Kipaji Halisi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 2,280
- 1,363
Mkuu yes, kuwa meya wa jiji ni lazima kwanza uwe diwani, tena sio kuwa diwani ili mradi tuu ni diwani, lazima uwe diwani wa kuchaguliwa na sio viti maalum!. Masaburi ni diwani wa Kata ya Kivukoni, ambapo mtaa wa Magogoni ni moja ya mitaa yake!.
Kwa kukusaidia tuu, hata kuwa waziri ni lazima kuwa mbunge, ila kuwa Waziri Mkuu, ni lazima uwe mbunge wa kuchaguliwa kutoka majimboni!.
Kiukweli sisi Watanzania ni ignorants mpaka basi, kuna vitu simple mtu alipaswa kuvijua, hatujui!, kuna maswali simple tuu unapata jibu uki google, lakini watu wanauliza!, sitashangaa mtu akiuliza humu eti Kikwete ni rais wa wapi vile?!.
Ndio maana watu wanashinda wana lia lia tuu, kulalamika na kunung'unika, kujiandikisha kupiga kura, hawajiandikishi na wakujiandikisha, hawapigi kura!.
Pasco
Km mtu hajui hata udiwani unapatikanaje hadi umeya...unategemea huyo ajiandikishe kupiga kura?...maana uchaguzi mkuu huku bara unachagua kuanzia diwani..mbunge halafu rais...unakua na kura tatu tofauti mkononi..btw Pasco nina 'idea' ya kufanya short films inayohusu ishu fulani naweza kukuona?
Last edited by a moderator: