Yusuph Mwenda: Kati ya watanzania Milioni 62, wanaolipa kodi ni Milioni 2 tu

Yusuph Mwenda: Kati ya watanzania Milioni 62, wanaolipa kodi ni Milioni 2 tu

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema Tanzania yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 60 lakini walipa kodi hawazidi watu milioni 2 jambo ambalo linasababisha watu hao wachache wanaolipa kodi kulazimika kubeba mzigo mkubwa

Kwa hiyo huyo kamishna anamaanisha katika watanzania mil 62, wote wana sifa ya kulipa kodi ikiwemo watoto, wazee, watu wasiojiweza n.k?...
 
Labda angesema direct tax ila indirect tax tunalipa wote mfano kwenye luku kila mtu anakatwa kodi, kununua bando la simu unakatwa kodi, kununua soda unakatwa kodi maana VAT ni shift able na tunaoilipa ni watumiaji wote wa mwisho.

So direct tax wanalipa million 2 ila indirect tax wanalipa zaidi ya million 30.

Kingine watu million 62 hawazalishi, mind you zaidi ya 50% ya waTanzania ni under 18 yaani watoto. So ilipaswa takwimu zake ziwe kwenye labor kwamba watu wangapi wanaozalisha hawalipi kodi. Utakuta wenye kazi au biashara ni million 10 pekee so takwimu zinakua tofauti na ukitoa general population
Pamoja na hayo pia kuna tatizo kubwa la unemployment na underemployment
Hii peasant economy ya hii nchi ni tabu na dhiki tu .
Watu wengi wapo vijijini ambapo productivity Yao pia ni ndogo mno + income pia ni ndogo mno .
Yet hata hayo mapato yanayopatikana yanaishia kwenye matumbo ya watu wapumbavu wachache tu na si kwenda kwenye lengo la kuboresha maisha ya raia na kuleta unafuu wa maisha na kutengeneza mifumo ya kuboost uchumi na kipato cha mwananchi ili makusanyo yaongezeke .
Hii nchi ina systemic issues nyingi mno .
Systemic failure ni kubwa kwa hii nchi
 
Anajua kuliko wewe,hajaokotwa huyo amekulia humo TRA
Maofisi ya serikali mengi kuna watu weupe vichwani Mivyeo wanapanda kwa kuangalia miaka tu anayokaa ofisini lakini kichwani unakuta hamna kitu na kazi hajui

Huyu kamishina ni mmojawao
Hamna kitu hapo hiyo statement katoa ni ushahidi kuwa kichwani hamna kitu kwenye maswala ya kodi
 
Sidhani kama kuna sababu ya kulipa kodi ile ya moja kwa moja wakati Rais mwenyewe anaongoza kutumia vibaya pesa ya kodi inayokusanywa!. Hivi inaaingia akilini kweli Rais kufanya ziara ya siku nne akiwa na msafara wa magari yasiyopungua 100?
Kuna faida gani ya kulipa kodi inayoishia kwenye anasa za Serikali? 😡
 
Kwa hiyo huyo kamishna anamaanisha katika watanzania mil 62, wote wana sifa ya kulipa kodi ikiwemo watoto, wazee, watu wasiojiweza n.k?...
Ndiyo wasomi wetu hao wanaopewa mamlaka.Ndo maama mambo yanashindikana kwa sbb wanaplana kwa kutumia vitu ambavyo havipo.TPSF nao wamekuwa vilaza sijui kwanini?wanaongea kama wanasiasa
 
Direct tax. Kodi ya moja kwa moja. Indirect tax zinalipwa na watanzania wote. Tax base ya direct tax inatakiwa kuongezeka, hii nchi direct tax inalipwa na watu wachache sana.
Kama hamjaweka mfumo Bora wakufan ya watu wafanyebiashara na kupata kipati basi mtabaki na wachache.Madini yanasombwa bila kulipa Kodi harafu mnakazaniana vitu vidogo
 
Hii nchi ccm itatawala sana sababu ya elimu yetu. Hivi kweli mkuu huelewi anachomaanisha mpaka unamuita mpumbavu? Hujui kwamba tax base ya direct tax inapoongezeka ndo ahueni kwa masikini wanaolipa indirect tax?

We unaambiwa kati ya watu M60 ni M2 tu ndo walipaji wa direct tax, hapo huoni tatizo, unaona anayetaka kutatua hilo tatizo ni mpumbavu, hizo indirect tax zinazolipwa na hoehae zinafutikaje bila kuongeza idadi ya walipakodi wanaolipa direct tax?

Huyu unayemuita mpumbavu akifanikiwa kurasimisha biashara zisizo rasmi kama madalali wa mazao ambao wanapata fedha kudalalia mazao, washereheshaji ambao kila weekend wanapata kazi, watu wa mission town ambao kila siku hapa mjini wanapiga pesa na hawana hata tin number, akifanikiwa kuoneza makampuni PAYE na SDL zikaongezeka, unaona kabisa hilo ni wazo la kipumbavu?
SAMIA ONGEZA TOZO.
 
Nguvu kubwa ya kudai kodi iendane na usimamiaji wake!
Kama CAG anasema almost 500billion haionekani imeenda wapi alafu hamna mwenye mamlaka anaeuliza, unategemea nini toka kwa wahusika?
Lets get serious here!
 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema Tanzania yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 60 lakini walipa kodi hawazidi watu milioni 2 jambo ambalo linasababisha watu hao wachache wanaolipa kodi kulazimika kubeba mzigo mkubwa na hivyo wakati mwingine kusababisha malalamiko ambayo kwenye mazingira ya kawaida yangeweza kuepukika

Akizungumza katika wa kikao kazi kilichowakutanisha TRA na viongozi wa wafanyabiashara Tanzania chini ya uratibu wa TPSF kilichofanyika Johari Rotana Hotel jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Julai 18, 2024 Mwenda aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni amesema mkakati alioingianao ofisini kwa sasa ni kuhakikisha namba ya walipa kodi inaongezeka nchini.

Pia soma hapa Tunduma: Rais Samia Awataka Wafanyabiashara Walipe Kodi na Tozo kuepuka mikopo. Asema Haziendi Kwenye Mifuko ya Viongozi

Kamishna Mkuu wa TRA bwana Yusuf Mwenda amewataka Wafanyabiashara wasirubuniwe na maofisa wachache wahuni wa TRA

====

My Take
Population structure ya Tanzania ni Pyramid in shape, tuna kundi kubwa la Vijana ambao sio wazalishaji Bali wategemezi.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C9mAfWGtK5h/?igsh=bWlvOTgxeDh5OW9q

Ndiyo maana tunasema mfumo wa kodi siyo rafiki, tumetoa mapendekezo mengi humu ya nini kifanyanyike
 
Analysis ya hovyo!!!!!! Work force, Un employment rates, graduates jobless etc!
 
Waanzishe matumizi ya mobile money kwa kila kitu. Yaani mtu ukae Mwaka mzima bila kushika cash.
Kenya wanatumia huu mfumo wa pochi la biashara. Daladala, machinga,mama ntilie etc wanatumia mfumo huu ndani ya mpesa. Sio lazima ulipe cash. Unatumia application ti kwenye CM yako.Wanakatwa kodi kiduchu sana. Ndo maana uchumi wa kenya unazidi kupaa pamoja na matatizo kibao wanayopitia.
 
Namuunga mkono Yusufu. Apambane kuongeza wigo wa walipa kodi za moja kwa moja(Direct tax), Tukiwa wengi, lets say hata 15M uwezekano wa kupunguza kodi kama za VAT na matozo tozo kwenye bidhaa inawezekana.

Hakuna sababu bibi kizee wa miaka 80 kwenda kununua mkate wa kunywea chai alipie 18% ya kodi kwenye mkate na vijana wapo mtaani wanapiga udalali wa majengo na kodi hawalipi.

Yusufu atafute mfumo, wote ambao anaweza kuwarasimisha awarasimishe. Wenye nguvu tulipe kodi. Atengeneze mazingira mazuri ya kikodi kwa makampuni mapya ya wazawa, vijana waajirike. Nchi ina fursa hii, watawala wakiacha tamaa za kujilimbikizia mali, nguvu ikaelekezwa kwenye nguvu kazi na masoko,tozo na VAT zinaweza kuwa chini sana.
 
Back
Top Bottom