Yussuf Kagoma, kiungo mahiri wa Singida United aliyemtemesha ulimi James Akaminko

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Jana nimeshuhudia mchezo mzuri sana baina ya Azam na Singida lkn kubwa zaid ni pale kiungo asieimbwa sana Yussuf Kagoma akimfanya atakavyo kiungo wa kimataifa wa Ghana James Akaminko, Kagoma ambaye msimu huu alichezea Geita Gold na kuondoka dirisha dogo, ameingia moja kwa moja kwenye kikosi cha Singida na kuonyesha kuwa yeye ni mwamba hasa.

Akaminko ambaye anasifika kwa utulivu na utawala wa sehemu ya kiungo alishindwa kabisa kabisa kuonyesha utofauti wake na Kagoma kwani Kagoma alimfanya na kumgeuza atakavyo pale kwenye dimba la amani karume mjini Zanzibar.

Hawa ndio wachezaji wanaotakiwa kuchezea Stars na timu kubwa kama Simba au Yanga.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Nilishangaa kwa nini tulimfuata mudathiri tukamuacha huyu fundi Yusuph Kagoma kutoka mkoa wa kigoma.
 
Kagona anakuja vizuri ila Akaminko ni kitu kingine kabisa.
 
Usisahau pia alikuwa anapata na msaada kutoka kwa Ndemla na zile paso zake rula.
 
Performance ni kitu cha muda ila ubora wa mchezaji upo palepale!!, Wachezaji wengi wa Tz hawana muendelezo wa viwango hivyo.
Naunga mkono hoja, kuna dogo alikuwa Dodoma jiji Cleophas Mkandala, alikuwa anaupiga mwingi akikamata dimba anawafunika mpaka wakongwe, kaenda Azam siku hizi mdebwedo, au mfano mwingine Salmin Hoza kabla hajaenda Azam
 
Jana nimeshuhudia mchezo mzuri sana baina ya Azam na Singida lkn kubwa zaid ni pale kiungo asieimbwa sana Yussuf Kagoma akimfanya atakavyo kiungo wa kimataifa wa Ghana James Akaminko, Kagoma ambaye msimu huu alichezea Geita Gold na kuondoka dirisha dogo, ameingia moja kwa moja kwenye kikosi cha Singida na kuonyesha kuwa yeye ni mwamba hasa.

Akaminko ambaye anasifika kwa utulivu na utawala wa sehemu ya kiungo alishindwa kabisa kabisa kuonyesha utofauti wake na Kagoma kwani Kagoma alimfanya na kumgeuza atakavyo pale kwenye dimba la amani karume mjini Zanzibar.

Hawa ndio wachezaji wanaotakiwa kuchezea Stars na timu kubwa kama Simba au Yanga.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
dah,hii battle imenipita, hawa ndo viungo bora wangu ,kwa sasa nbcpl
 
Naunga mkono hoja, kuna dogo alikuwa Dodoma jiji Cleophas Mkandala, alikuwa anaupiga mwingi akikamata dimba anawafunika mpaka wakongwe, kaenda Azam siku hizi mdebwedo, au mfano mwingine Salmin Hoza kabla hajaenda Azam
Aziz Andambwile
 
Kagoma na Ndemla ukiwaangalia ni kama unasikiliza wimbo mzuri kwenye safari barabara tambarareeee
 
Back
Top Bottom