Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na siku hizi kupata sholarship hata huko uchinani na ujerumani ni mpaka ufanye TOEFIL na hiyo mitihani ya kiinglishi.Na bado tu tunang'ang'ania eti kiswahili kikuzwe zaidi.
Waambie hawa watu!!baba wa watu ha-deserve huu udhalilishaji/ujinga...:mad2:
kiingereza sio ishu kabisaa.
wengi tunabuma buma tu kuhusu hio lugha :confused2:
Waambie hawa watu!!
Makamba ni SecGen wa CCM siyo UN hivyo kujua kiigereza siyo ishu kabisa bana! Kazi yake ni humu ndani kwa ndani self container lol! Akitoka atasindikizwa na wenyewe wenye kukimudu.
u made my day aisee! aaluuuuuuh!Ngeli ni wito wakuu.
HAPA MJADALA UTAKUWA UMEVAMIWA......ni sawa na kusema MBOWE KAFELI MASOMO......au MBOWE ANAMILIKI CLUB BILLICANAS ambapo machangu,bangi,mashoga, unga na UCHAFU WA KILA NAMNA UNAPATIKANA ndiye mwenyekiti wa chama cha siasa....CHAMA HIKI KIKIPATA MADARAKA SI KITARUHUSU NDOA ZA MASHOGA?
Kwa mfano wako ina maana Watanzania wote wakiongea kiingereza basi umasikini wetu utakwisha? Vipi Malawi wengi wanaongea kiingereza mbona bado ni masikini? Tuache kasumba ambayo haitatusaidia kitu chochote. Tumuhukumu Makamba kwa uozo wake wa kutokuwa kiomgozi bora na kuwa wale wanaofuata upepo, sio kwa kuongea lugha ya wageni.
Imekuwa proved kwamba mtoto anayefundishwa kutumia lugha ya mama yake (mother tongue) huelewa zaidi anachofundishwa kuliko kutumia lugha ya kigeni. Ni sawa na Nyang'aus ingawa wanaongea kiingereza lakini hesabu zinawapiga chenga na wengi ni hoe hae zaidi kuliko Watanzania. Ukiangalia kwenye nyanja za kimataifa kuanzia UN na its associated agencies Watanzania wako wengi zaidi kuliko hao Wakenya ambao kila siku wanajisifia kuongea hiyo lugha.
Kiingereza ni lugha, jambo la muhimu ni kwamba kama unataka kufanya biashara na nchi ambazo wanaongea hiyo lugha ni vizuri zaidi kujifunza ili uweze kuwasiliana nao vizuri zaidi vinginevyo tafuta wakalimani. Huweze kupiga hatua ya maendeleo kwa kujua kiingereza peke yake as a language bado kuna mambo mengi zaidi ya hilo. Hata ukienda Uingereza kwenyewe asilimia kubwa ya raia wake hawaki-master kiingereza kuwashinda wasomi kutoka bongo kwenye lugha yao wenyewe, kwa hiyo basi tuwe tuna-balance wakati tunaongelea swala la lugha.
Lete mada zenye akili wewe!!!kwa hiyo unataka ajue kingereza then nn?hao wanaojua hiyo lugha ndo mambumbu wa haja.
Mie toka nimeanza kumjua Yusuph Makamba sijawahi kumsikia akiongea hata neno moja la Kiingereza ila
ni kwamba ni bingwa wa kukariri mistari ya biblia na ya kwenye misahafu..
sasa kuna mtu ananibishia sana anasema jamaa yuko fiti kwenye hiyo lugha ya kiingereza ila hapendi kuitumia tu ... wanaomfahamu vyema mnisaidie maana inawezekana nikawa nabisha bila kufahamu.
Asanteni.
Kupenda kuongea kiingereza ni kuendekeza ukoloni mambo leo, nenda france au germany halafu kajifanye unapenda kuongea kiiingereza ndio utaona kitakacho kutokea,ni vizuri kupenda lugha yetu adimu ya kiswahili so Makamba hana kosa ila anadumisha lugha.Hivyo hivyo Mgosi ongea hata kishambaa tutakuelea kwani wote sisi ni wabantu, kama ni mbwai mbwai halafu ekai mambeza kabisa inywi.
Msimbague mtu kwa lugha au kabila au rangi yake waungwana
Cha kujiuliza ni JEEEEE MWENZETU HANA AKILI KICHWANI?