Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Habari zenu jukwaa la celebrities. Niende kwenye mada hapo juu. Miaka ya mwanzo ya 2000, alikuwepo Msanii mwanafunzi wa secondary ya Wasichana Tabora aitwaye Farida Koshuma. Alikuwa na wimbo uitwao Ofisa au PESA. Akisifia pesa kipindi hicho na sauti nyororo kwelikweli. Nina muda mrefu sijamsikia Msanii huyu na sijui yupo wapi na anafanya nini. Pia sielewi baada ya kumaliza form six kule Tabora alienda wapi. Kama pia yupo mwenye taarifa au picha zake arushie humu.