtu mpaka ijulikane ombwe litazibwa na nani?

Uganda walimtoa Amin wakapita Marais kama 10, Same to Burundi waliompindua Rwagasore wakapita Marais kibao hapo kati nao ikawa mchezo kupinduana. Na hii ni case kwa nchi nyingi tu stability ilipotea baada ya mapinduzi.

So hapa sipingi serikali kubadilika ila sio kwa mapinduzi maana ombwe linabaki wazi so inakua gombania goli
Mbona unakwepa kutaja France, U.S.A, China, Russia ?
 
Usipolidhibiti Jeshi....kwa nchi zetu za kiafrika basi ujue kila uchao ni mapinduzi tu ......

Hayati JKN anabaki kuwa kiongozi bora kuliko wote Afrika....

Siempre El Commandante JKN,amen[emoji120]
JKN alidhibiti jeshi gani huyu huyu anaye shikilia record ya Rais aliye nusurika kupinduliwa mara nyingi ?
 
Ombe baada ya kifo Cha Mondlane? Ndio na kulitokea vita ya miaka mingi sana almost 15 years vita ilipelekea vifo Million 1....
Mindi you Mondlane hakupinduliwa yalikua mauaji tu, ila case ya Nyerere angepinduliwa well and good kiti angekalia nani JWTZ? TANU? Upinzani kina Kambona? Hayo ndio yangetuletea vita ya miaka nenda rudi.

Tuweke tume huru Rais aingie kwa haki ila mambo ya kupinduana sio ya kushabikia
Dogo mjinga sana hiyo tume huru CCM wakuletee wewe na ukoo wako ?
 
Ndio MAANA bas nyerere alitoa kauli ile kuhusu chadema kama chama makini KUMBE alikua anamaanisha kuwa kipo chini ya pot jasusi sio!!?

Ndio maana chadema ipo imara aiseh ina mizizi mirefu sana!

Nasikia hata kikwete alitishia kuwa akikatwa ataenda chadema na atashinda KUMBE alijua chadema ni kitu gani Aiseh!

Kama mambo yapo hivyo Bas nachelea kusema mnywaji Mkuu wa konyagi wa chadema sio mtu wa kawaida atakua pot huyo!!!
2005 chadema haikua chochote,jakaya alisema ataenda cuf,yule mzee kauzu wa iringa aliyekua katibu mkuu akasema 'anayetaka kutoka CCM,akachungulie kaburi'
 
Hatibu Gandhi, au Hatty MacGhee, alikuwa dereva teksi aliyefichua njama ya jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982 nchini Tanzania.

Alizaliwa huko Zanzibar mwaka 1948 na alihamia Dar es Salaam mwaka 1970 ambapo alianza kufanya kazi ya uchukuzi wa umma.

Mwaka 1982, alikuwa akiwasafirisha wapanga mapinduzi kuhudhuria vikao vyao vya siri. Alisikiliza mazungumzo yao na kugundua kuwa walikuwa na mpango wa kumuua Rais Julius Nyerere na kuipindua serikali.

Alichukua hatua ya kishujaa ya kuripoti kwa vyombo vya usalama na kusaidia kuwakamata wahusika na kuzuia jaribio la mapinduzi. Kwa kutambua ujasiri wake, serikali ilimpa tuzo ya cheti cha heshima na gari jipya.

Baada ya tukio hilo, alibadili kazi na kuanzisha biashara yake mwenyewe. Alikufa mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 61.
Angalia pengine unahadithia habari za mapokezi zisizo na ukweli wote. Jaribio kama hili linapotokea siyo kila kitu kinawekwa wazi. Njama zilijulikana kwa namna nyingine kabisa lakini mambo yote hayakuwekwa wazi ili kulinda mifumo ya usalama ya kukusanya habari na wahusika wake. Watch out!
 
Back
Top Bottom