Yusuf Manji; kielelezo cha “malaika waliogeuzwa shetani”

Maisha ya fahari, utata na kusikitisha sana.
 
Ila haya maisha. Jamaa nasikia alifanya booonge ya pati baada ya kusikia jiwe amevuta. Unaambiwa jamaa alifurahi utafikiri alihakikishiwa na Allah kwamba atakuwa Hafi ng'oo

..sasa kuna kitu gani cha ajabu hapo?

..Jpm alijaribu kumuua Manji, sasa unashangaa au unalaumu nini Manji kufurahia kifo cha Jpm?

..Yeye Jpm hakuwa akifurahia kuteka, kutesa, na kuua, aliohisi ni maadui zake?

..Kauli ya Jpm kwamba waliokuwa wakishi kama malaika wataishi kama mashetani inakueleza nini?

..Jpm alikuwa binadamu. Kuna watu aliwatendea wema hao lazima walisikitishwa na kifo chake. Jpm pia aliwakosea watu fulani hivyo tusiwashangae waliofurahia kifo chake.
 
Ngoja nikuache kwa muda. Nitakurudia
 
Hadithi hii inatukumbusha ukuu wa MUNGU. Vyote tunavyosumbukia duniani ni bure tu,ni ubatiri tu. Ni vya muda mfupi tu. Unatamba navyo kwa muda mfupi sana.

Kitu ambacho watu wengi hatujifunzi ukuu wa MUNGU ni namna ya kuishi. Matajiri wengi wanaishi kwa wasiwasi sana,wanaishi kwa mashaka sana tofauti na masikini au mwenye ukawaida. Na zaidi matajiri wengi hata viongozi walio matajiri wamedhurumu sana hapa. Wametanya mambo ya kutisha ya kuogofya huko gizani. Lakini MUNGU anawaona. Kwa hiyo wanaishi kwa mashaka hapa duniani hawana Amani na huko mbinguni (kama kuna adhabu) wanatumikia adhabu kubwa.
Tofauti na masikini. Mara nyingi masikini ndie anaefurahia maisha. Ksbb hana baya. Na huko mbinguni pia atafurahia maisha,(kama kuna maisha baada ya hapa). Ukuu wa MUNGU.

Ukuu mwingine wa MUNGU ni kwamba tajiri anakula nyama na masikini anakula nyama pia. Kwa hiyo kilichopo hapa duniani kinacholiwa, MUNGU kawapa wote wakile. Na bahati kubwa masikini wa kijijini huko,pamoja na umasikini wake MUNGU kamuongezea vyakula vya asili na hali ya hewa nzuri ya asili huko kijijini. Na ndio maana masikini wa huko kijijini ana maisha marefu kuliko tajiri huku mjini.
Mkumbuke MUNGU siku za ujana wako na uhai wako
 
Mwandishi ana kalamu nzuri sana ya uandishi
 
Mi naipa heshima hii comment huenda ningeamua kumpongeza msimuliaji nisingeweza Kutumia maneno mazuri kama haya
 
Kauli ya kutoongea na mbwa ilikuwa ya Manji au Hans Pope kwenye mgogoro wa wamiliki wa malori enzi za JK huku Magu akiwa Waziri wa ujenzi
 
Kauli ya kutoongea na mbwa ilikuwa ya Manji au Hans Pope kwenye mgogoro wa wamiliki wa malori enzi za JK huku Magu akiwa Waziri wa ujenzi

mkuu ni story ya kijiweni ambayo kila aliekuwa mbaya wa magu alikuwa anapachikiwa.
 
Uandishi mzuri, ila kumtaja taja Magufuli na kumuelezea sifa zake kwa kupotosha na kuweka kinyongo, yaonesha wazi kuwa wewe ni mtu wa visasi usiyesamehe.
 
Mwandishi nafahamu ulifaudika na mgogoro wa Manji na Mengi.Hebu tufafanuliwe japo kiduchu
Hapana, ni mmoja wa waliokutana na madhila ya Musiba baada ya kupora sehemu yao ya kupatia kipato pale maeneo ya Gerezani karibu na uwanja wa netiboli miaka ya nyuma.

Maisha haya cha muhimu ni kujifunza kunyenyekea hata kama unapata ugumu sana kujishusha na kupokea maumivu ya kile unachofanyiwa na binadamu mwenye pumzi ya Mungu.
 
Nimejifunza kadhaa kwenye uzi huu.
Mosi paragraph ya mwisho nukuu ya huyo mwinjilisti ilifaa kuwa uzi mwingine.

Pili sikuwa na kumbukumbu nzuri kesi ya manji na mengi kumbe aliye shinda ni manji.

Tatu Magufuli aliacha athari kubwa sana hapa nchini athari chana na hasi, atakuwa kwenye ndimi za watu na kalamu za waandishi miaka na miaka, kila mmoja akielezea engo yake vile avyomchukulia na kumdhaania magufuli, wa mabaya ataelezea yake wa mazuri ataelezea yake wa mrengo wa kati kadhalika.

Mwisho jitihada hazizidi kudra, unaweza ukawa na kila aina ya nyenzo lakini kuna jambo dogo litakushinda , kuonyesha binadamu pamoja kujiinua na kujishusha kwake ni mdhaifu kwa wakati wote.

Wapuzike kwa amani wote walio tangulia walio tajwa kwenye uzi huu.
 

..Manji alishughulikiwa ktk kesi ambazo hazikuhusisha vigogo wa Ccm.

..Na hizo ndio kesi ambazo zina mashiko na zingeweza kumtia Manji hatiani, ila tatizo zingewaumiza pia vigogo wa Ccm.
 
..Manji alishughulikiwa ktk kesi ambazo hazikuhusisha vigogo wa Ccm.

..Na hizo ndio kesi ambazo zina mashiko na zingeweza kumtia Manji hatiani, ila tatizo zingewaumiza pia vigogo wa Ccm.
Tuishie hapa
Kila mtu aendelee kufahamu anachokifahamu
 
Jama ana kitabu kipo sokoni bei ni 75k
 
Makonda amechangia pakubwa kifo cha Manji pamoja na kufilisika
Alikuwa anafuata order kutoka kwa Boss Kubwaa ...
Hata kama ni wewe ungefanya aliyofanya Makonda kumfurahisha Boss ..
Boss kubwa alimkausha Manji kiasi kwamba hakuna aliyeamini tajiri amekwisha ... Alifreez account zote za Tsh na US dollar bila kupepesa macho..

Ikawa haitoshi akachukua viwanja vikubwa alivyokuwa akimiliki Chanika, Kigamboni ... Alikuwa na kampuni ya kununua mazao mashambani na kupeleka nje ikafutiliwa mbali ...
Ilikuwa hatari sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…