Yusuph Mlela: Sijaona tofauti ya filamu zetu na za nje

iron finger

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
358
Reaction score
220
Mwigizaji Mlela anasema anasema tofauti kubwa ya filamu nje yaani Africa, Ulaya na America na zile za bongo ni fedha tu. Wenzetu wanawekeza fedha nyingi kwenye filamu moja tofauti na sisi. Je wewe mdau unaamini maneno yake?

Kwamba kama tukiamua siku moja kuwekeza pesa nyingi katika filamu zetu siku moja Mlela anaweza kuingia katika tuzo za Oscar kupambana na wakina Denzel Washngton au Jammie Fox?

Napata mashaka kidogo mimi naamini tofauti ni kubwa zaidi ya pesa..
 
Tuwekeeni na picha yake tumfahamu, ameongea vapour...
 
Teh Teh ameanza kutumia mihadarati.
 
Of course inaweza kua ni kweli kwa upande mwingine, maana movie nzuri inahitaji bajeti nzurii...hata ukiangalia movie za nje ambazo zimehit sana, cheki bajeti yake. Sikatai kua zipo ambazo wana low budget na bado zinakua nzuri, but nyingi nzuri hua na bajeti ya juu.
Japo kibongo bongo tunaweza kua na bajeti nzuri af wasanii wazuri au wakakosa..so kwetu kila kitu kinapwaya japo mi najua hakuna kitu kinachoshindika kama tukiamua, bongo movie inawezekana one day na sisi tukawa kama Hollywood na Bollywood... ni kua serious tu. Mi ni mpenzi sana na movie za nje na za kibongo kidoogoo sanaa, sio kwamba Dina uzalendo ila naona hakuna jipya na hawako serious hawa wasanii wetu, nawish hata one day director mmoja wa nje ajitolee kufanya movie na hawa wasanii wetu walau waone hata mfano tu koz wao wanachukulia hii fani kama masihara wakati wenzao ndo maisha..
But kuna movie za kibongo na tamthilia ambazo walishadirect wazungu na unaona kabisa kuna utofauti flanii...na kama unafatilia utagundua there is something different, kwa mf. Siri ya Mtungi, and I hope so bajeti yake haikua ya kitoto...
 

tatizo la wasanii wa bongo wanaamini eti kipaji ndio kila kitu wanasahau kuwa Elimu ni kitu muhimu sana, nimedirect wasanii wa kibongo na wakenya! wasanii wa kenya wanajua wanachokifanya, wabongo bado sana.
 
Mlela ndo mwenyekiti wa mtaa gani?
 
Kwamba tofauti kubwa ya filamu nje yaani Africa, Ulaya na America na zile za bongo ni fedha tu ni kauli isiyo sahihi coz' anapozungumzia filamu manake ni zile ambazo zimeshazalishwa kwahiyo tofauti kubwa hapo ni kwamba za kwetu hazina mvuto wakati za kwao zina mvuto!

Tukija sababu za tofauti hiyo ndipo tunaweza kuzungumzia suala la pesa... kwamba nalo lina mchango mkubwa katika ubora wa filamu... ubora wa mahudhui na ule wa kiufundi! However, don' forget kwamba filamu inaweza kuvutia hata kama kuna hatupo vizuri kiufundi (technical wise) na ndio maana hata enzi za VHS, watu bado walikuwa wana-enjoy filamu ingawaje wakati mwingine tulikuwa tunalazimika kutoa kanda kutoka kwenye deki, kurudishia tape kwenye njia yake, then mchezo unaendelea!

Tatizo kubwa la filamu zetu ni stori na directing.... endapo tungekuwa na ma-director wazuri na waandishi wazuri wa script, waigizaji sio tatizo kabisa... kwa aigizaji hawa hawa tulionao tunaweza kutengeneza filamu za kuvutia endapo wanapata waandishi wazuri wa script na directors! Ushahidi wa hili unaweza kuonekana hata kwenye tamthilia ya Siri ya Mtungi... wengi wanaisifia wakati waigizaji wengi hata uzoefu hawakuwa nao hapo kabla lakini kwavile walipata ma-director wazuri, wameweza kuwakilisha uhalisia (moja ya kazi muhimu ya director) na wamefanya tamthilia kuwa mzuri... simply because stori ni mzuri! Nimeshasema mara kadhaa hapa... ukishakuwa na stori mbaya, hata ukichukua A-List Actors kutoka Hollywood, bado filamu itakuwa mbaya tu... kwavile ni wazoefu, wanaweza kuwakilisha uhalisia bila tatizo lolote... pale inapotakiwa kulia, wataonekana wanalia na kwanini wanalia... ikiwa ni kilio cha huzuni au cha faraja! Pamoja na yote hayo, hawataweza kuibadilisha stori mbaya kuwa mzuri coz' ni ready written material unless kama wataamua kuitupa script kapuni na kuanza kuigiza pasipo na script. Kama mlikuwa hamfahamu, hili linafanyika sana kwa Bongo Movie...

Kutokana na ukweli huo, ni kweli hapana shaka endapo Bongo Movie inapata investment ya kutosha na kisha kuzingatia weledi wa kazi, basi wanaweza kufanya kazi vizuri sana... don't think of Oscar Awards! Kukiwa na investment ya kutosha, watakuwa na uwezo wa kununua script zilizoenda shule na watakuwa na uwezo wa kuchukua waongoza filamu wanaoifahamu kazi yao! Tatizo ni pale wanapoingia watu wenye pesa kama Proin lakini bado na wao wanafanya business as usual! Kumbe issue sio pesa peke yake, bali wanatakiwa kuingia kwenye industry watu wanaoifahamu tasnia ya filamu vizuri na kuchukua initiative ya kufanya mabadiliko!
 
Huyu atakua anaotaa ndoto za alinacha😁😁😁😁😁😁
 
tumuache ajifarague tu kwa ujinga wako, siri ya mtungi tupu hawaiwezi....!
 
Kheeee..hawa jamaa bwana yaani wanaona ma movie yao na apocalypto sawa!?

ha ha ha kwa hizi movie zao za "jambazi kuvaa koti refu na miwani nyeusi" mlinzi wa geti kua fyatu" "jini linavuka barabara kwa kucheki kwanza kulia na kushoto" " nguo za kichangudoa ndo wanavaa maofisini" ha ha ha af ndo wajifananishe na movie za.nje....fyatu kama walinzi wao
 
Mwambie wenzake wamesota madarasani, akasome Theatre, acting for stage and screen, Directing, Cinematography, Set designing, Lighting etc ndio aseme hizo pumba. Hajui pesa sio kitu katika filamu, art work matters a lot. Kuna filamu zimetumia pesa nyingi ila mwisho wa siku hewa. Mwambie Mlela ana mawazo ya mtoto anayefikiri matunda yanaota kwenye fridge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…