ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema Tanzania yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 60 lakini walipa kodi hawazidi watu milioni 2 jambo ambalo linasababisha watu hao wachache wanaolipa kodi kulazimika kubeba mzigo mkubwa na hivyo wakati mwingine kusababisha malalamiko ambayo kwenye mazingira ya kawaida yangeweza kuepukika
Akizungumza katika wa kikao kazi kilichowakutanisha TRA na viongozi wa wafanyabiashara Tanzania chini ya uratibu wa TPSF kilichofanyika Johari Rotana Hotel jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Julai 18, 2024 Mwenda aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni amesema mkakati alioingianao ofisini kwa sasa ni kuhakikisha namba ya walipa kodi inaongezeka nchini.
Pia soma hapa Tunduma: Rais Samia Awataka Wafanyabiashara Walipe Kodi na Tozo kuepuka mikopo. Asema Haziendi Kwenye Mifuko ya Viongozi
Kamishna Mkuu wa TRA bwana Yusuf Mwenda amewataka Wafanyabiashara wasirubuniwe na maofisa wachache wahuni wa TRA
====
My Take
Population structure ya Tanzania ni Pyramid in shape, tuna kundi kubwa la Vijana ambao sio wazalishaji Bali wategemezi.👇👇
Tunawatu milioni 2 kati ya milioni 62 wanaolipa kodi Tanzania. Sasa Kuna mzigo mkubwa unaobebwa na watu wachache halafu kusapoti zaidi ya asilimia 98 ambao hawalipi kodi na katika hao milioni mbili sio kila mmoja analipa kodi kila mwezi. Hivyo tulikaa chini ili kuona ni jinsi gani tunaweza kurahisisha usimamizi wa ulipaji kodi ili kuvutia walipaji kodi wengi na hata kupunguza baadhi ya viwango ambavyo hawa watu wanazilipa.
Tulishauri tuwe tunakaa kila robo ya mwaka ili kuhakikisha tunafanya assessment ya mazingira ya biashara hasa katika usimamizi wa mambo ya kodi" - Raphael Maganga - Mkurugenzi Mtendaji TPSF