Yusuph Manji anakodi Yanga, Mo Dewji anachukua bure Simba

Waswahili utawajua tu!Ndio maana maendeleo hakuna kwa sababu ya uchambuzi wa kiswahili swahili tu
 
Kaka naona kama umechanganyikiwa na hauelewi wala kujua unachojaribu kujitia ujuaji.

Uchumi ni nini na fedha na uhasibu ni nini?

Goodwill is not sth that can be quantified like any tangible asset, na wala c brand name ni ile hali ya let’s say kampuni kama coca na umaarufu wake wote iuze kwa bei ya kutupa au kampuni kama banana wine inunuliwe na giant wine manufacturer kama Diageo kwa bei kubwa kuliko uhalisia hvo ndo aidha vinaleta positive au negative goodwill! Hyo taswira unayoitajka wewe ni brand equity na sio goodwill.


#Jipange
 
Tatizo letu Watanzania "matusi" tumeyaweka mbele. Kisomi na kitaalamu unapombinga mtu huwa tunajenga hoja. Lakini mtu makini hujitahidi kujieleza kwa lugha moja, mtu mwenye kuchanganya lugha ni wazi na bayana kuwa "dhana" anayoijadili haijui.

Uchumi ni nini? Fedha ni nini? Na uhasibu ni nini?
Ukitaka kuyajua haya nenda chuo kikuu uwaulize kwa nini wanatoa shahada ya uchumi, shahada ya masuala ya fedha na shahada ya uhasibu. Lakini pia Jiulize kwa nini Kuna bodi ya wahasibu nchini?
 
Ndiyo. Kaona biashara ya mazao haitoshi sasa anataka kuingia kwenye biashara ya wanyama
ni mpigaji sana yule jamaa, Sikiliza vizuri sana maelezo yake utaona boshen za wazi kabisa
 



Ngwananzengo, wanachama wa timu hizi lazima waanzie mahali fulani.
Hatua ya kwanza kabisa ni kukubali kuwa mifumo waliyonayo sasa haifai tena. Kunahitajika mabadiliko. Hicho ndicho walichokifanya. Baada ya hapo ni kuainisha wafuate mfumo gani kulingana na mazingira yao. Hapo ndio ninyi wataalamu sasa ndio mnapoingia. Fanyeni uchambuzi. Leteni faida na hasara ya mifumo hii mipya ya uendeshaji. Ikiwezekana sio mbaya pia kuonyesha njia, ni wapi wanachama wapite kufikia malengo yao.

Kuwalaumu tu wanachama haitoshi na haisaidii. Kwa mfano kumtaka mwanachama wa kawaida kutoka Mpigwa huko Urambo au hata Tandare Uzuri hapa jijini ajue thamani halisi ya Simba, ni kumtwisha mzigo sui wake!!
 
Sawa kabisa mkuu Baba Kiki nafurahi kwamba umelisoma bandiko na umeelewa. tafashali niambie sehemu ambayo sijatosheleza maelezo nifafanue kwa kina. Mimi nimefanya utafiti mrefu na wa kina juu ya mifumo yote. Nawakaribisha kama mna maswali ya msingi mkuu
 
Simba wanaelewa wanachofanya

Yanga hata hawajui wanafanya nini....wamekurupukaaaaaaa
 
Simba wanaelewa wanachofanya

Yanga hata hawajui wanafanya nini....wamekurupukaaaaaaa
Mkuu labda ungefafanua zaidi. Ni kwa vipi yanga hawajui wanachofanya na Simba wanajua.Fafanua.
 
Hili swala watu wanaliongelea kiushabiki kila mtu akivutia kwake kwa hiyo hata kwa wale wasioelewa kweli wanashindwa kujua yupi ni bora mo au manji
 
Mkuu labda ungefafanua zaidi. Ni kwa vipi yanga hawajui wanachofanya na Simba wanajua.Fafanua.

Mchakato wa Simba umekuwa shirikishi sana na unapelekwa Proffesionally

Wanachama sasa kwa miezi sita wanaingia katika phase ya kupewa elimu

Then mabadiliko ya katiba yatafanyika

Then valuation ya timu pamoja na determination ya share Price itafanyika ndani ya hiyo miezi sita

Jana imekubaliwa kuwa Memorandum of Understanding itasainiwa ndani ya mwezi mmoja kutoa room ya kufanya process zingine.

Simba hakuna conflict of interest.....MO yuko nje ya kamati tendaji ya timu hivyo anatoa room ya process hii kuangaliwa kiumakini bila yeye ku influence decision.

Simba wanaelewa wanachofanya kwa sababu wao ndio walianza hii process..wiki moja baadaye manji kakurupuka na kuita kikao cha dharura pasipo kiongozi yeyote mwenzake kujua ni nini kinaenda kujadiliwa

Simba ilishaanza mjadala wa kubadili mfumo muda wa miaka miwili iliyopita kabla ya mkutano mkuu uliopita ...tofauti na Yanga walioambiwa ndani ya dakika kumi...wakakurupuka na kuanza kushangilia
 
Yanga bana nyie mpeni uyo kwa miaka 10 ndo mtajua faida yenu sisi acha tule bil20 na 49% baada ya iyo miaka 10 ndo mtajua simba iko wapi na nyie mko wapi
 
Ngoja nmpge ng'ombe alie moooo
Ha ha ha
Jangwan ulipita upepo wa vumbi tuu ila leo n upepo wa neema ya ngao ya jamii
Naipenda Yanga
 
Mkuu
1. Sikubaliani sana na IMANI YAKO kwamba Yanga inakurupuka- As a matter of fact mchakato huu ulipendekezwa Yanga 10+ years ago
2. Manji anachoungumza sasa baada ya kuibeba sana Yanga single-handedly ni kuifanya isimame kwa miguu yake. Kuna leo na kesho
3.Mo ananunua timu. Maandalizi ya mchakato wa Simba lazima uwe mrefu kwasababu there's no turning back.
4.Manji anakodisha timu, analeta proposal in no time wenye timu wakikubaliana na dau na muda zinawekwa procedure.
Sasa naomba nikukumbushe
a) Mo amekuja kununua Simba (being a major share holder tena kwa kuuziwa 51% shares at the rate of Tshs 20B ina maana wanasimba wengi hawataweza kuweza kununua atleast 1% ya shares)
b)Mo amekuja na technocrats wake na hata mikataba inajadiliwa kwake (premises) una uhakika gani hana interest
c)Umesahau yaliyotokea kwenye mkutano wa Simba wanachama hawakutaka hata kusikia kuhusu kingine walivyofika kwenye topic ya process. What is the difference?
d)Manji amegharamikia billions kwa ajili a Yanga as a chairman(through up&downs) ; Mo alivyoona timu imeyumba akaenda nunua Africa Lyon. Mbona hamuanzi kuogopa kua atawaambia tumefilisika tugawane mali tuvunje kampuni?
 
Sasa ndio umeandika nini hapa,unatuharibia taaruma zetu,kama una degree yoyote kajichungulie form four ulipata nini!huwezi kusema mtu ananunua hisa 51% kwa billion 20 unasema kapewa bure bora aliekodi?unajua kila kitu unachosikia Mo anaongelea kipo dunia nzima,kasome Company law alafu uniambie alichofanya Manji mpaka sasa wasomi wote wameshindwa kumuelewa maana kwenye form ya partnership hakuna kukodi kwenye share hakuna stahili hiyo,alafu unakuja mbele ya wanaume unaongea ongea utumbo,kama jambo hujui kwani lazima uandike,nyie ndio mnaofanya sisi wasomi wachache tudharaulike kwa upumbavu wenu humu,kaa uliza watu hivi alichofanya Manji na Mo kunatofauti gani au kuna fanana katika kipi,wanaojua mambo watakuja hapa wakupe shule,usikulupuke tena dogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…