Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Jana nimeshuhudia mchezo mzuri sana baina ya Azam na Singida lkn kubwa zaid ni pale kiungo asieimbwa sana Yussuf Kagoma akimfanya atakavyo kiungo wa kimataifa wa Ghana James Akaminko, Kagoma ambaye msimu huu alichezea Geita Gold na kuondoka dirisha dogo, ameingia moja kwa moja kwenye kikosi cha Singida na kuonyesha kuwa yeye ni mwamba hasa.
Akaminko ambaye anasifika kwa utulivu na utawala wa sehemu ya kiungo alishindwa kabisa kabisa kuonyesha utofauti wake na Kagoma kwani Kagoma alimfanya na kumgeuza atakavyo pale kwenye dimba la amani karume mjini Zanzibar.
Hawa ndio wachezaji wanaotakiwa kuchezea Stars na timu kubwa kama Simba au Yanga.
Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app