Kwamba tofauti kubwa ya filamu nje yaani Africa, Ulaya na America na zile za bongo ni fedha tu ni kauli isiyo sahihi coz' anapozungumzia filamu manake ni zile ambazo zimeshazalishwa kwahiyo tofauti kubwa hapo ni kwamba za kwetu hazina mvuto wakati za kwao zina mvuto!
Tukija sababu za tofauti hiyo ndipo tunaweza kuzungumzia suala la pesa... kwamba nalo lina mchango mkubwa katika ubora wa filamu... ubora wa mahudhui na ule wa kiufundi! However, don' forget kwamba filamu inaweza kuvutia hata kama kuna hatupo vizuri kiufundi (technical wise) na ndio maana hata enzi za VHS, watu bado walikuwa wana-enjoy filamu ingawaje wakati mwingine tulikuwa tunalazimika kutoa kanda kutoka kwenye deki, kurudishia tape kwenye njia yake, then mchezo unaendelea!
Tatizo kubwa la filamu zetu ni stori na directing.... endapo tungekuwa na ma-director wazuri na waandishi wazuri wa script, waigizaji sio tatizo kabisa... kwa aigizaji hawa hawa tulionao tunaweza kutengeneza filamu za kuvutia endapo wanapata waandishi wazuri wa script na directors! Ushahidi wa hili unaweza kuonekana hata kwenye tamthilia ya Siri ya Mtungi... wengi wanaisifia wakati waigizaji wengi hata uzoefu hawakuwa nao hapo kabla lakini kwavile walipata ma-director wazuri, wameweza kuwakilisha uhalisia (moja ya kazi muhimu ya director) na wamefanya tamthilia kuwa mzuri... simply because stori ni mzuri! Nimeshasema mara kadhaa hapa... ukishakuwa na stori mbaya, hata ukichukua A-List Actors kutoka Hollywood, bado filamu itakuwa mbaya tu... kwavile ni wazoefu, wanaweza kuwakilisha uhalisia bila tatizo lolote... pale inapotakiwa kulia, wataonekana wanalia na kwanini wanalia... ikiwa ni kilio cha huzuni au cha faraja! Pamoja na yote hayo, hawataweza kuibadilisha stori mbaya kuwa mzuri coz' ni ready written material unless kama wataamua kuitupa script kapuni na kuanza kuigiza pasipo na script. Kama mlikuwa hamfahamu, hili linafanyika sana kwa Bongo Movie...
Kutokana na ukweli huo, ni kweli hapana shaka endapo Bongo Movie inapata investment ya kutosha na kisha kuzingatia weledi wa kazi, basi wanaweza kufanya kazi vizuri sana... don't think of Oscar Awards! Kukiwa na investment ya kutosha, watakuwa na uwezo wa kununua script zilizoenda shule na watakuwa na uwezo wa kuchukua waongoza filamu wanaoifahamu kazi yao! Tatizo ni pale wanapoingia watu wenye pesa kama Proin lakini bado na wao wanafanya business as usual! Kumbe issue sio pesa peke yake, bali wanatakiwa kuingia kwenye industry watu wanaoifahamu tasnia ya filamu vizuri na kuchukua initiative ya kufanya mabadiliko!