Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema Tanzania yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 60 lakini walipa kodi hawazidi watu milioni 2 jambo ambalo linasababisha watu hao wachache wanaolipa kodi kulazimika kubeba mzigo mkubwa na hivyo wakati mwingine kusababisha malalamiko ambayo kwenye mazingira ya kawaida yangeweza kuepukika
Akizungumza katika wa kikao kazi kilichowakutanisha TRA na viongozi wa wafanyabiashara Tanzania chini ya uratibu wa TPSF kilichofanyika Johari Rotana Hotel jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Julai 18, 2024 Mwenda aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni amesema mkakati alioingianao ofisini kwa sasa ni kuhakikisha namba ya walipa kodi inaongezeka nchini
====
My Take
Population structure ya Tanzania ni Pyramid in shape, tuna kundi kubwa la Vijana ambao sio wazalishaji Bali wategemezi.