Tatizo la bongo muvi ni tatizo la kimfumo...hata wamwagiwe mabilioni ya pesa hakuna chochote watakachofanya bila kwanza ya kuandaa mfumo rafiki na jamii ya wasanii na waandaaji wa filamu wanaojua nini maana ya filamu.
Kwa bahati mbaya ni kuwa karibia wote waliopo ndani ya mfumo huu sio watu sahihi wa kujali na kutaka kuona wanafikia kutengeneza filamu zilizo FILAMU...kwa mfano kina JB, Ray na wenzake wengine hawana guts za kususia mfumo uliopo, wa steps na wengine, sasa ni kwa vipi mtu unatengeneza muvi kwa karibu mwaka wa kumi sasa lakini bado huna uwezo wa kukataa kutengeneza muvi za pati one na two, au kutengeneza muvi kila mwezi...na kila wakiulizwa kila siku wanatoa sababu kibao zisizo na maana.
Kwa jamii kama hii inayoshindwa hata kujikomboa kwenye mfumo usio sahihi kwa kuwa tu wanapata pesa za bia mbili na kubadilisha nguo mbili tatu na magari, sidhani kama kuna la maana la kutarajiwa kutoka kwao.
Ukiangalia project kama ya Siri ya Mtungi...ni kweli wametumia pesa nyingi....lakini sio mfano sahihi wa kutumia...ule ni mradi mmoja tu unaojitegemea na hauna uhusiano wa moja kwa moja na kiwanda cha bongo muvi, popote pale anaweza kujitokeza mwenye uwezo na kufanya kama Siri Ya Mtungi...lakini tunahitaji mfumo rasmi ambao utaathiri kwa njia moja ama nyingine kiwanda cha filamu na kufika hadi kwa wasambazaji.
Kwa hiyo Bongo Muvi inahitaji wenye ujasiri wa kifikra wakishirikiana na hao walio ndani, kutafuta njia sahihi ya kufanya filamu, na kama ni pesa basi zije baada ya kupatikana mfumo sahihi unaotambua utendaji sahihi (weledi) kwenye maeneo yote husika, kama Uandishi, Uongazaji, Upigaji picha (cinematograph), Uwezo wa kuigiza n.k.