Yusuph Mlela: Sijaona tofauti ya filamu zetu na za nje

Yusuph Mlela: Sijaona tofauti ya filamu zetu na za nje

Mwigizaji Mlela anasema anasema tofauti kubwa ya filamu nje yaani Africa, Ulaya na America na zile za bongo ni fedha tu. Wenzetu wanawekeza fedha nyingi kwenye filamu moja tofauti na sisi. Je wewe mdau unaamini maneno yake?

Kwamba kama tukiamua siku moja kuwekeza pesa nyingi katika filamu zetu siku moja Mlela anaweza kuingia katika tuzo za Oscar kupambana na wakina Denzel Washngton au Jammie Fox?

Napata mashaka kidogo mimi naamini tofauti ni kubwa zaidi ya pesa..

Labda nimsaidie tofauti chache ambazo haitegemei hela:

1. Vipaji: Kwetu mtu anaingia kwenye uigizaji kwa sababu ya kutafuta umaarufu na pesa; wakati kwa wenzetu ni kipaji. Mfano Ray (Vicent Kigosi), anafaa sana kuwa mtunzi tu lakini sio muongozaji na muigizaji.. ndio maana anaishia tu kusema "pumbaavuuuuuu" na vimaneno vingine visivyoleta tija.. Au Mboto anafaaa kuwa muigizaji lakini sio muongozaji.. n.k. Huu ni mtazamo wangu naweza kupingwa pia..

2. Seriousness na uhalisia: Mtu huku bongo anaigiza movie utafikiri ni igizo la watoto.. Mtu anakomalia kuvaa nguo za bei ghali ili aonekane wakati scene anayoigiza ni ya mtu masikini.. Au unakuta mtu kapiga black na wave kwenye nywele na ndevu kapiga "O" kali wakati anaigiza kama mtu wa kijijini mwenye dhiki.. Au unakuta sister duu kama Irene Uwoya hivi anavaa nguo fupi na ya kutia aibu as if anaenda club tena usiku wa manane then ndio anaenda nayo ofisini.. Au unakuta mtu anajifanya anafanya kazi then anaishia kuchezea mouse tu badala ya kuwa serious na kazi as if ni ukweli.. Au unakuta mtu ni askari then anavaa nguo za kawaida na ofisi yake ni kama benki vile... Au mtu anafungwa jela then selo yenyewe ni kama nyuma ya mlango wa geti tu..

3. Mtu movie inakuwa haina proper editing au basi hata kuangaliwa kwanza na wao wenyewe before haijawa released. Niliwahi kukutana na movie ya kibongo DSTV, ambapo kuna sehemu camera ilicheza na jamaa wakafikiri wameshaizima kumbe bado inachukua tukio.. Then ule upuuzi wote uliokuwa unaendelea ukawa captured na haukuwa removed mpaka movie inaenda kwenye international channel kama Africa Magic. Au unakuta mtu kakosea jina na kumwita msanii mwenzake jina lake halisi badala ya lile la kuiigiza then hicho kipande hakitolewi. Sidhani kama hili linahitaji pesa ni common sense tu..?

4. Sub-titles ndio usiseme, mpaka aibu.. Live ya kuishi inakuwa leave ya kuondoka.. n.k. Kuwapata vijana walio na utaalamu wa editing mfano pale Guardian au wale wa Citizen na Daily News sidhani kama watataka hela ya kununua nyumba..!

5. Movie zote zina wimbo au mandhari ya muziki mmoja tu...

Niwaachie na wadau wengine waongeze kwenye list... but even bila hela bado watu hawajui kuigiza period..!! Wanakalia usharobaro na usista-duuu badala ya kufanya kazi...
 
ha ha ha kwa hizi movie zao za "jambazi kuvaa koti refu na miwani nyeusi" mlinzi wa geti kua fyatu" "jini linavuka barabara kwa kucheki kwanza kulia na kushoto" " nguo za kichangudoa ndo wanavaa maofisini" ha ha ha af ndo wajifananishe na movie za.nje....fyatu kama walinzi wao[/QUOTE

yani ni 100% truth.... wako sharo sana hawa watu
 
Basi hio ya fedha ndo tofauti kubwa ya kwanza,you can't have a low badjet ukategemea filam yako iwe ya kiwango.Kwanza hamnaga hela ya kuwalipa hao wasanii wenye vipaji mnaishia chukua under ground,unategemea nini?
 
24 season ufananishe na hizi za kantangazeee

Weeeeeeee...weee...achaaaa. Kwamba mlela akipewa gunia la dolari anakuwa jack bauer?
Tuacheni masihara sie sote watu wazima japo tumedondosha mikono sweta.

Angalizo..muvi nzuri ni subject ya story nzuri, script nzuri, proper choices za location na ziwe live, extras wa kutosha, actors na actress wazuri kwa maana ya elimu yao uwezo wa kubeba uhalisia, mavazi na customs na mwisho kabisa pesa ya kutosha kufanikisha hayo ikiwemo supporting effects na kamera nzuri mike nzuri na zinazoendana na tukio lenyewe linaloigizwa kwa wakati huo.
 
Kwangu kama angeongea tofauti na hivyo ndio ningeshtuka, hapo bado hujamsikiliza JB na Ray.

Yaani kwa akili yao ni kuwa tukileta production crew ya Hollywood, 35mm basi mambo yatakuwa mambo.

Ni sawa kwa mfano umesikia Longido kuna njaa, alafu anajitokeza mfadhili kumhoji mtendaji "niwasaidie nini kwa haraka" alafu mtendaji akasema "naomba uniletee Lamboghini Veneno Roadster ili niwe nawatembelea wanainchi wangu kwa urahisi (inauzwa dola milioni nne na nusu)....anyway, Mfadhili atabaki ameduwaa mpaka utakapomwambia mimi ni mbongo....then atatabasamu na kusema Oooh I see.

Kifupi ni kuwa wao wenyewe hawajui tatizo ni nini.
 
Tatizo la bongo muvi ni tatizo la kimfumo...hata wamwagiwe mabilioni ya pesa hakuna chochote watakachofanya bila kwanza ya kuandaa mfumo rafiki na jamii ya wasanii na waandaaji wa filamu wanaojua nini maana ya filamu.

Kwa bahati mbaya ni kuwa karibia wote waliopo ndani ya mfumo huu sio watu sahihi wa kujali na kutaka kuona wanafikia kutengeneza filamu zilizo FILAMU...kwa mfano kina JB, Ray na wenzake wengine hawana guts za kususia mfumo uliopo, wa steps na wengine, sasa ni kwa vipi mtu unatengeneza muvi kwa karibu mwaka wa kumi sasa lakini bado huna uwezo wa kukataa kutengeneza muvi za pati one na two, au kutengeneza muvi kila mwezi...na kila wakiulizwa kila siku wanatoa sababu kibao zisizo na maana.

Kwa jamii kama hii inayoshindwa hata kujikomboa kwenye mfumo usio sahihi kwa kuwa tu wanapata pesa za bia mbili na kubadilisha nguo mbili tatu na magari, sidhani kama kuna la maana la kutarajiwa kutoka kwao.

Ukiangalia project kama ya Siri ya Mtungi...ni kweli wametumia pesa nyingi....lakini sio mfano sahihi wa kutumia...ule ni mradi mmoja tu unaojitegemea na hauna uhusiano wa moja kwa moja na kiwanda cha bongo muvi, popote pale anaweza kujitokeza mwenye uwezo na kufanya kama Siri Ya Mtungi...lakini tunahitaji mfumo rasmi ambao utaathiri kwa njia moja ama nyingine kiwanda cha filamu na kufika hadi kwa wasambazaji.

Kwa hiyo Bongo Muvi inahitaji wenye ujasiri wa kifikra wakishirikiana na hao walio ndani, kutafuta njia sahihi ya kufanya filamu, na kama ni pesa basi zije baada ya kupatikana mfumo sahihi unaotambua utendaji sahihi (weledi) kwenye maeneo yote husika, kama Uandishi, Uongazaji, Upigaji picha (cinematograph), Uwezo wa kuigiza n.k.
 
Zaidi ya umalaya na ushoga, hawa bongo movie naona uwezo wao wa akili ni mdogo sana. Wakati wewe unacheza pool kinondoni wenzako wapo university wanasoma sanaa. Mnakuaje sawa hapo?
 
watu wapo kwenye move industry tokea 18 century pum.bavu anaongea pumba
 
kuna siku drogba alicheza uwanja wa taifa baada ya mechi humudi anahojiwa anasema hana tofauti na drogba, simtofautishi mlela na humudi kwa kauli zao
 
Sitaki kuamini.hata kidogo Hollywood ifanane na tanzania,nigeri tu wametupiga bao,wajipange sana,yaani unifananishie rambo na bongo movie?!?
 
Mwigizaji Mlela anasema anasema tofauti kubwa ya filamu nje yaani Africa, Ulaya na America na zile za bongo ni fedha tu. Wenzetu wanawekeza fedha nyingi kwenye filamu moja tofauti na sisi. Je wewe mdau unaamini maneno yake?

Kwamba kama tukiamua siku moja kuwekeza pesa nyingi katika filamu zetu siku moja Mlela anaweza kuingia katika tuzo za Oscar kupambana na wakina Denzel Washngton au Jammie Fox?

Napata mashaka kidogo mimi naamini tofauti ni kubwa zaidi ya pesa..


mavi yake....
 
Duuh amepoteza muda mwingi kwenye fani hii bila kujifunza
 
Back
Top Bottom