Katika thread hii nimefaidishwa na CV ya Makamba (Hajui "ung'eng'e")
Nafasi ya watanzania kuongea kiengereza ni tatiza la kihistoria,
Waarabu walipokuja walikitumia kiswahili ktk utawala,biashara,dini,nk. Hivyo walikieneza toka pwani kuelekea bara.
Wajerumani na baadaye Waingereza walipokuja walikuta kiswahili kimeshaenea na kukitumiwa katika sehemu nyingi, hivyo walitumia lugha zao, za kikabila pamoja na kiswahili ktk shughuli zao hivyo kiswahili kikapata fursa nyingine ya kuenea zaidi kuliko ktk nchi nyingine.Hii ndio maana kikawa kinatumiwa zaidi hapa kwetu kuliko kwa hao majirani zetu.
Kiengereza hapa kwetu kwa sasa kinafundishwa zaidi shuleni,wakati mfumo wetu wa elimu tangu tupate uhuru unamatatizo yaliyosababishwa na Nyerere na waliomrithi baadae akina Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete.
Waalimu wetu wengi hawaingii katika fani ya ualimu kwa mapenzi yao,bali huingia kwa kuwa wamekosa pa kwenda. Mfano wanaofaulu kiwango cha juu kidato cha nne huendelea kidato cha tano,ktk vyuo vya ufundi na wale wanaofaulu kiwango cha chini kupangiwa ualimu Grade A ili waje wafundishe watoto wetu primary. Ukiangalia matokeo ya waalimu hao walipokuwa kidato cha nne wengi wao wamefeli kiengereza na hesabu halafu wanakuja kupewa watoto wawaandalie msingi wa kiengereza na hisabati!Tunatarajia nini?
Aidha wanaofaulu kidato cha sita kwa daraja la juu huchagua course mbali mbali km Mass com, sheria,nk. Wale wanaofaulu kwa kiwango cha chini huambulia ualimu ili wakafundishe kidato cha tano na sita. Kwa upande mwengine wanafunzi waliokosa sifa za kwenda chuo kikuu ndio huambulia kwenda kusoma diploma ili wawe waalimu wa kidato cha kwanza mpaka cha nne!Fanya utafiti mdogo tu utagundua wengi walioingia katika ualimu wameingia kwa vile hawakuwa na pakwenda. Mfano humu JF mdau wakati anaomba ushauri wa kutafuta kazi aliambiwa aende akatafute "tempo" ualimu,wakati mwengine mtu anaweza kuambia "kama umekosa chuo basi nenda kasome ualimu!"
Ukiangalia wale wanaoongea kiengereza kizuri leo hii Tanzania wengi wao wamekipata sio kwa kutegemea shule za umma tu,bali walikuwa na njia nyingine mbadala.Hii inaonesha jinsi shule zetu zilivyoshindwa kuwafanya vijana wetu waweze kumudu kiengereza.
Maoni haya sio kuwa nawakandia waalimu wetu,la hasha!Kwani hata mimi ni mwalimu nimewahi kufundisha kwa miaka kumi na moja Dar,Zanzibar na Mbeya.Nimeyashuhudia mengi nilipokuwa nafundisha.Kwani hata miongoni mwetu wakisimulia walipokuwa vyuoni na sekondari walikuwa na tatizo la kiengereza lakini hatimae anafundisha kiengereza,Matokeo yake vijana wanajaa kutafuta tuition kwa ustaadh!
Kujua lugha za wengine ni vizuri ili kuwajua pamoja na kujua utamaduni wao,Mataifa makubwa yaliyoendelea leo hii ambayo hayatumii kiengereza kama yaliyotajwa awali Ujerumani,Japan,nk walikuwa na mikakati maalumu kupitia lugha zao.Aidha mataofa mengine yanayoendelea kama China,Malaysia,India,nk wameamua kutumia lugha zao badala ya kiengereza na ndio maana wanazidi kutauacha mbali.Ingawa wanatumia lugha zao haina maana kuwa hawajifunzi kiengereza bali wanatilia mkazo zaidi lugha zao.Mfano tukiwadarasani huku niliko mwanafunzi mwenyeji kama hajaelewa concept huuliza kwa lugha yao na lecturer hujibu kwa lugha yao.Tunaotumia kiengereza hukodoa macho tu.Aidha mwalimu humruhusu mwanafunzi wa masters kufanya assaignment kwa lugha yao badala ya kiengereza.Kichekesho kinakuja pale tunapowalazimisha kuongea kiengereza katika group discussion!
Karibuni nilikwenda katika maonyesho yao ya biashara na kilimo nikiwa nimeongozana na marafiki zangu ambao nimadoctor wanaofundisha engeneering vyuo vikuu huku,mmoja anatoka Tanzania na mwengine Sierra Lione,wasimamizi wa maonesho walikuwa wanatupiga chenga kwa vile tunaongea kiengereza,baada ya kujitambulisha wale marafiki zangu ndio tulitafutiwa mtu wa kutupatia maelekezo.Bongo mgeni anayezungumza kiengereza inakuwaje?
Kwa mawazo yangu,tunahitajika kufanya mageuzi ya kweli katika mfumo wa elimu.
Ni vyema tujifunze lugha za wengine ili tuweze kuwasiliana nao,na hapa sio kiengereza tu.
Watanzania tunapaswa tujue taaluma na kuwa wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali,lugha baadae,kwani unaweza kuwa mtaalamu kwa mfano katika tiba uliyejifunza China kwa miaka kadhaa na ikawa hujui kiengereza ukaja ukajifunza kwa miezi mitatu tu!Hivyo taaluma kwanza kupitia katika lugha yoyote (hata kikwere kama kipo)lugha baadaye!
Nawasilisha,