Yusuph Kagoma kwenda Yanga

Yusuph Kagoma kwenda Yanga

Tsyamatsy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
265
Reaction score
421
Kweli Utopolo wenye akili ni wawili Tu! Kwa hili la Yusuph kugomea kwenda Yanga na jinsi Utopolo wanavyohaha kisa sio Mchezaji bali ni kutaka kutunishiana misuli na Semaji la CAF kweli aliyesema huko wenye akili ni wawili Tu apewe maua yake.

Angalia jinsi mapovu yanavyowatoka midomoni kisa sio Mchezaji bali eti kauli za Semaji la CAF ndio mijitu yote hiyo yanapambana na jeshi la mtu mmoja, loh! Mnatia aibu, mmeshakua sasa, mambo ya mipasho muwaachie Akina Mashauzi na Khadija Khopa.

Kwani suala hilo hamuwezi kuliendesha/ kulishughulikia bila kuita waandishi wa habari? Tutoleeni utoto wenu! Mlikuwa wapi siku zote? Hii inaonyesha Semaji la CAF anawakera kiasi cha kukosa usingizi!

Simba Raha Sana! Jitu moja tu la Simba linawakera! Kwa taarifa yenu hamtutoi relini kwenye mechi zetu za kimataifa, kwani ndio lengo lenu kipindi hili. Aluta continue! Simba mbele Kwa mbele! Kagoma kagoma kuja kwenye vyura!
 
Na kweli yusufu kagoma kwenda Yanga sema tu viongozi wanamlazimisha. Yeye anaipenda Simba
 
Mkuu umeona taarifa ya Yanga ya leo?
Umeona zile nyaraka?
Namaanisha mikataba Yanga Vs FG, Yanga Vs Yusuf Kagoma?
Na dole gumba kaweka siyo saini pekee.
MM nimeona mkataba kati ya Yanga Na FG...sijaona wa kagoma
Hata kama ni hivyo basi kuna loop hole ktk hiyo mikataba inayofanya iwe invalid....kitu kinachompa Kagoma uhuru au haki yy kuwa Simba...
 
Kwa hiyo tunachojadili hapa ni kipi? Umeisikiliza clip ya Mwanasheria wa Yanga? Je wewe umeuona mkataba wake na Simba?
Mnataka wa Simba wa kazi gani? Mkataba ni siri kati ya watu wawili au pande mbili...nyie kuuleta hadharani ni matatizo yenu..na hata FG wakiamua kuwa sue huyo mwanasheria wenu wanaweza why aonyeshe mkataba wao hadharani?
Ndo maana hayo mambo yalikua kwny kamati huko ya usuluhishi...
 
Back
Top Bottom