Yusuph Mwenda: Kati ya watanzania Milioni 62, wanaolipa kodi ni Milioni 2 tu

Yusuph Mwenda: Kati ya watanzania Milioni 62, wanaolipa kodi ni Milioni 2 tu

Hii nchi ccm itatawala sana sababu ya elimu yetu. Hivi kweli mkuu huelewi anachomaanisha mpaka unamuita mpumbavu? Hujui kwamba tax base ya direct tax inapoongezeka ndo ahueni kwa masikini wanaolipa indirect tax?

We unaambiwa kati ya watu M60 ni M2 tu ndo walipaji wa direct tax, hapo huoni tatizo, unaona anayetaka kutatua hilo tatizo ni mpumbavu, hizo indirect tax zinazolipwa na hoehae zinafutikaje bila kuongeza idadi ya walipakodi wanaolipa direct tax?

Huyu unayemuita mpumbavu akifanikiwa kurasimisha biashara zisizo rasmi kama madalali wa mazao ambao wanapata fedha kudalalia mazao, washereheshaji ambao kila weekend wanapata kazi, watu wa mission town ambao kila siku hapa mjini wanapiga pesa na hawana hata tin number, akifanikiwa kuoneza makampuni PAYE na SDL zikaongezeka, unaona kabisa hilo ni wazo la kipumbavu?
SAMIA ONGEZA TOZO.
Umejenga hoja yako vizuri na umeeleweka, vipi upande wa matumizi? Unapata picha ya uwiano unaolingana? 🤔
 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema Tanzania yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 60 lakini walipa kodi hawazidi watu milioni 2 jambo ambalo linasababisha watu hao wachache wanaolipa kodi kulazimika kubeba mzigo mkubwa na hivyo wakati mwingine kusababisha malalamiko ambayo kwenye mazingira ya kawaida yangeweza kuepukika

Akizungumza katika wa kikao kazi kilichowakutanisha TRA na viongozi wa wafanyabiashara Tanzania chini ya uratibu wa TPSF kilichofanyika Johari Rotana Hotel jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Julai 18, 2024 Mwenda aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni amesema mkakati alioingianao ofisini kwa sasa ni kuhakikisha namba ya walipa kodi inaongezeka nchini.

Pia soma hapa Tunduma: Rais Samia Awataka Wafanyabiashara Walipe Kodi na Tozo kuepuka mikopo. Asema Haziendi Kwenye Mifuko ya Viongozi

Kamishna Mkuu wa TRA bwana Yusuf Mwenda amewataka Wafanyabiashara wasirubuniwe na maofisa wachache wahuni wa TRA

====

My Take
Population structure ya Tanzania ni Pyramid in shape, tuna kundi kubwa la Vijana ambao sio wazalishaji Bali wategemezi.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C9mAfWGtK5h/?igsh=bWlvOTgxeDh5OW9q

Kwani kuna shida gani hapo?
Mbona kati ya Watanzania wengi kuna kakundi ndiyo kamejimilikisha kuitawala nchi kinyume na na matakwa ya walio wengi lakini hamlisemi hilo?
 
Direct tax. Kodi ya moja kwa moja. Indirect tax zinalipwa na watanzania wote. Tax base ya direct tax inatakiwa kuongezeka, hii nchi direct tax inalipwa na watu wachache sana.
Hao walipa direct tax wanawapelekea tu hao wanaolipa indirect tax kwa serikali. Maana nikinunua TV kwa 800k mwenye duka ananisaidia tu kupeleka VAT kwa serikali ila mlipaji hasa ni mimi.

Msiwabeze sana wanunuzi wa mwisho...
 
Indirect tax inalipwa na kila mtu. Kila raia anayefanya manunuzi analipa indirect tax. Huwezi simama ukajitenganisha na wengine kwamba wewe unalipa indirect tax. Hata uliyenunua tv kwake naye anafanya manunuzi. Tumsapoti huyu Yusufu kuongeza wigo wa direct tax.

Wigo wa direct tax ukikua, tukapunguza matumizi mabaya ya fedha hizi indirect tax zinaweza kuwa na unafuu.
 
uyu alowekwa saiv ndo kilaza zaid anashindwa kufkir asume katika hao watanzania 60 milion kuna watoto chin ya umr wanafunz watoto wachanga watalipaj kodi kuna weng ambao awazalish lakn awalip kod direct ila in direct kila mtu analip kod na sio raia tu hat wagen wanaoish ote hap wanalip kod cz kod ipo kweny bidhaa km vocha mafuta maj ht sigara ukinua shat frij tv mrad umepew risit hpo kod imekatwa na ndio mana kuna kitu inaitwa return yn weng wangepew elim ya kod kuna kiwango ambacho ukifnya sana manunuz ukifksha umetunz risit ukiend lipia biashar yko tra na zle risit mfano za frij tv nguo na vtu vng ulivnunua umetunz yle makato yanajumlishwa pia kweny kod yko na retun unapew shid serkl enyew ilitakiw watoe elim ya kod kuanzia shulen ila imefchw fchwa kias kuna watu wanalip zaid cz awana uelewa mfn unaez agiza bidhaa dubai labda km spea used za magar unafunga we unauza jumla unlipia kod bnadarin kweny kontena na ukishusha mzigo dukan kwko unapouuzq kwa jumla hapo pia una mashine ya risit na unalipa kod miez 3 tatu uliokadiliwa unaemuuzia jumla nae akienda kuweka dukan kwake nae analipa kod bidhaa iyo 1 aliolpia aloingiz muuzaj wa jumla then akij mteja wa reja reja nae analpia kod anapoinunua akiituma mkoan labd kweny bas anailipia na serkal inakat kod kwenye kampun ya bus inaosafirisha mizigo pia yan utitir wa kod kwa bidhaa 1 asume walipe kod watu milion 2 wakurungwa wangeagiza ma shanging kila mwaka af mtaan yanatumik ful tym derev ht asahau nyanya sokon anachoma wese wangeyatmbeza 150 kwenye misafara yachome wese kwa kod ya raia milion 2 aache upotoshaj hpo apo kwenye wanaolipa ya wa2 milion 2 tra wengine ambao si waamnf wanakula rushwa kila siku wanalalamikiwa nchi ingeenda ht kukopesheka tusingekopesheka kimataif kwa kod ya wat 2mil
 
Ongea kwa takwimu. Kati ya hao M2 na hao wa kariakoo wamo humo? Afisa kaangalia business tin nchi nzima kakuta ni 2m, wewe unasema business tin ni ngapi?
Madali wote na wengine waliopo mjini na mikoani wanaotengeneza fedha na hawana tin au tin zao ni non business Ndo nawazungumzia.
Strategy za kukusanya mapato ziwe inclusive Kwa kurasimisha sekta ambazo bado hazijarasimishwa kama udalali wa majengo nk lakini jitihada hizo pia ziende sambamba na kuziba mianya ya ubadhirifu wa mapato ya serikali + kuangalia uhalisia , kuweka mifumo mizuri ya kustimulate uchumi , ajira nk
Spending power iongozeke ,hapo ndio tutapiga hatua na si hizi blablaa za kuongeza makusanyo kwa Lundo la mafukara nchini huku matumizi yakiwa ya ovyo na umasikini unaongezeka
Kenya ndio maana imefikia mahala wakaona huu ni Upumbavu mkubwa .

Juzi tu hapa makamishna baadhi wa TRA wamekutwa na kashfa ya ubadhirifu wa bilioni saba na nyingine cash wameficha nyumbani ,akili za wapi hizi ?
 
Indirect tax inalipwa na kila mtu. Kila raia anayefanya manunuzi analipa indirect tax. Huwezi simama ukajitenganisha na wengine kwamba wewe unalipa indirect tax. Hata uliyenunua tv kwake naye anafanya manunuzi. Tumsapoti huyu Yusufu kuongeza wigo wa direct tax.

Wigo wa direct tax ukikua, tukapunguza matumizi mabaya ya fedha hizi indirect tax zinaweza kuwa na unafuu.
Tengenezeni mazingira ya kukuza vipato vya watanzania, biashara ndogondogo haziwezi kukupa mlipakodi hata ufanyaje.
 
Tengenezeni mazingira ya kukuza vipato vya watanzania, biashara ndogondogo haziwezi kukupa mlipakodi hata ufanyaje.
Ndio, Yusufu anapaswa kuona ujumbe huu. Huo mpango wake isiwe ni kuwachukua hoe hae walipe kodi rasmi bali uwe ni kurasimisha sekta zenye vipato na kuongeza usajili wa makampuni yenye uwezo wa kuajiri.
 
Hii nchi ccm itatawala sana sababu ya elimu yetu. Hivi kweli mkuu huelewi anachomaanisha mpaka unamuita mpumbavu? Hujui kwamba tax base ya direct tax inapoongezeka ndo ahueni kwa masikini wanaolipa indirect tax?

We unaambiwa kati ya watu M60 ni M2 tu ndo walipaji wa direct tax, hapo huoni tatizo, unaona anayetaka kutatua hilo tatizo ni mpumbavu, hizo indirect tax zinazolipwa na hoehae zinafutikaje bila kuongeza idadi ya walipakodi wanaolipa direct tax?

Huyu unayemuita mpumbavu akifanikiwa kurasimisha biashara zisizo rasmi kama madalali wa mazao ambao wanapata fedha kudalalia mazao, washereheshaji ambao kila weekend wanapata kazi, watu wa mission town ambao kila siku hapa mjini wanapiga pesa na hawana hata tin number, akifanikiwa kuoneza makampuni PAYE na SDL zikaongezeka, unaona kabisa hilo ni wazo la kipumbavu?
SAMIA ONGEZA TOZO.
Chizi anapotaka kusapoti ujinga ....ww unamjaza mameno kamishina yy kasema watanzania wanao lipa kodi ni m 2 tu sasa sisi tunahoji hizi kodi za kwenye luku,miamala,mafuta ya magati na bidhaa zote sio kodi ??Huyo ni msomi na kapewa ofsi ya serikali kuisimamia anatakiwa aeleze vitu kisomi.Sasa kama mm tu wa la tatu b nimeona huyo kamishina katulisha uongo ww unatetea nn.
 
Ww wa drs la 3B umemwelewa tofauti na mm wa drs la 2C hivyo kila mtu lazima atatoa maoni kutokana na alivyoelewa.
 
Back
Top Bottom