Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
YUSUFU HAKUKUMBUKA NYUMBANI, HII INAMAANA GANI?
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Moja ya mambo yanayonitafakarisha ni kuhusu kisa cha Nabii Yusufu katika Biblia.
Kisa hiki Leo tutakiangazia katika pembe nyingine tofauti kabisa na vile tulivyozoea kufunzwa Makanisani na nyumba za Ibada.
Muhtasari wa Kisa cha Yusuph.
i. Yusufu ni mtoto wa kumi na moja Kwa Yakobo, Kwa mke aitwaye Raheli/Recho. Kwa mama yake ni mtoto wa Kwanza. Mdogo wake aliitwa Benjamin hawa ni tumbo moja.
ii. Yusufu na nduguye, Benjamin walijikuta Yatima kwani Mama yao, Raheli alifariki wakiwa wadogo.
iii. Yusufu akataka kuuawa, lakini Kwa bahati akauzwa wa Waishmael ambapo walimuuza pia huko Misri.
iv. Yusufu alikuwa mzuri wa uso(Handsome boy) bila Shaka ni kutokana na Mama yake alikuwa mzuri wa uso pia.
v. Yusufu alikuwa mcha Mungu kwani aliyashika mafunzo ya Baba yake.
vi. Kuuzwa Kwa Yusufu ni matokeo ya migogoro ya kifamilia baina ya mke mkubwa na mdogo, Leah na Raheli. Migogoro hii iliathiri pia watoto. Hapa kuna la kujifunza Kwa habari ya kuoa mke zaidi ya mmoja.
vi. Yusufu uzuri wake ulimbeba na kumpa ngekewa ya kuingia kwenye familia ya kifalme Kama Kijakazi.
Vii. Tabia ya Yusufu ikamuinua na kumfanya awe na cheo kikubwa katika nchi ya Misri akiwa Kama Waziri.
Ajabu ni kuwa Yusufu baada ya kutusua kimaisha baada ya miaka mingi Sana.
i. Hakukumbuka Nyumbani
ii. Hakumkumbuka Baba yake, Yakobo.
iii. Hakumkumbuka Mdogo wake, Benjamin.
iv. Hakuwakumbuka ndugu zake, waliochangia Baba, ndio watoto wa Mama yake mkubwa aitwaye Leah, na vijakazi waliozaa na Baba yake.
Je mafanikio ndio yaliyomfanya Yusufu asipakumbuke nyumbani kwao?
Je ni mfumo WA kizamani kwamba mtu akishauzwa na kuwa chini ya utawala mwingine hapaswi kukumbuka nyumbani kwao?
Ndugu zake walipokuja Kwa shida ya njaa wakitafuta chakula, YUSUFU akawatambua yaani akawakumbuka lakini wao hawakumkumbuka/kumtambua.
Sababu ya Jambo hili(Yusufu kuwatambua ndugu zake, lakini wao wakishindwa kumtambua huweza kuwa zifuatazo;
i. Ndugu zake hawakuwa na mabadiliko yoyote makubwa ya kimaumbo na Kihali. Hii ni kutokana bado walionekana kujishughulisha na kazi Ile Ile ya ufugaji tangu walipomuuza ndugu Yao.
Wakati Yusufu yeye alikuwa na mabadiliko ya kiumbo na Kihali. Yusufu wa zamani sio Yusufu wa leo. Sio Yule aliyekuwa akiishi maisha ya kichungi/ufugaji. Leo anaishi Kama mfalme, mavazi yake, chakula chake, Vito vya thamani anavyovaa, mafuta anayopaka, ulinzi n.k
2. Nduguze walimuuza Yusufu Kama mtumwa. Hivyo Kama wangekutana naye wangetarajia kumkuta akiwa Kama mtumwa akiwa kachoka na kachakaa.
Sasa Yusufu walimkuta Kama Mfalme hivyo sio rahisi kumkumbuka.
iii. Yusufu wanayemjua kimamlaka alikuwa mdogo wao hivyo walikuwa wakimtuma enzi hizo. Si mnajua watoto wa mwisho wanavyotumwa tumwa na kaka zao. Sasa huyu waliyekutana naye alikuwa anatuma watumishi na alikuwa na mamlaka hivyo sio rahisi kumtambua.
Hata Nduguze wasingejieleza walipotoka na Kueleza habari za Baba Yao, Yakobo, bado Yusufu angewakumbuka.
Sasa kitu kinachonifanya niandike hivi leo.
Kwa nini Yusufu hakuwakumbuka ndugu zake siku zote tangu atoboe kimaisha mpaka siku ndugu zake walipoletwa na njaa zao?
Swali hili linahekima ndani yake, na kupitia hekima hiyo tunaweza kujifunza mambo kadhaa.
Hii inatuambia kuwa, hata kwenye maisha ya kawaida, mtu anapofanikiwa na kutoboa kimaisha ni rahisi Sana kusahau ndugu zake.
Ni rahisi Sana kusahau kwao.
Kitu pekee kinachoweza kumfanya MTU akumbuke ndugu zake ni shida, majanga yanapotokea, ndugu wanapopiga simu ndio mtu aliyetoboa anakumbuka ndugu zake.
Ni kawaida mtu akifanikiwa kutomfikiria mtu masikini na mwenye shida.
Lakini ni kawaida Kwa mtu masikini kumfikiria mtu tajiri/ndugu tajiri.
Mwenye shida humfuta mganga hiyo ni semi ya wahenga yenye maana katika maisha halisi.
Ndio maana hata matajiri wa leo, Kama ni ndugu yako, usipomkumbusha kumbusha mara Kwa mara sio ajabu akakusahau.
Hata hivyo shida mara nying ndio hukutanisha watu kuliko Furaha au Raha.
Tuishie hapa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Dar es salaam